JamiiForums
JF Official Account
- Nov 9, 2006
- 6,229
- 5,285
Bado siku 4 tu kufikia Septemba 21, 2024, ambapo tuzo zitatolewa kwa Washindi wa Awamu ya 4 ya Shindano la Stories of Change (SoC).
Mwaka huu (2024), kupitia maandiko ya washiriki kwa ubunifu mkubwa yamelenga kuboresha mustakabali wa Tanzania kwa kipindi cha Miaka 5-25, kwa kuzingatia Dhima ya Shindano Tanzania Tuitakayo.
Aidha, mbali na tuzo kwa Washindi wa maandiko bora, pia kutakuwa na kutambua mchango wa Wazalishaji Bora wa maudhui ndani ya JamiiForums.com kwa ushiriki wao katika majukwaa.