2019 ilivyoondoka na watu maarufu.

2019 ilivyoondoka na watu maarufu.

dimaa

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2016
Posts
4,174
Reaction score
5,658
Tuko mwishonimwishoni mwa mwaka 2019. Ambapo tumepitia changamoto mbalimbali za kimaisha, wengine hali ikiwa ni Tete na wengine hali ikiwa si mbaya kiuchumi.

Pamoja na serikali kujitahidi kuweka miundombinu ya nchi vizuri, mwaka 2019 tutaukumbuka kwa matukio tofautitofauti, yakiwemo yakuondokewa na watu mbalimbali, wakiwemo wanasiasa , viongozi wa dini , wanamichezo, watoto na nk.

Ila kifo hakina makosa, tuwakumbuke wafuatao :

1. Familia ya Anna zambi.
Hili tukio liligusa hisia za watu wengi mno, ila Mimi nilihu unika mno, sikuwa na jinsi. Ni tukio lililotokea wilayani handeni Kama sijakosea, liliondoka na familia ya watu 5, akiwemo baba, mama na watoto 3.
Wakielekea kwenye mahafali ya mtoto wao was kidato cha nne wilayani moshi katika shule ya mother theresia of Calcutta, mungu hakupenda wafike kwenye mahafali ya mwanao gari ikasombwa na mafriko.

2. Ruge mutahaba.
Huyu alikuwa ni mwasisi na mmiliki wa clouds media groups (CMG). Alifariki mwezi
February nchini Africa kusini alikokuwa akipatiwa matibabu na kuzikwa kijijini kwao bukoba.

3. Reginald mengi.
Alikuwa ni mwenyekiti na mmilili wa IPP media, alifariki mwezi Mei 2019 mjini Dubai na kuzikwa nyumbani kwake moshi.

4. Ephraim kibonde
Alikuwa mtangazaji wa clouds Media groups, alifariki siku chache baada ya Kumzika ruge mutahaba jijini mwanza na kuzikwa jijini Dar es salaam.

5. Dr Omary nundu

6. Mzee akilimali

Nk.

NB: Ongezea na wengine unaowakumbuka.








Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom