2019 FIFA Women's World Cup

2019 FIFA Women's World Cup

Wananichukiza nimeacha kuangalia mechi zao,yaani mchezaji anafunga goli la ushindi dakika ya 90 halafu havui jezi wakati wa kushangilia (Joke)😂😂😂
Hata wakivua jezi, huwezi kuona miili yao kwani wana nguo za ndani zinazohifadhi vifua vyao.
 
Michezo ya quarter finals za leo imekwisha huku Uholanzi ikiilamba Italia 2-0, na Uswidi nayo ikiilamba Ujerumani 2-1. kama hukuona mashindano haya basi ulikosa uhondo sana kwani timu zote zilicheza vizuri. Burudani zaidi ilikuwa ni ile sheria mpya ya FIFA ya 3 minute cooling break katika dakika ya 30 kwa sababu kulikuwa na joto kali sana uwanjani, kwa hiyo mchezo ukawa unasimamishwa kwa dakika tatu kusudi wachezaji wanywe na kujimwagia maji ya baridi kupooza miili yao.

Mchezo baina ya Uholanzi na Italy ulianza kuonekana mwanzo kuwa Italy iliiemelewa sana. Yule msichana mwenye jina la kingoni yaani Gama alifanya kazi ya ziaza kulinda lango la timu yake ya Italy lakini mwishoni alielemwa, ikafikia mabeki wa Italy kufanya faulo nyingi zilizosababisha kufungwa. Wao wenywe hawakuwa washambuliaji zaidi ya kujilinda tu.



Kwenye mchezo baina ya Ujerumani na Sweden, Ujerumani ilianza mchezo kwa nguvu sana na kuutawala mchezo mzima kabla kibao hakijawageukia. Kwa hiyo Ujerumani iliongoza kwa bao 1-0 katika katika dakika 20 za kwanza kabla Sweden haijasawazisha bao hilo kifundi sana. Hadi kipindi cha kwanza kinaisha Mchezo ulikuwa droo kwa bao 1-1. Baada ya kipindi cha pili kuanza Sweden ikajipatia bao la pili na kuanza kuutawala mchezo. Ujerumani ilijitahdi sana kupata bao la kusawazisha na walifanya kosa kosa nyingi tu, lakini ndiyo hivyo, Sweden ikawafanyia roho mbaya sana hadi kipenga cha mwisho mabao yakabaki 2-1.



Michezo ya nusu fainali itafanyika Jumanne na Jumatano wiki ijayo kama ifuatavyo

1142410
 
Michezo ya quarter finals za leo imekwisha huku Uholanzi ikiilamba Italia 2-0, na Uswidi nayo ikiilamba Ujerumani 2-1. kama hukuona mashindano haya basi ulikosa uhondo sana kwani timu zote zilicheza vizuri. Burudani zaidi ilikuwa ni ile sheria mpya ya FIFA ya 3 minute cooling break katika dakika ya 30 kwa sababu kulikuwa na joto kali sana uwanjani, kwa hiyo mchezo ukawa unasimamishwa kwa dakika tatu kusudi wacheazaji wanywe na kujimwagia maji ya baridi kupooza miili yao.

Mchezo baina ya Uholanzi na Italy ulianza kuonekana mwanzo kuwa Italy iliiemelewa sana. Yule msichana mwenye jina la kingoni yaani Gama alifanya kazi ya ziaza kulinda lango la timu yake ya Italy lakini mwishoni alielemwa, ikafikia mabeki wa Italy kufanya faulo nyingi zilizosababisha kufungwa. Wao wenywe hawakuwa washambuliaji zaidi ya kujilinda tu.



Kwenye mchezo baina ya Ujerumani na Sweden, Ujerumani ilianza mchezo kwa nguvu sana na kuutawala mchezo mzima kabla kibao hakijawageukia. Kwa hiyo katika dakika 20 za kwanza kabla Swedene haijasawazisha bao hilo kifundi sana. Hadi kipindi cha kwanza kinaisha Mchezo ulikuwa droo kwa bao 1-1. Baada ya kipindi cha pili kuanza Swedene ikajipatia bao la pili na kuanza kuutalwa mchezo. Ujerumani ilijitahdi sana kupoata bao la kusawazisha na walifanya kosa kosa nyingi tu, lakini ndiyo hivyo, Sweden ikawafanyia roho mbaya sana hadi kipenga cha mwisho mabao yakabaki 2-1.


Michezo ya nusu fainali itafanyika Jumanne na Jumatano wiki ijayo kama ifuatavyo

View attachment 1142410
Hapa Bingwa ni USA tu. Mfaransa alichofanywa jana atajuta kuandaa haya mashindano. USA wanajua sana.
 
Hapa Bingwa ni USA tu. Mfaransa alichofanywa jana atajuta kuandaa haya mashindano. USA wanajua sana.
Kwa jinsi USA ya sasa inavyocheza, lolote laweza kutokea. Katika michezo ya USA dhidi ya Sweden, Spain na France, walikuwa wanaelemewa sana, na usndindi wao mwingi ulikuwa wa bahati bahati tu. Kwa hiyo matoekao ya mchezo baina ya USA na England, bado ni patapotea, na iwapo watakutana na Sweden tena kwenye fainali, mambo yanaweza kuwa magumu sana kwa USA.
 
USA inazidi kuchanja mbuga ingawa haichezi vizuri sana kuazidiwapinzani wake. Leo imewabugiza England 2-1 ingawa England ndiyo iliyoonekana kucheza vizuri na kuutawala mchezo wote. England itajilaumu sana kwa kukosa penalty iliyopigwa na Steph Houghton katika dakika ya 84 na kupanguliwa na golikipa Alyssa Naeher wa Marekani.



Kwa sasa Marekani inawasubiri Uholanzi na Sweden wajichuje kesho kusudi mmoja wao ndiye apambane na USA siku ya Jumapili. Sweden ilishawahi kufungwa na USA bao 2-0, ila Netherlands haijawahi kufungwa na timu yoyote. Timu zote mbili Netherlands na Swededn ni timu kali sana ambazo zinaweza kuipa USA wakati mgumu sana.sana kama ka
 
Mpira wa leo baina ya Sweden na Uholanzi nao ulikuwa wa burudani sana. Timu zote ziliceza kwa nguvu sana huko katika kipindi cha Kwanza Sweden ilitawala mchezo wote na ilikuwa na kosa kosa nyingi sana kwenye goli la Uholanzi, lakini kipindi kiliisha bila timu hizo kufungana. Katika kipindi cha pili timu zote ziliongeza nguvu na kucheza vuta nikuvute huku zikiwa zinaelekea kulingana nguvu. Mpaka mwisho wa kipindi cha pili bado walikuwa hawajafungana. Hivyo basi wakaingia kwenye dakika 30 za nyongeza. Katika kipindi hicho cha nyongeza, Uholanzi ilikuja juu sana ikatawala mchezo kama vile Sweden ilikuwa imeshachoka sana. Katika dakika ya 99, Uholanzi ikapata goli la kwanza kwa mchezo mzuri sana ulichezwa na Jackie Groenen. Bao hilo liliwamasha tena Sweden wakaanza mashambulizi ya nguvu katika dakika kumi na tano za mwisho lakini hayakuzaa matunda yoyote. Hivyo hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa Uholanzi ilikuwa inaongoza kwa 1-0.



Jumamosi Sweden itapambana na England kutafuta mshindi wa tatu, halafu fainali itakuwa baina ya USA na Netherlands siku Jumapili usikose uhondo.
 
Wananichukiza nimeacha kuangalia mechi zao,yaani mchezaji anafunga goli la ushindi dakika ya 90 halafu havui jezi wakati wa kushangilia (Joke)😂😂😂
Ona jinsi wanavyofurahia goli, kuna wanaovua jezi kama unavyotaka, na kuna wanaokata viuno kiwanjani na miondoko mbalimbali ya kufurahia goli.
 
Kwa wale wliokosa mchezo wa leo baina ya England na Sweden watakuwa walikosa uhondo sana. Mpira wa leo ulikuwa wa nguvu kwa pande zote mbili zikicheza kwa kasi na kwa ufundi kwa muda mrefu sana. Sweden ndiyo iliyoanza kupata mabao mawili katika kipindi cha kwanza. Baada ya muda si mrefu, England ikapata bao la kwanza hivyo hadi kipindi cha kwanza kinaisha Sweden ilikuwa inaongoza 2-1. Kipindi cha pili kilipoanza England iliongeza mashambulizi sana na muda mfupi baadaye wakapata bao ambalo ndilo lingekuwa la kusawazisha lakini VAR ikaonyesha kuwa mfungaji Ellen White alikuwa offside. Kipindi cha pili kilikuwa kigumu kwa pande zote mbili ingawa England ilionyesha kuwaelemea Sweden. Hata hivyo hakukuwa na mabadiliko yoypote ya magoli hadi kipindi cha pili kinakwisha. Hivyo basi Sweden iliibuka kuwa mshindi wa tatu wa 2019 FIFA Women's World Cup baada ya kuifunga England 2-1.

 
Leo USA tunanyanyua kwapa(kubeba kombe la dunia)
 
Haya tena, mambo yenyewe ndiyo hivyo. Timu ya marekani ambao ndio mabingwa wa dunia kipindi kilichopita imetetea hadhi yake hiyo na kuubeba ubingwa huo tena kwa kuwafunga uholanzi mabao 2-0. Timu ya uholanzi ilijitahidi kucheza kwa nguvu sana ila USA iliwabana mbavu kwa nguvu sana hadi wakashindwa kupumua. Watakuwa wanamshukuru sana goli kipa wao ambaye ndiye amepewa golden glove kwa kuzuia mashambulizi mengi sana yaliyoelekewa langoni mwake.



All in all, uhondo wa 2019 FIFA Women's World cup ndiyo umekwisha sasa. Kwa bahatii mbaya Copa America nayo inakwisha leo mchana na vile vile Gold Cup (Copa Oro) nayo inakwisha leo usiku.

1148917
 
Hizo video private nitaedit link zake pole pole. Ingawa zile za FIFA pia hazionekani, wewe gonga tu kuziangalia moja kwa moja Youtube. Wanataka Views
 
Back
Top Bottom