2025 Tanzania itafanya uchaguzi au tutegemee marudio ya 2020?

2025 Tanzania itafanya uchaguzi au tutegemee marudio ya 2020?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Kipenga kimepulizwa kwamba tupo Hadi 2030, hapo Bado miaka minne kuelekea uchaguzi.

Je, 2025 tutegemee uchaguzi au tubaki kusubiri uchafuzi? Kibaya zaidi kamati inayojadili mambo ya Muda mfupi ,Kati na mrefu ikiwa na akina Zitto ndiyo hiyo iliyompa baraka hizo mwenye nchi Kwa niaba ya watanzania bila hata kutumwa na wananchi.

Uchaguzi utakuwepo? Kama utakuwepo vyama vilivyofika ikulu Jana vitakuwa upande Gani na Mwenyekiti wao?

Chadema ataweza kupambana na dola,CCM na vyama shikizi? Na kama inatamani kupambana nao, hakuna haja yakuanza harakati Sasa Kwa kudeploy timu majimboni kuanza kuelimisha umma?

Si wakati muafaka wanavyuo kuanza kujinyoosha tayari Kwa kuanza safari mpya ya ukombozi? Ikumbukwe CCM haitaweza kufanya harakati zozote Kwa sababu wanaamini Rais akiwa madarakani awezi kushindwa; ila sanduku la kura linawenyewe.
 
Dalili zinaonesha yatakuwa ni marudio ya 2020 ila hayo ya mwaka 2025 yatakuwa yamelegezwa kidogo, wapinzani sampuli ya kina Zitto watapewa majimbo kadhaa yakuwafunga midomo waje kusema uchaguzi ulikuwa huru na haki.
 
Back
Top Bottom