2021 AFCON Special Thread

Aboubakary n mfungaji bora .... hawez kuwa mchezaj bora ..coz mchezaji bora wanaangalia vitu vingi zaid ya kufunga tuu ...Ukimuangalia Mane kwanza amekua akianzisha mashambulizi ....ametoa assist kadhaa na pia ameweza kuiongoza team yake mpaka kufika fainal ...
 
Anaitwa bouna sarr yupo bayern Munich
 
Wakuu nina maswali


Kwanini Algeria kwenye mashindano haya alivaa shati katika Ina badge ya fifa timu nyengine hazikufanya hivyo ?



Je kuchukua afcon unaweza fuzu mojakwamoja world cup ?
 
Asanten sana wanangu wa Senegal Hakika mmeifanya siku ya Leo kuwa mzuri sana, nimpongeze mtoa mada kwakwel umejitajidi sana kuweka update za kinachoendelea Ubarikiwe sana hata sisi tusioenda vibanda umiza tumeumizana humu humu hahaha, niwape pole mlioumia ndio mpira hata sisi tuliumia hivyo hivyo timu zetu pendwa zilipotolewa usifikir tulipenda kuhama hama hapana, Ila yote Kwa yote tumepata burudani, Nipende kukushukuru wewe uliyetumia bando kuuchangamsha Uzi huuu wengine milikuwa mkipita Kimya Kimya mbarikiwe sana. Basi Kwa niaba ya fundi mitambo na clue nzima ya matangazo iliyoongozwa na kiongozi wetu muanzisha mada, tufunge ukurasa huu wa kwanza na tufungue wa pili kuzichambua timu zetu kama zitatoboa world cup
 
Wakuu nina maswali


Kwanini Algeria kwenye mashindano haya alivaa shati katika Ina badge ya fifa timu nyengine hazikufanya hivyo ?



Je kuchukua afcon unaweza fuzu mojakwamoja world cup ?

Amechukuwa ubingwa wa Fifa arab cup, may be ndiyo nembo yenyewe iyo, lakinii cna uhskika
 

Algeria vipi mkuu?
 
ni nani huyu mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Star wa Cameroon kwenye World Cup ya 1990 pale Italy.

Alikuwa kashastaafu kabla ya Rais Paul Biya kumuomba aiongezee nguvu timu ya taifa ya Cameroon iliyokuwa inaenda kwenye michuano hiyo.

Basi kama ilivyo ada, kauli ya Rais ni sheria, Roger Milla akarudi timu ya taifa na mechi ya ufunguzi, Argentina bingwa mtetezi dhidi ya Cameroon, Roger Milla akafunga goli huku Cameroon ikiishangaza Dunia kwa ushindi wa 1-0.

Shangilia yake kuelekea kwenye kibendera ikampatia umaarufu mkubwa na ni icon ya mojawapo ya World Cup ya 1990

Kutokana na ushujaa huo, mwanamuziki nguli kutoka DRC, Pepe Kalle katika albamu yake ya Gerant akamtungia Roger Milla kibao ambacho mpaka leo kimebaki na umaarufu wake!!

Nafikiri umemsoma sasa Roger Milla kwa ufupi
 
Mwez ujao hawa Mashujaa wanakutana tena kutafuta Qualification ya wc
 
Sijui kwann hachezi ulaya
Waarabu ndicho nachowapendea hawana time na mzungu....angalia hata akina aboutrika n.k ni mafundi haswaa lakini hawakuwa na tamaa ya kwenda nje, nationality yao ndio kitu cha kwanza, na wala hawaringi
 
Mwez ujao hawa Mashujaa wanakutana tena kutafuta Qualification ya wcView attachment 2111237

Kwanini walioongoza kundi kwa maana nafasi ya kwanza na yapili wasipite moja kwa moja w/c


Just think timu zinazokutana ni bora, Algeria, Morocco, Senegal, Egypt, Nigeria, Cameroon n.k.....moja ikishinda inapita na nyingine inabaki, kwa maana timu chache sana zitakazoshiriki....ebu niambie timu kama Algeria na morocco wakimiss, timu ipi tutegemee itatuwakilisha na kufanya vyema!! Sijajuwa FIFA wana malengo gani kwa timu za Afrika
 
Waarabu ndicho nachowapendea hawana time na mzungu....angalia hata akina aboutrika n.k ni mafundi haswaa lakini hawakuwa na tamaa ya kwenda nje, nationality yao ndio kitu cha kwanza, na wala hawaringi
Alafu Ulaya wanatoa matimu mengi mengine hata hayaeleweki.

Afrika tupewr timu kumi, nchi zipo 54 na timu zilizo competitive ni zaidi ya 15,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…