Baada ya mashindano ya AFCON22 timu za Afrika zinajiandaa kwa WC Qatar.
Katika timu 10 za Afrika zilizofuzu mchujo wa mwisho wa kupata timu 5, ni nchi moja tu DRC ambayo haikushirikia AFCON Cameroon iliyoisha leo.
Kwa maana nyingine tumeziona timu 9 (ukiondoa DRC) zikionyesha nguvu zao ikiwa zitafuzu WC.
Kwa mtazamo binafsi katika timu zote zilizoshiriki AFCON, Ivory Coast ndiyo iliyoonyesha soka kubwa ambalo kama ingefuzu WC nina uhakika ingesumbua, bahati mbaya haimo katika 10
Tuziangalie timu 10 zitakazotoa 5 kuelekea Uarubuni kwa WC
DRC- Ukiacha mechi za kufuzu ambazo imetumia wachezaji wa kulipwa hatuwezi kupima uwezo wake, haikushiriki AFCON. Tunabaki kuamini tu kama itafuzu ina wachezaji wa kulipwa
Nigeria- Ni dhaifu sana ukilinganisha na zilizowahi kushiriki WC. Haina mpangilio wa soka, wachezaji wanatumia vipaji na uzoefu wao bila team work
Tunisia- Mchezo wao ni ule ule wa kila mara, haina timu ya kutisha lakini ina timu ya matumaini
Ghana- Ina timu mbovu sana kama itafuzu WC inahitaji kubadili mchezo na hata wachezaji.
Kama itafuzu WC haivuki hatua ya kwanza. Ghana imepoteza ile ''total football'
Cameroon- Ina timu nzuri sana hasa viungo na beki, haina forward ikimtegemea Aboubakary.
Abou akiwa chini ya ulinzi Camroon imezima. Ikifuzu WC inaweza kuingia 16 lakini si zaidi ya hapo
Egypt- Ina timu nzuri hasa ulinzi. Wanacheza 5-4-1 wakimtegemea Salah.
Kama Cameroon, ukimweka Slaa chini ya Ulinzi Egypt haina kazi.
Mali- Wanatumia nguvu sana kuliko maarifa, hawana mashambulizi ya kupanga.
Si timu ya kutumainia WC kama itafuzu.
Morroco- Wana timu nzuri pia lakini ushambuliaji wao si mzuri.
Wana viungo wazuri na hutegemea sana ''winger' . Kwa mipira ya kudondosha, ni ngumu sana kuzifunga timu za Europe. Ikifuzu WC inaweza kuingia 16 si zaidi ya hapo
Senegal- Ina timu nzuri lakini beki yake inakatika sana. Inahitaji kuimarisha eneo la kiungo na kuacha kumtegemea mshambuliaji mmoja tu. Ikifuzu inaweza kuingia 16 si zaidi ya hapo