Moja kwa moja kwenye mada maana nimevurugwa.
Kulingana na mkwamo wa uongozi uliopo madarakani na msimamo wake wa kuziba masikio ili kutosikiliza maoni ya Raia wake (mimi pia nikiwemo), ninaomba Chama chetu pendwa cha Mapinduzi (CCM) kijitafakari na kutuangalizia mbadala atakayebeba mikoba ya huyu aliyopo.
Maana haihitaji utumie nguvu nyingi sana kuona mkwamo wa uongozi wa sasa na kwamba asilimia kubwa ya wananchi hasa wanyonge, hatuuelewi-elewi.
Hivyo nikiwa Raia na mpiga kura, naomba kutoa maoni ya kutoka ndani ya kuta za moyo wangu kwamba CCM kama kweli bado inataka kuendelea kubakia madarakani, basi iangalie mbadala.
Vinginevyo, mtalazimisha mambo hali ambayo inaweza kuleta machafuko katika nchi yetu..
Hebu hekima itokayo kwa Mwenyezi Mungu, ikawaongoze wale wa kwenye kamati kuu, kama walivyoongozwa mnamo mwaka 2015.
Ni matumaini yangu kuwa maoni haya yatafanyiwa kazi kwa mtizamo chanya kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi yetu.
Tanzania imebarikiwa kila kitu isipokuwa viongozi tu hasa wale wa ngazi ya juu..
Kama sisi ni kundi la ng'ombe (kwa mfano tu, japo sisi siyo ng'ombe) basi ng'ombe waliotangulia mbele yetu wana kisirani na wanatembea mwendo wa madaha na wataratibu huku sisi wa nyuma (wananchi wa hali ya chini), tukionewa kwa kutandikwa viboko (tozo + maisha magumu) ili mwendo uongezeke!
Naomba kuwasilisha.