2021 AFCON Special Thread

Huyu refaree leo ndio utopolo kabisa. Najisikia aibu kuwa mwafrika. Maana hakuna kitu tunachoweza. Kwanza alimaliza mpira dk ya 85. Kukazuka tafrani, mpira ukaendelea. Akatoa streight red card kwa mchezaji wa mali hata alipotakiwa kwenda kujiridhiaha kupitia VAR, akaangalia na akatoa maamuzi ya red card ni sawa.
Akaongeza kituko kingine cha mwaka. Akamaliza mpira dk 89. Japo kulikuwa na cooling time muda mpira uliposimama kuruhusu wachezaji wanywe maji.

Huyu lazima aondoke kama ndugai. CAF hawewezi kumvumilia.
Ni aibu kubwa kwa waandaaji wa haya mashindano.
 
Ameugua malaria,utakuwa utetezi wake
 
Wachambuzi uchwara wa soka wa UTV wote wanasema lie chalenge ilistahili streght redcard. Wallah ninaudhika sana.
 
Sheria zinasemaje mpira uki malizwa kabla ya dakika 90? Huyu mwamuzi leo katuwashiklisha uafrika wetu nmeona aibu kinoma imagine hio game ina onywesha duniani kote
 
Refa anapomaliza mpira dk ya 89 ana maana gani? Hata dk za 90 kuna nyongeza pia ,kuna cooling time imetumika Kama dk moja ,hizi ni hujuma ,kuna timu wanaweza kurudisha goli dk za nyongeza na wakaongeza ,najua CAF watamwadhibu ila kwa Tunisia ni hujuma kubwa maana game haitarudiwa.
 
Lakini pia huyu Refa Mwaka 2018 Alisimamishwa na CAF kwa Tuhuma za Kupanga matokeo. Lakini Cha Ajabu Alichezesha katika world cup 2018.
 
Kilichotea katika game ya Tunisia vs Mali mbona kama sijaelewa. Game imeisha dk ya 89 na sec 50.
Kwanza mara ya kwanza alimaliza dakika ya 85.Watu wakamzonga tena akarudia kosa lile.
 
Duh ila refa amekuwa mtemi hatari
 
Nafikiri Tunisia Wanaweza ku complain mchezo ukarudis katika mazingira haya.

1. Wamefungwa goli 1, goli ambalo walikuwa na chance kubwa ya kurudisha, ukizingatia mali walikuwa pungufu, tumeshaona Big mechi zikiamuliwa kwa Dakika za Nyongeza.

2. Refa mwanzo alimaliza mpira Dk ya 84 means kuna kitu kilikuwa kinaendelea kichwani mwake.

3. Historia ya Refa wa leo sio nzuri kwa mpira wa Afrika

Wanaweza shinikiza mechi kurudiwa kwa Maandishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…