Michezo ya quarter finals za leo imekwisha huku Uholanzi ikiilamba Italia 2-0, na Uswidi nayo ikiilamba Ujerumani 2-1. kama hukuona mashindano haya basi ulikosa uhondo sana kwani timu zote zilicheza vizuri. Burudani zaidi ilikuwa ni ile sheria mpya ya FIFA ya 3 minute cooling break katika dakika ya 30 kwa sababu kulikuwa na joto kali sana uwanjani, kwa hiyo mchezo ukawa unasimamishwa kwa dakika tatu kusudi wacheazaji wanywe na kujimwagia maji ya baridi kupooza miili yao.
Mchezo baina ya Uholanzi na Italy ulianza kuonekana mwanzo kuwa Italy iliiemelewa sana. Yule msichana mwenye jina la kingoni yaani Gama alifanya kazi ya ziaza kulinda lango la timu yake ya Italy lakini mwishoni alielemwa, ikafikia mabeki wa Italy kufanya faulo nyingi zilizosababisha kufungwa. Wao wenywe hawakuwa washambuliaji zaidi ya kujilinda tu.
Kwenye mchezo baina ya Ujerumani na Sweden, Ujerumani ilianza mchezo kwa nguvu sana na kuutawala mchezo mzima kabla kibao hakijawageukia. Kwa hiyo katika dakika 20 za kwanza kabla Swedene haijasawazisha bao hilo kifundi sana. Hadi kipindi cha kwanza kinaisha Mchezo ulikuwa droo kwa bao 1-1. Baada ya kipindi cha pili kuanza Swedene ikajipatia bao la pili na kuanza kuutalwa mchezo. Ujerumani ilijitahdi sana kupoata bao la kusawazisha na walifanya kosa kosa nyingi tu, lakini ndiyo hivyo, Sweden ikawafanyia roho mbaya sana hadi kipenga cha mwisho mabao yakabaki 2-1.
Michezo ya nusu fainali itafanyika Jumanne na Jumatano wiki ijayo kama ifuatavyo
View attachment 1142410