2024 Kilimo kimewatoa Wachina Milioni 33 Kwenye Ufukara.Tukiuliza SGR imeondoa Watu Wangapi kwenye Umaskini Majibu ni matusi.Tuna shida ya Vipaombele

2024 Kilimo kimewatoa Wachina Milioni 33 Kwenye Ufukara.Tukiuliza SGR imeondoa Watu Wangapi kwenye Umaskini Majibu ni matusi.Tuna shida ya Vipaombele

Nia njema kwenye mradi ambao hauna impacts Kwa majority poors?

80% ya Barabara ni mavumbi na huko kwenye mavumbi ndio majority wanaishi na zingine hazifikiki.

Hizo Sgr Zina msaidia nani? Si unaona wanatoa data za watu waliosafiri na Mapato ila hawatoi running cost ,unajua Kwa nini wanaoficha upande wa pili?
Uko sahihi kabisa, miradi haina direct impact kumgusa mwananchi wa chini. Lakin kuna class fulani inawanufaisha. So tunatokaje hapa?
 
Umeongea vyema shida hii ichi wajinga ni wengi, mwanasiasa akija na porojo zake yeye kiongozi wa wanyonge watu wanachekelea. Badala wahoji sasa huo unyonge atawaondoleaje?
 
Nadhani kama ulifuatilia mchakato wa kilichotokea Dodoma tarehe 19.01.2025 utagundua tunapokwama. Mabadiliko ya dhati yanaletwa na siasa safi plus watu wenye uwezo na nia thabiti. Si ufisadi, ujanja ujanja na short-cuts.
Tanzania tumejikita sana kwenye ufisadi na hadaa... Tegemea matokeo ya ufisadi na hadaa kutamlaki kila kona!
Resources nyingi zinazotumika sasa kumsimika incompetent president madarakani zitatumika kutengeneza watu wajanja wajanja wanaoongea hiki na kutekeleza kingine wasichokiamini.
Wachina wanajua wanakotaka kwenda hapa Ulimwenguni... Wanajua wachokitaka kwa viongozi wao na wanawaandaa kikamilifu wanaopaswa kuwapeleka huko!
Watanzania bado sana na bahati mbaya tumenasa kwenye mtego wa kugeuzwa wachuuzi! Kwa wengi maendeleo ni kutumia vitu vilivyotengenezwa kwa teknolojia ya wengine!
In short kilichotokea Dodoma kinadhihirisha uwezo na upeo wetu!
 
Toka tumepata uhuru adui zetu ni wale wale hatujapunguza hata mmoja ila huenda wameongezeka. Kuna wapiga deal kubwa kubwa.
Ujinga ndio tatizo kubwa yanafuata mengine ukihoji unatulizwa
 
Kupanga ni kuchagua ila hapa Tanzania Sina hakika kama.tunajua kuchagua mipango ya kipo kianze au kipi kifuate.

China imeripoti kwamba mwaka 2024 imewatoa Wachina zaidi ya Milioni 33 kutoka kwenye ufukara Kwa kutumia sekta ya Kilimo baada ya serikali Yao kuwekeza huko Kwa Nguvu zote.

Hao watu walioondolewa kwenye umaskini wengi wao walikuwa na kazi za vibarua ama mashambani au mjini kwenye viwanda nk.

Tukiacha China ,hivyo hivyo ndivyo Nchi nyingi za Asia zinafanya.

Hapa Tanzania Huwa tunakurupuka tuu na miradi ya Kisiasa ya kupigia picha na bahati mbaya mafukara nao Kwa kuwa hawajieleqi kwamba ufukara wao umehatibu Hadi akili wanashangilia mambo ya Wanasiasa wavivu wa kufikiria Kwa kufanya miradi cheap na isiyo ya msingi.

Kiongozi yeyote anaejitambua lazima atafahamu idadi ya maskini na mafukara kwenye Nchi yake na hivyo atatekeleza miradi Ile ambayo itaondoa au kupunguza ufukara na sio kama inavyofanyika hapa Tanzania.

Tanzania yetu hii Kuna juhudi zinafanya lakini ni kidogo sana na haziwezi kuondoa umaskini hasa wa kipato.Ndio maana Umeme uko Kila Kijiji ila unakuta kaya zilizounganisha hazifiki hata 20.

View: https://x.com/ChenMingjian_CN/status/1881711347450180073?t=a1jDQDpke3_H8USZQ-NRUA&s=19

My Take
Nchi iache miradi ya maonesho na kupigia picha Bali wafanye miradi ya kusaidia watu kuondokana na umaskini mfano Kilimo,uvuvi,ufugaji, biashara,Utalii na viwanda Vidogo.

Vietnam Ina Uchumi mara 5 ya Tanzania yaani $420bln vs $80bln respectively lakini wanaanza mradi wa Ujenzi wa Sgr 2027.Hawana mda wa kuzika hela kama tunavyofanya Kwa miradi ya kupigia picha.

Kama tunaendelea na utaratibu huu basi idadi ya maskini itazidi kuongezeka maana tuko top 5 ya Nchi Zenye maskini wengi Africa.

View: https://x.com/ChenMingjian_CN/status/1879152795099742531?t=gYrRQUM4cTqzwG3yPxVhSQ&s=19

View: https://x.com/ChenMingjian_CN/status/1879891363426144686?t=zwPnTaHnoJPxoJIS_pNGjg&s=19

Chama Cha Mazezeta
 
Toka tumepata uhuru adui zetu ni wale wale hatujapunguza hata mmoja ila huenda wameongezeka. Kuna wapiga deal kubwa kubwa.
Mkuu tatizo tumenasa kwenye mfumo wa umaskini unaotukuza vitu na watu waliolimbikiza vitu. Wenye limbikizo la vitu wanaonekana ni wa maana sana kwenye jamii. Wengi wanatumia njia haramu kujilimbikizia vitu ili waonekane tofauti mbele ya jamii.
Wenye madaraka wamemong'onyoa mifumo imara ya kuwaendeleza wenzetu ili wawe wafike hatua ya kujikwamua. Nchi imegeuzwa ya kichuuzi chuuzi... Wasomi wetu wanajiuliza swali zito wanasoma ili iweje! Ili wasipoteze kila kitu nao wanaamua kujiunga na watawala walioshindwa kuwakwamua!
Nchi nyingine zilizowahi kujitambua wananchi waliamka na kuwafurusha miungu watu!
Historia ya maendeleo ya watu ndivyo ilivyoniongoza!
 
Mwamba ni kama maji usipoyanywa utayaoga !
Kila siku habari zake lazima zije jamvini 🤣🙏🙏
 
Hao wachina milioni 33 wana mijengo,mandinga na account zao zimaenona?
 
Wewe usiwe unakurupuka na kuandika uozo. Unajua network ya railway zilizojengwa China? Hao millioni 30 wangesafirisha mazao yapi kivipi? Halafu uelewe kama ni infrastructure investment ni serikali ndiyo inahusika zaidi kujenga. Wakulima walihimizwa kulima na kupewa subsidies, serikali ya Tanzania lazima iwe inawahimiza wakulima wake kulima na wawape subsidies. China ardhi inakodishwa kwa wakulima, Tanzania ardhi bure karibu sehemu nyingi. Uvivu na ukosekanaji wa ubunifu kwa serikali na wakulima ndiyo unaleta umasikini.

SGR investment na uhmizwaji kwa wakulima kufanya kazi vinaenda simultaneously.
Umewahi kulima halafu wakati wa mavuno mipaka ikafungwa?

Umewahi kusafirisha hata maharage tuu kwenda nje? Mfano UAE
 
Biashara yoyote duniani ina hitaji vifuatavyo:-
1. Bank and banking
2. Insurance
3. Transportations
4. Advertisement
Zingatia sana hiyo No 3
 
Nchi nzuri sana Kwa ramani ila life ni misery,ukitaka kujua wewe angalia hata kaya zenye ving'amuzi
Wanaotakiwa kupanga vipaumbele ni akina nani, Kwa miaka yote sitini waliopewa dhamana ya ku utilize rasirimali na kodi za nchi hii ili kuwaletea wananchi maendeleo ni akina nani? Tukisemaga vijana wengi wa CCM hamjitambui mnakuwa wakali
 
Wewe usiwe unakurupuka na kuandika uozo. Unajua network ya railway zilizojengwa China? Hao millioni 30 wangesafirisha mazao yapi kivipi? Halafu uelewe kama ni infrastructure investment ni serikali ndiyo inahusika zaidi kujenga. Wakulima walihimizwa kulima na kupewa subsidies, serikali ya Tanzania lazima iwe inawahimiza wakulima wake kulima na wawape subsidies. China ardhi inakodishwa kwa wakulima, Tanzania ardhi bure karibu sehemu nyingi. Uvivu na ukosekanaji wa ubunifu kwa serikali na wakulima ndiyo unaleta umasikini.

SGR investment na uhmizwaji kwa wakulima kufanya kazi vinaenda simultaneously.
points zake huyo ndugu huwa anazitafuta kwa ajili ya kumpinga JPM tu 🤣🤣🤣 !
 
Madhara ya kuiacha ccm itawale miaka yote hii, hakuna direction!
 
Watu wakiitwa wanyonge wanafurahi na wanapiga
Makofi kwa kwa kwa

Ova
 
Unazungumzia kilimo wakati rais mwenyewe (Samia) anatokea kwenye mazingira ya watu wasiopenda kilimo.. zaidi ya kushinda kijiweni huku wakicheza bao na ubishani wa Simba na Yanga.. Tanzania hii tungekuwa na Makabila mfano wa Wasukuma, Wambulu, Wabena ama Waha nchi hii ingekuwa Agriculture hub in Africa
 
Back
Top Bottom