Habari zenu Jf.
Heri ya mwaka mpya 2022, natumaini wengi wenu ni wazima na wale wenye udhaifu wowote basi Mungu aliye juu sana awatie nguvu ,shauri ,ujasiri na uhodari katika kushinda udhaifu huo.
2022 one of my plan is to give more.........
Mwaka mpya umeanza kila mmoja yupo kwenye kuangalia mwaka huu atafanikisha lipi na kwa njia gani. Kwa upande wangu nina lengo moja kubwa la kutoa zaidi au kuwa mkarimu zaidi.
Nitahakikisha mwaka huu nawafanyia ukarimu watu wengi zaidi ambao watahitaji msaada wangu au watanihitaji. Najua unaweza kujiuliza imekuwaje jambo hili nikaweka hapa kwenye jukwaa la uchumi na biashara, jibu ni jepesi tu kwa sababu ninataka kutoa zaidi kwenye upande huu wa uchumi, yaani watu wafanikishe mipango yao ya kiuchumi na biashara kwa msaada au ukarimu nitakao weza kuwapa.
Kwa zaidi ya miaka mitano nipo kwenye biashara ya kutoa huduma na bidhaa za maswala ya maji , hapa namaanisha uchimbaji wa visima, pampu za maji kuuza na kufunga, kufunga mifumo ya maji safi na maji taka , kuuza fittings na fixtures za mifumo ya maji.
Sasa basi najua watu wengi wanachangamoto kwenye hii nyanja ya maji , hivyo nimekusudia kutoa msaada na ukarimu kadili ninavyoweza katika kusaidi kutatua changamoto zote za huduma na bidhaa hizo ikiwa mtu amekwama sehemu.
Mfano kwa uzoefu nilioona kwa kupokea simu nyingi za watu wakitaka huduma ya kuchimbiwa visima vya maji lakini wengi wao walishindwa gharama, sasa hua sijisikii vizuri kumwona mtu anakosa huduma muhimu ya maji ambayo yapo tu bure huko chini ya ardhi kisa pesa yake haitoshi, je siwezi kufanya kitu kumsadia mtu kama huyu ? sasa hapa lazima nijitoe kwa huyu mtu, kutoa huku kunaweza kuwa ni muda wangu, ushauri, connections, n.k ili tu ile haja ya moyo wake ipate mwanga wa kuanza.....kwa kuanzia tu na jambo hili kuna mkakati utaandaliwa kuona tunasaidiana vipi...
Kuna wale wanaoshindwa kufanya underground water survey , ambayo ni hatua muhimu sana kabda ya kuchimba kisima, hapa napo panahitaji la msaada, ......
Kuna watu wapo kwenye ujenzi wa nyumba, wakifika kwenye kuweka mfumo wa maji niliwai kuwashauri huko jukwaa la ujenzi, December 2021 kuwa wajaribu kukusanya pesa na kununua material kwa bei ya jumla kwenye godown moja kwa moja kupunguza gharama, hapa nilijitoa pia sasa mwaka huu nitajitoa zaidi kwa kutafuta godown mbili tatu katika location tofauti tofauti, zenye bei nzuri za material na nitawawekea pricelist zao hapa hapa jamii forum na kwenye social media account, fanya kuifollow account ya kampuni kule twita na istagrama ili usipitwe na hayo yajayo.. @evigt_water
Mambo mengine ni upande wa huduma ya ufundi wa bomba au kufunga pump, kampuni kama kampuni tunao mafundi wazuri ila watanzania wenzangu wapo wanashindwaga kumudu installations, sasa siwezi kuona umenunua pump au plumbing fittings au plumbing fixtures kwetu halafu ushindwe ghalama ya installation aise mwaka huu hata kukukopesha ikiwezekana iwe na iwe ili haja ya moyo ya mteja wangu itimie..
Mambo ni mengi naamini na changamoto zingine zitajitokeza kadiri ya namba za siku zitakavyosoma ndani ya 2022, ila lengo langu ni kutoa zaidi.
ANGALIZO: Wapo watu wanaoweza kumudu gharama za project zao ila watataka kuchukua advantage za andiko hili, ni kwamba utakuwa unawakosea watanzania wenye shida ya kweli , utatenda dhambi bure . Kama unamudu gharama za project yako katika hali ya kawaida, usijiingize kwenye gharama ya misaada , moja ya gharama ya misaada ni kupoteza muda. OKOA MUDA WAKO.
Pia kwa kuwasaidia vijana wenzangu wanaoweza kujituma nawakalibisha kufanya kazi nasi kwa upande wa masoka, water engineering, plumbing, n.k . tutalipana kwa project basis na commission basis.
Kazi njema. Karibuni nyote kwa ushauri na maoni.
usisahau kutafuta account zetu za kijamii..
Subscribe
Jamiiforum@evigt,
twitter @evigt_water
Instagram @evigt_water
Whatsapp +255699494650
Whatsapp +255759600809
Lindi street/kko