Magari ya umeme bado naona itakuwa changamoto kubwa sana Tanzania hasa kwenye upande wa miundombinu, ufundi na spares.
Mpaka sasa spare za baadhi ya magari hata ya 2010 bado ni shida sana, mafundi wenye uwezo wa kutengeneza other than Toyota cars ni tuseme kama hakuna.
Miundombinu ni tatizo kubwa sana, barabara zetu ni all weather roads kuanzia posta mpaka nanjilinji. Hybrid or EV cars ni sensitive sana, kitu kidogo sana unaliacha porini.
Mvua ikinyesha, ukapitisha gari kwenye haya madimbwi yetu, gari inapiga shoti. Umezubaa ukapiga shimo, gari inakata umeme forever na ukichangia hakuna fundi, basi utapaki gari gereji.
Binafsi, napenda sana gari za umeme. Kungekuwa na reliability ya maintainance, mafundi na spares, ningepambana ndani ya miaka hii miwili ninunue full electric au hybrid kama Tesla.
Sasa toka barabara kuu mpaka kwangu tu, ukiwa na gari lele mama utalipaki ndani ya week sio kwa mashimo haya.
Ngoja nibaki na haya ya mafuta kwanza, labda nikihama nchi naweza tumia umeme au barabara zetu zikiwa za kisasa.
Sent using
Jamii Forums mobile app