Cybergates
JF-Expert Member
- Dec 2, 2016
- 697
- 1,474
Programming ni kama investment, unajifunza leo lakn mafanikio ni yabaadae.Hapana Hapana Kweli kila mtu na maono yake Aisee.Lakini Anime can do nothing over programming.Yani Anime labda uwekeze kwenye Social platform kama TikTok na youtube..Ila programmng ni multi-talent unaweza fanya mambo mengi
Kweli mkuu hamna kazi rahisi, hata kwenye Programming kuna shida tu hamana unafuuHata upande wa animation nao unahitaji muda na moyo wa kujifunza hata huko mambo hayajakaa kilelemama. Blender, Adobe After Effect, Premiere Pro, Cinema 4D na softwares nyingine nyingi zinazohusisha animation zinataka muda na moyo wa kujifunza
Kama programmng njo huku kwenye M2MKila mtu na lake mimi nianze kujifunza mapicha picha labda ninyongwe sina interest hivyo usiwasemee wengine
Coding baby
Programming ni nzuri ila inahitaji muda, moyo na kujitoa kwa hali ya juu. Inabidi ukubali kubadilika pale ambapo teknolojia inakimbilia. Mwaka 2019 nilianza kujifunza website design, muda huo huo nilikuwa najifunza Adobe Ps, sikuchukua hata round nilibwaga vyote viwili.
Kwasasa nimebaki na ufahamu wa juu juu tu, ila nimejifunza fani yoyote inahitaji muda, moyo, kujitoa, mazoezi na kufuata teknolojia inakokimbilia.
Itakuchukua muda mkuu.Samahani mkuu kama hutojali naomba unifahamishe inaweza kunichukua muda gani ku master industry ya programming? Sio inilipe kwa maana inisaidie zaidi professionally kuendana na field niliyonayo im water resources engineer by profession.
Itakuchukua muda mkuu.
Naweza kusema hivyo kwa sababu niko kwenye safari hiyo na inahitaji ujitoe kweli hasa kama unajifunza mwenyewe.
Ila ukijitoa utaanza kuona unaensa mapema hata within two months utaweza tengeneza vitu vidogo vidogo. Baadae utajifunza kuwa unaweza kutumia frameworks pia kufanya vitu vingine zaidi
Huwezi tenganisha Animation na programming kama unajitambua.Maoni!!
Wengi huwa tuna malengo ya kujifunza mambo mapya huu mwanzo wa mwaka,
Je ni kipi cha kujifunza kati ya animation na programming?
Kama mimi ningeambiwa nichague ningeenda na animation
Animation ina fursa sana na soko kubwa kulinganisha na programming, kuanzia 2D hafi 3D soko. Ukianza leo mpaka May nahuakika utakua umeanza kula matunda ya kazi yako
Software nyingi za animation zimekua integration na AI ivyo inafanya kazi kuwa rahisi
2024 GO WITH ANIM
Dhu!Huwezi tenganisha Animation na programming kama unajitambua.
Tena hususani Animation, hiyo field unayozungumzia na ulichokichagua ndio havitengani na programming, watu wanakaa wanaona engine zinazingua wanatengeneza za kwao kama Disney angalia walichokifanya kwenye Moana.
Ilibidi wakae watengeneze engine itakayoweza kurender na kuanimate maji kiurahisi, kilichotumika ni programming.
Angalia software kama Maya Autodesk, Cinema 4D n.k zInarun na Python kwenye animation n.k unaweza program plugin zako mwenyewe kwaajili ya kuanimate, kufanya baking n.k pia programming language nyingi tu hutumika kwenye animation.
Manual animation inafanyika lakini Ina ukomo ambapo suala la programming linakuja.
Kama unapenda mambo ya 3D/2.5D/2D
Chagua kati ya hivi uanze na kipi
Modelling/Sculpting
hapa industry standard software unazohitaji kujifunza ni
(Zbrush for sculpting, Maya for Modelling hard surface, AutoCAD for Environment modelling)
Ukijifunza hizo software vizuri zitakusaidia na blender kumbuka makampuni mengi hayaihitaji japo ni powerful na uzuri wa hizi software ukimaster Moja kuhama nyingine ni rahisi Mfano C4D to Maya
Retopology
Hiki ni kipengele kipana sana nacho mana ukizingua hapa utaleta ugumu kwenye vipengele vinavyofuata, na ni muhimu kwasabu hapa ndipo character anakuja kuwa optimized, zipo software zinafanya automatic japo ni lazma upitie manually kuhakikisha character ana polygons ambazo zimekata sawa for next step.
UV Mapping & Baking
Hapa kama ulifanya retopology vizuri basi kazi itakuwa sio ngumu sana na zipo pia software za baking ja uv mapping na unwrapping unaweza fanya kwenye software ulizofanyia modelling.
Rigging
Hapa Sasa napo kama ulifanya Retopology vizuri kurigg haitasumbua sana japo ni kipengele nacho na Kuna muda programming inaingia, for advanced level.
Animating
Sikuizi animation wanatuma 3 reflecting kwenye green screening japo ni gharama lakini manual animation, unahitaji pia kuelewa tabia ya unacho kuanimate, kama ni binadamu basi ujue Physiology and anatomy ya mwili unamive vip, mfano ndani ya dakika macho anablink mara ngapi n.k, na programming pia inaingia hapa.
Lighting
Hapa napo panahitaji concept za uhalisia in real world ilibkuleta matokeo mazuri, mfano concept kama Jua likiwa mashariki kivuli kinakuwa wapi na ni saa ngap n.k,
Rendering
Hapa suala la PC linahusika kuanzia uwezo wa GPU mpaka CPU, na wenzetu wanazo rendering farm, kwaajili tu ya kufanya rendering.
Hapo Kila kipengele kimoja kina upana wake kwahiyo chagua wewe uanze na Nini, mana kama unataka uwe una animate itabidi utengeneze character au ununue kwaajili ya license.
Hii field nayo usijeona ni rahisi kuliko programming utakuwa umejichanganya, unaweza Kesha siku nzima unafa keying ya sekunde 20 tu,
Usiingie kwenye hii field kwasabu ya mihemko mana nayo inahitaji kujitolea ilibusikate tamaa.
AI imesaidia siku izi kwa kiasi Fulani lakini mambo Bado ni magumu.
Usikate tamaa
[/FONT][/B]snipa
Maoni!!
Wengi huwa tuna malengo ya kujifunza mambo mapya huu mwanzo wa mwaka,
Je ni kipi cha kujifunza kati ya animation na programming?
Kama mimi ningeambiwa nichague ningeenda na animation
Animation ina fursa sana na soko kubwa kulinganisha na programming, kuanzia 2D hafi 3D soko. Ukianza leo mpaka May nahuakika utakua umeanza kula matunda ya kazi yako
Software nyingi za animation zimekua integration na AI ivyo inafanya kazi kuwa rahisi
2024 GO WITH ANIM
Mimi mwenyewe najifunza python. Passion na commitment tu mkuu.Daah inaonekana ni ngumu kwa mtu ambae anakuwa na muda kidogo wa ziada wa kujifunza au sio?? Kwa sasa ninajifunza python kwenye upande wa field yangu ya water resources engineering tutorials zinani impress kwa maana naona namna mpya ya ku design systems kwa codes shida ni kwamba sina foundation kabisa ya programming mana wengi wanashauri kuanzia chini kabisa.
Nimesema jifunze animation, haijalishi unatumia nini. Kama unatimia AI tumia kama unatumia adobe tumiayani kwa technology ilivyokua na ujio wa AI kukuki zinazoweka kutengeneza matangazo ya animation, logo, picha mpaka animation videos bado unataka ujifunze animation ?!!
hauko serious we jamaa
Na shida ya kusomea programming bongo ni hii,, labda usome nje na ikiwezekana patia ujuzi nje ila ukienda na huu mfumo wetu huku ukiingia kwenye ushindani unaweza ukajiona mweupe,,,,.... Wakenya naona wanatupiga Gap na wanyarwandaMambo yanayobadilika ni mengi na muda ni mchache...
Sisi tuliosomea Engineering kwenye upande wa electronics, tulijua mpaka transistor inavyofanya kazi, tukaanza kuona IC zinatumika sana kuliko kuungaunga circuit kwa kwa ma transistor, resistor na capacitor....
Tukawa tunawacheka waleo ile kuwa hata hawajui ndani ya IC kuna nini na inafanyaje kazi...
Ikaeenda mpaka kwenye logic gates, tukajina tunajua sana binary na hexadecimal...
Mara zikaja Microcontroller (Arduino) tayari ni complete board, unahitaji tu kuprogramme sequence, sisi tulibaki tu kwenye differential amp na op amp kwa kujifanya tunajua ku calculate output voltage.
Mara Microprocessor( Rasberry Pi) hizi hapa, ambazo zinatengeneza mfumo mzima na hata computer nzima....
Kwa hiyo naona jinsi hizi API na AI zinavyokwenda, kwa sisi huku ambao hatuhusiki na manufacturing, ambapo ndio pia coding zitakuwa ready made, utashtukia hata hauhitaji kujua C++ wala Python
Kila kitu kina kuwa tayari ni wewe tu unatakavyoweza kukifanya applicable kwenye teknology mpya itakayo kuwa ina trend muda huo.......
Safi sana, useful thread.... haya mimi nataka kijana mmoja ambaye atanisaidia kutengeneza application fulani ambayo ninahisi kama ikikaa sawa ina weza kuwa potential kwa taasisi za serikali.Maoni!!
Wengi huwa tuna malengo ya kujifunza mambo mapya huu mwanzo wa mwaka,
Je ni kipi cha kujifunza kati ya animation na programming?
Kama mimi ningeambiwa nichague ningeenda na animation
Animation ina fursa sana na soko kubwa kulinganisha na programming, kuanzia 2D hafi 3D soko. Ukianza leo mpaka May nahuakika utakua umeanza kula matunda ya kazi yako
Software nyingi za animation zimekua integration na AI ivyo inafanya kazi kuwa rahisi
2024 GO WITH ANIM
Kuna hii kozi ya bure ya Artificial Intelligence. Kwenye hii kozi wanafundisha lugha ya Python. Hii ni kozi kutoka chuo kikuucha Harvard, kozi inafundishwa kwa muda wa wiki 11. Kozi hii ni ya BURE KABISA.
Link hii hapa CS50's Introduction to Artificial Intelligence with Python | Harvard University
Harvard Free 11-week AI CourseAu hapa
kama ulivyosema ungeanza chini kwanza. Python kwa upande wangu naona ni kama umeruka hatua nyingi hapo katikati.
Nipo hapa mkuu natengeneza native android & ios appsSafi sana, useful thread.... haya mimi nataka kijana mmoja ambaye atanisaidia kutengeneza application fulani ambayo ninahisi kama ikikaa sawa ina weza kuwa potential kwa taasisi za serikali.