2021 AFCON Special Thread

Nigeria? Timu zilitabiliwa ni Senegal na Algeria na kidooogo Cameroon na Egypt. Ila mm niliwapa sana nafasi Ivory Coast na Burkina Faso
Achana na utabiri angalia mpira uliokua unachezwa..

Hao senegal wanabahati tu wanacheza vibaya kishenzi hakuna timu hapo...timu inaonekana kali kwenye makaratasi tu.
 
Bukinabe waqt wanasubiri nyumbani patulie baada ya wajeda kupindua nchi inabidi muwavumilie tu bado wapo,Japo najua mtawachukia wamechana misala yenu kwani wengi wenu mliwapa baada ya kuwatoa Nigeria ila muwe wastahmilivu tu kwao bado sio kuzuri.
 
World cup ya wapi ndugu? Ivory coast kundi lake liliongozwa na Cameroon kwa hiyo hatua ya mtoano hawapo, hao ni watazamaji tu kwa world cup 2022 Qatar.
 
World cup ya wapi ndugu? Ivory coast kundi lake liliongozwa na Cameroon kwa hiyo hatua ya mtoano hawapo, hao ni watazamaji tu kwa world cup 2022 Qatar.
Asee wajinga sana. Wana soka nililolipenda kama Ulaya vile.

Ukiona vizuri Egypt alikua anawaogopa, ilitakiwa wawe wakali first hf hata kutupia Goli ili kuwatoa kiakili Egypt.
 

Ubaguzi unawatafuna sana waafrica
 
Huyu referee wa mchezo huu Wa Tunisia na Burkina Faso ni ovyo kabia, alivunja mechi kabla ya dakika alizoengeza kumalizika. Na pia cha ajabu zaidi mechi ilisimama mara mbili kwa ajili VAR, dakika hazipungui saba zilipotea, na pia mechi ilisamama mara kadhaa kwa injuries. yote haya na bado akaishi kuengeza dakika nne tu nahizo pia hakuzimaliza.

Africa kuna mambo ya ovyo sana na bado yanachukuliwa powa tu.
 
Sijawahi kuona mechi ya mwarabu na giza refa akawa mwarabu, lazima awe giza tu hata kwenye caf cl ni hivyo hivyo

Ila kuna wakati mwingine hawa akina Vivuli huwa wanawasaliti wenzao na kuwa upande wa Waarabu
 


Hivi mwenye jukumu la kuongeza dakika ni read wa kati au kamisaa wa mchezo husika?
 
Ila kuna wakati mwingine hawa akina Vivuli huwa wanawasaliti wenzao na kuwa upande wa Waarabu
Mpira hauchezewi chumbani broo au sio karata zile kwamba utaficha kila kitu hadharani, lini giza alifanya usaliti?
 
Hakuna cha dharau, wamepigwa kihalali. Kuanzia dakika ya kwanza mchezo kwa upande wao ulikuwa mgumu. Burkinafaso siyo wanyonge, miaka siyo mingi walifika fainali ila wakapoteza kwa Egypt.
Ile Fainali walipoteza kwa Nigeria 2013 kama sikosei
 
Mi naona kombe linabaki Cameroon kuna mikakati naiona imesukwa.
Kwa mikakati naamini. Jana nimeangalia ile match kwa umakini sana. Gambia mpaka dk 40 wachezaji watatu walikuwa wamekula Yellow kosa mojawapo ni kipa kupoteza muda. Just imagine goalie anapoteza muda dk ya 30 na kadi nyingine very soft.
 
Kwanini EGYPT Vs MOROCCO inachezwa saa 12 jioni na sio saa 1 kama match nyingine zilivyochezwa?
 
Sema yote 9, Burkina Faso nidhamu yao ipo chini sana.....jana walipata kazi nyingi zinazoepukika....

Ngoja tuone next game labda ni tension ya mechi ya jana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…