2025 tukichaguana kwa U-Simba na U-Yanga, nani ataibuka mshindi?

Hata mimi binafsi nashangazwa na tabia hii ya kuingia na mabango ya kusifia viongozi wa kisiasa ambayo imeota mizizi hasa kwenye timu niipendayo ya yanga. Kukiwa na mechi mara asante Rais kwa kufanya hiki au kile! Kuna vitu vizuri vingi amefanya Rais na serikali yake na watu wameviona au wanaviona kuna sababu gani ya msingi watu mnaanza kuingia na mabango uwanjani ambako kila mtu huko ana itikadi yake. Je akina Rungwe mzee wa ubwabwa wafuasi wao wakianza kuingia na mabango ya kuhusu ubwabwa Wallace Karia na wenzio mtavumilia?
 
Huku ni kudhalilisha viongozi, hebu ona yule mpenzi wa simba aliyetandikwa bao 5-1 pamoja na kwamba amebebelea bonge la picha ya Samia!! 🀣
 
Huku ni kudhalilisha viongozi, hebu ona yule mpenzi wa simba aliyetandikwa bao 5-1 pamoja na kwamba amebebelea bonge la picha ya Samia!! [emoji1787]
Leo hao watani wamelala na viatu na usiku ulikuwa mrefu balaa.Naipenda yanga ila iache kujihusisha na siasa itawagawa mashabiki wake
 
Rage,Kapuya,Tulia,Lusinde nk ni Simba
 
Yanga ataibuka mshindi[emoji23]

CCM wote Yanga

Mbowe, Tundu Lisu, Halima Mdee Yanga

Abdul Nondo Yanga

Mdude Yanga[emoji3]

Wastaafu Mwinyi na JK Yanga [emoji3]

Mo Yanga [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji91][emoji91][emoji209]
Zito Kabwe
 
Hilo halitaondoa Mashabiki kufurahia na kuondoa umoja wao. Kumbuka kila shabiki wa YANGA/SIMBA ana chama anachokikubali. Hao wajinga wanalijui hilo, ndio maana wanaleta maswala ya uvyama wakiamini wanaweza kuawavuruga kwa hilo.
 
Hivyo vitu havitokei kwa bahati mbaya, hao watu wanaandaliwa na kupewa mabango.
Kwa kifupi hivyo vilabu vyote vya kariakoo vina nasaba na chama tawala.
 
Hivyo vitu havitokei kwa bahati mbaya, hao watu wanaandaliwa na kupewa mabango.
Kwa kifupi hivyo vilabu vyote vya kariakoo vina nasaba na chama tawala.
Zamani haikuwa hivyo, Awamu hii ya mpito ndo Ina mambo hayo!!
 
Tunajua kuwa Mwenyewe hata Mambo ya Mpira hayajui ila Wewe ukiongozwa na Yule Mnafiki mkubwa mwenzenu wa Pwani na Kawe Beach mmemlazimisha apende Mpira na aipende zaidi Yanga SC yenu.

Sawa na Sisi Simba isiyo ya Samia tunasema tu kuwa tukutane katika Uchaguzi Mkuu wa 2025 kwani huenda Machungu yetu ya Kutengwa, Kunyanyaswa na Kupuuzwa na wale Wanaoipenda Yanga SC tu tukayatolea hapo hapo na tukaanza Kuheshimiana.

GENTAMYCINE nimeshaonya mara kwa mara hapa Jamiiforums kuwa Viongozi mlioko Serikalini / Madarakani mkishalewa Pombe zenu msikimbilie Kukurupuka kutoa Kauli za Kuwagawa Watu ( Watanzania ) hasa Kisiasa kwani ni Hatari sana na msifanye nalo Mzaha hamsikii.

Haya Kwako Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ( ambaye ni mwana Yanga SC lia lia ) umemsikia Mwigulu Nchemba anasema Yanga SC hii ni ya Samia na CCM? Je, nawe uko ndani yao?

Mbowe kwakuwa hata Rangi za Chama chako cha CHADEMA zinasadifu zile za Klabu yangu ya Simba SC nashauri hebu mrudishe Chamani Genius Dk. Wilbroad Slaa, nitafute GENTAMYCINE nikupe Strategies kisha anza kuwa karibu na Mashabiki wa Simba SC na nakuhakikishia Uchaguzi Mkuu wa 2025 CHADEMA yako kinashinda na Dk. Slaa anakuwa Rais wa Tanzania.

Siyo kila mwenye PhD basi ana Akili.
 
Mmeendelea na Taifa stars tena,
 
Freemasons watakuwa wamefeli wakirihusu hili kutokea.
Wana mbinu nyingi za kiwagawa watanzania.

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Wapenzi wa Yanga nchi nzima ni asilimia 54 na Simba 46. Tafuta jibu sasa.
 
Mpira ni Burudani lakini kwenye Nchi hii unatumika pia KUPUMBAZA Masikini.

Kama leo Wanayanga wengi wamelala na NJAA lakini WAMEFURAHI.
Wanapikiwa Supu wanasafiri kilomita 30 kuja kunywa supu nauli ya kuja na kurudi Tsh.20000/= Je hiyo Tsh 20000/= angekunywa supu ngapi huko kwako?
Kweli wajinga wapo wengi sana Nchi hii

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…