2025; CCM TUANGALIZIENI MBADALA

2025; CCM TUANGALIZIENI MBADALA

Moja kwa moja kwenye mada maana nimevurugwa.

Kulingana na mkwamo wa uongozi uliopo madarakani na msimamo wake wa kuziba masikio ili kutosikiliza maoni ya Raia wake (mimi pia nikiwemo), ninaomba Chama chetu pendwa cha Mapinduzi (CCM) kijitafakari na kutuangalizia mbadala atakayebeba mikoba ya huyu aliyopo.

Maana haihitaji utumie nguvu nyingi sana kuona mkwamo wa uongozi wa sasa na kwamba asilimia kubwa ya wananchi hasa wanyonge, hatuuelewi-elewi.

Hivyo nikiwa Raia na mpiga kura, naomba kutoa maoni ya kutoka ndani ya kuta za moyo wangu kwamba CCM kama kweli bado inataka kuendelea kubakia madarakani, basi iangalie mbadala.

Vinginevyo, mtalazimisha mambo hali ambayo inaweza kuleta machafuko katika nchi yetu..

Hebu hekima itokayo kwa Mwenyezi Mungu, ikawaongoze wale wa kwenye kamati kuu, kama walivyoongozwa mnamo mwaka 2015.

Ni matumaini yangu kuwa maoni haya yatafanyiwa kazi kwa mtizamo chanya kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi yetu.

Tanzania imebarikiwa kila kitu isipokuwa viongozi tu hasa wale wa ngazi ya juu..

Kama sisi ni kundi la ng'ombe (kwa mfano tu, japo sisi siyo ng'ombe) basi ng'ombe waliotangulia mbele yetu wana kisirani na wanatembea mwendo wa madaha na wataratibu huku sisi wa nyuma (wananchi wa hali ya chini), tukionewa kwa kutandikwa viboko (tozo + maisha magumu) ili mwendo uongezeke!

Naomba kuwasilisha.
Shida CCM mnapenda siasa za kinafiki,huyu Bi.Mchele alipaswa aondolewe ata sasa,kwani ni nani alisema ni lazima Rais amalize miaka mitano ndiyo tuchague mwingine,huu upuuzi ni lazima tuachane nao,mtu akiboronga anakaa pembeni!
 
Yaani nani akutafutie Rais.
Komaa wewe fanya kazi zako, hiiyo 2025 hakuna uchaguzi. Samia mpk 2030
 
Naona leo ndo uko zamu halafu umesahau kubadilisha-badilisha ID, maana tunawafahamu tena kwa majina wote mliopewa "asali" ili kuutetea uongozi uliopo kwa gharama ya kuuza uhuru na rasilimali za Watanzania.
Na sisi hatutakubali kuuzwa kirahisi-rahisi walahi.
Wewe ukiandika maoni yako humu sawa, ila wengine wakija na mawazo tofauti na yako wamelamba asali
 
Siyo kweli; imebaki mwaka 1 na miezi michache tu. Hivyo maandalizi ya kumwandaa mgombea asiye na makando-kando ni huu.
Kingine tunahitaji kiongozi ambaye amechangamka-changamka.

Siyo tunaletewa kiongozi hata akisimama kutoa hotuba, havuti usikivu wa watu kwa sababu kapoa utafikiri kiporo cha pilau la muhogo!
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Ni Samia mpaka 2030 tena tutaprint fomu moja tu Kwa ajili yake!!
 
Shida CCM mnapenda siasa za kinafiki,huyu Bi.Mchele alipaswa aondolewe ata sasa,kwani ni nani alisema ni lazima Rais amalize miaka mitano ndiyo tuchague mwingine,huu upuuzi ni lazima tuachane nao,mtu akiboronga anakaa pembeni!
Acha upuuzi Samia hajaboronga kwanini utulazimishe sie wanaccm kumtoa mwenyekiti Lulu kama dk Samia?
 
Hajaboronga kweli?!
1. TOZO
2. MAISHA MAGUMU
3. KUZIBA MASIKIO KUSIKILIZA MAONI YA RAIA
4. MIRADI KUSUA-SUA IKIWEMO SGR & JNHPP
5. WAANDAMIZI MAFISADI
6. REPOTI MBAYA YA CAG
7. KUUZWA KWA BANDARI ZA TANGANYIKA
8. RAIA WENGI KUKOSA IMANI NAYE
9. MIKATABA YA OVYO
10. SAFARI NYINGI ZA NJE ZISIZO NA TIJA N.K
 
Back
Top Bottom