Uchaguzi 2020 2020 na Uchaguzi Mkuu

Uchaguzi 2020 2020 na Uchaguzi Mkuu

solars

Member
Joined
Sep 1, 2020
Posts
91
Reaction score
161
Yamebaki masaa machache kabla hatujaenda kujipanga katika foleni kuelekea katika masunduku ya kupigia kura. Hili kila mtu mwenye akili timamu analipatia uzito wa kipekee kwani ndio muamuzi wa kumuweka madarakani kiongozi mkuu wa nchi, na kwa mujibu wa katiba ya nchi yetu, ni kiongozi atakayehudumu kwa takribani miaka mitano ijayo. Hicho sio kipindi kifupi, ni kipindi kirefu sana.

Kwa kuzingatia hilo, nadhani kila mmoja wetu anaweza kuona ni namna gani atajutia kwa kitendo kitakachopelekea kushuhudia mambo yanaenda kinyume au tofauti na alivyotegemea wakati anapiga kura. Hapa ndipo unakuja ule msemo kuwa majuto ni mjukuu, kama mababu zetu walivyotuasa. Sasa kwa hapa, mtoto ni nani na mjukuu ni nani?

Mtoto ni kura yako utakayopiga kesho; ndio mustakari utakaoamua ni na nani awe madarakani. Kufanya maamuzi yasiyo sahihi katika kupiga kura ndio yatazaa usiyoyategemea na kukuacha umeduwaa; na huyu ndio majuto mwenyewe. Hivyo basi, tutafakari kwa hekima kabla ya kupiga kura zetu, kwani ukifanya makosa huwezi kufanya masahihisho, kwa hiyo kama ni mzigo umebeba mgongoni, basi huutui mpaka miaka mitano ipite.

Tumewasikia wakinadi sera zao kila mahali walipokwenda kwa ajili ya kuomba kura. Kila mmoja wao alieleza vipaumbele vyake pindi atakapochaguliwa kuwa kiongozi. Kwa mtu makini, mpaka kufikia sasa hivi ameshampata mtu sahihi,ambaye hapo kesho atampa kura yake.

Ni jambo lisilotia shaka kuwa katika hao waliopitishwa na vyama vyao kugombea kinyang'anyiro hicho, yupo mmoja ambaye sera zake zimelenga kuwajali zaidi wananchi na mustakabali mzima wa taifa letu, huyu si mwingine bali ni Dr. John Pombe Joseph Magufuli.

Sisemi haya kwa sababu ya itikadi au ushabiki, la hasha. Nasema haya kutokana na ukweli kuwa kila alipopita alisema kile ambacho kiko ndani ya uwezo wake kiutekelezaji. Ameongelea mambo kadha wa kadha, kama vile afya, elimu, maji, barabara, nishati, na miundombinu mingine huku akielekeza huduma hizo kuwa na masilahi kwa matabaka yote ya watu hapa nchini; mtu wa kipato cha chini, cha kati, na cha juu, wote kwa namna moja au nyingine watanufaika kwa sera hizi zinazoonekana kutekelezeka.

Na hili halina shaka kwa kuwa tayari tumeona kwa kipindi cha miaka mitano anayomaliza. Hii inatupatia dira nzuri ya kuamini na kuona kuwa huyu kumbe tukimpa tena, atatusogeza mbali zaidi. Hapa gari limeshashika spidi tunachotakiwa kulichochea mafuta ili liende spidi kubwa zaidi (it is in dynamic state), kuliko kuanza kuliwasha gari ambalo limesimama tu (in static), nguvu ya kulianzisha itakuwa kubwa zaidi.

Mara nyingi tunaamini kwa kile tunachokiona, mheshimiwa huyu tumeyaona aliyofanya kwa kipindi alichokaa madarakani, sasa kwa nini tuwe ba shaka naye ilihali tunashuhudia mambo makubwa aliyoyafanya? Tusije kujilaumu baadae kwa kuchagua kwa kubahatisha na hivyo kuubeba huo mgogoro kwa kipindi cha miaka mitano.

Hivyo, tuone ni bahati kuwa na mgombea ambaye historia yake tunaijua vyema, na hivyo kutokuwa na mashaka ya kumchagua mtu sahihi. Mwanazuoni mmoja aliwahi kusema, "one bird in the hand worths two birds in the bush", tafsiri yake ni kuwa ndege mmoja uliyemshika mkononi ana thamani ya ndege wawili walioko porini. Maana yake hapa ni kuwa tushikilie kwanza kile tulicho nacho, kuliko kukipoteza, tukitegemea tutatafuta kingine.

Tuna ndege wetu tayari mkononi, tumtunze huyu, tusiwe na tamaa ya wale wawili wa porini. Kwanza hatujuwi kama tunaweza kuwakamata na isitoshe tutakapoenda huko porini kuwatafuta tutakutana na changamoto nyingi sana. Huko porini tunaweza kuchomwa na miti/miiba, kukumbana na wanyama wakali kama nyoka na wengineo, na zaidi ya hapo, hao ndege tunaowakimbiza hata tukiwapata wanaweza wakawa na matatizo yao, maana na wenyewe pia ni viumbe. Wanaweza wakawa na magonjwa kama vile typhoid, mafua ya ndege, na magonjwa mengine wahusianayo nayo.

Hivyo ni bora tukaridhika na huyu mmoja tuliyekuwa naye kuliko kusumbuka kuwafuata wale wawili wa porini huku tukiwa hatuna uhakika wa kuwapata lakini pia na afya zao. Kiongozi mmoja mwandamizi mstaafu kutoka Kanda ya Kaskazini, aliwahi kuwauliza wananchi wa moja ya mikoa ya huko kuwa, hivi inaingia akilini, nyumbani wameandaa wali na nyama, halafu eti hawa tulioandaliwa wali ma nyama tunauacha wali halafu tunakwenda porini kutafuta matunda pori. Hiyo inaingia akilini kweli? Labda mwenda wazimu ndio anaweza akafanya hivyo.

Hata mimi nakumbuka kipindi tulipokuwa watoto, kilikuwa kipindi cha mvua, watoto wa jirani yetu walienda porini kutafuta uyoga, walipata na wakarudi nyumbani wakapika na kula. Wakati huo mama na baba yao walikuwa shambani. Baada tu ya kumaliza kula, wakaanza kuumwa matumbo, wakahara na kutapika, muda mfupi baadae hali zao zilikuwa mbaya sana. Majirani wakawabeba na kuwapeleka hospitali, na wazazi wao kupelekewa taarifa huko shambani. Nilikuja kugundua kuwa kumbe sio kila uyoga huliwa, uyoga mwingine una sumu!

Ndugu zangu, kesho twende tukapige kura, asibaki hata mmoja. Tukampe Dr. John Pombe Joseph Magufuli kura za ndio. Lakini pia tumpe na wabunge na madiwani ili kukamilisha mafiga matatu, kwani figa moja au mawili hayainjiki chungu. Tusisahau miradi aliyoianzisha, aje akamilishe na kuanzisha na kuendeleza mingine. Huyu ni mtu wa watu, haangalii matabaka, rangi, kabila wala dini.

HUYU NI MWENZETU


download.jpg

 
Mimi nitampigia kura Tundu Antipus Lissu....
....Meko huyo wa kwenye picha atapigiwa kura na watu kama wewe na wasanii! Bora kumwaga sukari ziwa victoria kuliko kumpa kura yangu huyo dikteta!
 
Makala ndefu kumbe ya kuhitimisha kuomba kura,wananchi wana hamu na mabadiliko,kuna anayewaongoza watanzania katika msbadiliko ambaye ni Tundu Lissu, apewe kura.
 
shime watanzania, kulikuwa na sababu gani ya kukubali siasa za vyama vingi? Lini chama tawala nacho kitakuwa chama cha upinzani? Fursa ndiyo hii ya mabadiliko ya kisiasa, Watanzania tuandike historia iliyotukuka kwenye uchaguzi huu.
 
Vipi kuhusu mitandao ya kjamii kafungua nani?

Ni uyo anayetaka kura zetu au Lisu

Kama ni yeye bhas hapati kura yangu

Shetani Hana rafiki ndugu
 
Tundu Lissu tuepushe,haya mambo ya udikteta tumekuwa tukiyasikia Korea kaskazini leo yameanza Tz,shame on wakoloni weusi.
 
Kutuzimia "INTERNET" wakati tunalipia kwa hela zetu (Hela zenyewe za kuunga unga, bando mmetupandishia) sasa wamevuka mipaka, na ndio wamefanya tuwachukie CCM zaidi. Kwa hili hata makada wa CCM watampigia kura Lissu.

(Rais, Jeshi, TRA, Polisi, NEC, ZEC, BUNGE, TBC, BANK, TISS, Ma DC, Ma RC, Mawaziri, Makatibu, Viongozi Wa Vijiji/Vitongoji/Mitaa) wameungana ili "KUMKANDAMIZA" raia wa hali ya chini na kummaliza kabisa kimaisha.

Kulikua na haja gani ya CCM kufanya kampeni nchi nzima na magari LAND CRUISER VX zaidi ya 60 pamoja na chopper. Au kulikua na haja gani ya kuwa na uchaguzi. Kama waikua wamejipanga kutumia nguvu zote hizi? Si wangejitangaza tu bila uchaguzi.

Anaeunga "JUHUDI" za huyu kiongozi asiejielewa basi sio mzima kiakili.
 
Jiwe ni muoga Sana, jiwe limekuwa kokoto, wananchi wakikaza lzm alie
 
Dikteta uchwara anayezima mitandao kuturudisha kwenye communist China hapati kura yangu.
 
Mleta Mada bila Shaka Una ukaribu na Chama kinachotawala Dola, ambacho kinaendesha serikali, ndiyo maana umekuja kukiombea kura,

Sasa Kuna Uvumi na kuwa, Taarifa zimeshaenea duniani mitandao ya Imezimwa kwa sababu ya uchaguzi wa kesho,

Sasa mitandao ndiyo biashara na starehe za watu hasa vijana, Kitendo Cha kuizima Si hata ambao hawakupania kupiga kura wanapata ghadhabu??? Na kwenda kupiga kwa Hasira!??

Naomba unisaidie huko kuuliza kwa wahusika au hata Pengine TCRA Kama Ni uwongo Wakanushe, hili huenda wanasingiziwa, Je nikweli hili tatizo la mitandao linawahusu au Ni Mvua zimeharibu miundombinu?? Naomba uniulizie Tujue.
 
Mabadiliko ni lazima na ushindi ni kwa Tundu Lissu, tumechoka mateso ya ccm miaka Yote, na hii nchi si mali ya ccm ni ya wa Tanzania wote na kila mmoja ana haki ya kumchagulia, ccm tuheshimu maamuzi ya wengi ili Maisha yaendelee.
 
Back
Top Bottom