Star wa Cameroon kwenye World Cup ya 1990 pale Italy.
Alikuwa kashastaafu kabla ya Rais Paul Biya kumuomba aiongezee nguvu timu ya taifa ya Cameroon iliyokuwa inaenda kwenye michuano hiyo.
Basi kama ilivyo ada, kauli ya Rais ni sheria, Roger Milla akarudi timu ya taifa na mechi ya ufunguzi, Argentina bingwa mtetezi dhidi ya Cameroon, Roger Milla akafunga goli huku Cameroon ikiishangaza Dunia kwa ushindi wa 1-0.
Shangilia yake kuelekea kwenye kibendera ikampatia umaarufu mkubwa na ni icon ya mojawapo ya World Cup ya 1990
Kutokana na ushujaa huo, mwanamuziki nguli kutoka DRC, Pepe Kalle katika albamu yake ya Gerant akamtungia Roger Milla kibao ambacho mpaka leo kimebaki na umaarufu wake!!
Nafikiri umemsoma sasa Roger Milla kwa ufupi