2024 Watanzania tutaandamana kulazimisha Dkt. Magufuli aongezewe muda zaidi. Umeme wa Stieglers utakapowaka, hospitali, SGR zitaleta shangwe sana

Kitendo cha mtu mmoja kutaka kuongoza watu zaidi ya million 50 kwa miaka mingi ni ishara kwamba watu hao na kiongozi wao hawajitambui
 
JPM amerithi mengi kutoka kwa watangulizi wake na kuyaendeleza. Watakaomfuata nao watarithi ya JPM na kuyaendeleza. Zama za usultani zilishapita zamani.
 
Najitolea kukuroga mapema kabisa kabla haujaanza kuandamana..Tafadhali sana wana JF naombeni huyu mniachie mimi peke yangu nimgeuze tambala la deki, akanyagwe mpaka na mende
Huna sababu ya kujihangaisha. Dr. Bashiru amesema wazi kuwa CCM INATUMIA NGUVU ZA DOLA KUBAKI MADAKANI. Hivyo usimloge mwenzako wala msiandamane. Vyombo vya dola tayari vimo kazini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vurugu ndiyo zitakuwa na chanzo halali kwani sasa hivi wasemaji wanazidi kupaka kinyesi utawala wake.
 
 
Ndiyo mlivyowaza sio.?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…