NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,925
Yes, 2025 mimi mkuu wa kaya, mke wangu na house girl ambao ndio watu wazima kwenye nyumba hii nimepiga marufuku kwenda kupiga kura, kama ataongezeka mwengine awe tayari kuyakubali haya masharti.
Kipindi pekee ambacho nilipiga kura walau kwa matumaini hasa katika nafasi za wabunge na madiwani ni cha kikwete wakati anaaga 2015 ikiwa ndio mara yangu ya kwanza kupiga kura nikiwa na miaka 20, .
Ccm mmecheza kama pele kwenye kuhakikisha uongozi unabaki kwenu, kwa hili wala nisijivunge nawapigia salute, hata upinzani mmejua kuubana kwakweli, kwa awamu hii angalau mnawabana kistaarabu ila bado lengo ni lile lile, Big up sana kwenu.
Ya nini kwenda kujisumbua kupiga kura wakati wasimamizi, wanaohesabu na wanaotangaza wapo ccm, hivi kweli kabisa niamke asubuhi eti naenda kupiga kura ? Matokeo tayari yashajulikana kuna nini unaenda kufanya huko kwenye kura, hio tiki ya kuijaza kwenye fomu ya kupiga kura bora nimpe mtoto wangu maswali hata mepesi nianze kumsahishia kwa kumpa tiki.
Kama upo ccm tayari jua ishashinda wala hakuna haja kwenda kupiga kura, kama upo upinzani tegemea kuwa surprised, ukiamini kwamba ukubwa wa makusanyiko kwenye kampeni za upinzani ndio matokeo imekula kwako hio, ukiamini kwamba mnaoenda kupiga kura wengi ni upinzani it doesn't matter.
Na huu mchezo ulivyo sasa umeboreshwa na kunogeshwa zaidi na kuingia zaidi hata ndani ya chama, jana hata chaguzi za chama nafasi za mwenyekiti, makamu mwenyekiti bara na makamu mwenyekiti zanzibar walipita bila kupingwa, ni raha isiyo ni kifani, mchezo huu umeshaanza kuwa mazoea na 2025 sitashangaa ukijirudia na kuwa zaidi ya 2020 kwa watu katika nyadhifa kibao kupita bila kupingwa na wapinzani kuwekwa pembeni kwa kukosea kuandika barua ama kujaza form.
Ya nini niende kunisumbua kupiga kura, yani hio 2025 ntakuwa bize na kazi zangu tu, siku ya kura hakuna wa kwenda kupiga kura hapa kwangu.
Dedication: Jecha style