2025 ufanye nini? Kutoka kwa Mwalimu Mwakasege

emmarki

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2012
Posts
1,001
Reaction score
1,430
Salamu za Mwaka Mpya
Wa 2025
Toka kwa Christopher Mwakasege
1. Nakusalimu katika jina la Yesu Kristo, aliye Bwana na Mwokozi wa maisha yetu. Tunamshukuru Mungu sana, kwa kutupa neema yake ya kuingia katika mwaka huu wa 2025.
2. Mungu amekuwa akinisemesha juu ya mambo kadha wa kadha, yanayokuja mwaka huu wa 2025. Kati ya mambo hayo, ni hili alilonisemesha moyoni mwangu ya kuwa: “Inawapasa kumwomba Mungu siku zote, na wala msikate tamaa”.
3. Niliposikia maneno hayo moyoni mwangu, nilikumbuka maneno ambayo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, ya kwamba: “Imewapasa kumwomba Mungu siku zote, wala wasikate tamaa” (Luka 18:1). Moyoni nikasukumwa kusoma na kutafakari maneno ya Luka 18:1 – 14. Na nilipoyasoma, Mungu akanisemesha kwa undani zaidi.
4. Ni kawaida yangu, mara kwa mara, kumwomba Mungu nipate kujua juu ya mambo yaliyobebwa na miaka iliyo mbele yetu, na kujua anachotaka tufanye (Isaya 45:11 na 1Mambo ya nyakati 12:32). Na ndipo, kati ya mambo mengi aliyonisemesha kuwa yanakuja, ni hili ninalokushirikisha katika salamu hizi.
5. Kufuatana na ufahamu nilioupata, nikajua ya kuwa:
• Kuna mashambulizi yanayokuja kwenye mioyo ya watu, ili wapoteze umuhimu wa haki zao toka kwa Mungu katika maisha yao na wazipuuzie. Kufuatana na Luka 18:1 – 6, kuna haki inayotakiwa ipatikane “kisheria”. Na katika Luka 18:7 – 14, kuna haki inayotakiwa ipatikane “kimaombi”.
6. Mifumo ya kisheria isipozaa haki, basi inazaa “udhalimu” (Luka 18:5). Na mifumo ya kiroho isipozaa haki, basi inazaa “kujihesabia haki” (Luka 18:11, 12). Lakini Roho Mtakatifu anatuhimiza na kutusemesha ya kuwa: “Imetupasa kumwomba Mungu siku zote, na wala tusikate tamaa” (Luka 18:1).
7. Hii ni kwa sababu, ukitafakari vizuri maneno ya Yesu katika Luka 18:1 – 6, huku unalinganisha na Luka 18:7 – 14, utaona ya kwamba, pale ambapo “sheria” inashindwa au inachelewesha haki yako, maombi yako kwa Mungu, yanampa Mungu fursa ya kuingilia kati na kukupa haki yako unayoistahili!
8. Ni muhimu sana uingie katika mwaka huu wa 2025, ukiwa na Lengo la kuongeza Msukumo moyoni mwako wa kuombea haki zako – kifamilia, na kikazi, na kibiashara, na kitaasisi, na kieneo, na kitaifa, na kiulimwengu! Pia, weka lengo la kuongeza muda wa kukaa katika maombi juu ya jambo hili. Na weka lengo la kuimarisha imani yako, juu ya kujibiwa kwa maombi yako hayo (Luka 18:1, 7,8)
9. Nimeona kwa watu wengi, kunakuja msukumo utakaokuwa ukiongezeka, juu ya kuimarisha imani za watu katika kumwamini Mungu, juu ya kujibu maombi yao! Ila pia, nimeona zikija hali za namna nyingi zinazolenga kuwakatisha tamaa watu, ili wasiendelee kuomba, na waache kumtegemea Mungu. Roho Mtakatifu asingesema tumwombe Mungu, wala tusikate tamaa, ikiwa jambo la kukatisha tamaa tusiendelee kuomba halipo! Lakini tumshukuru Mungu kwa kutujulisha mapema!
10. Ikiwa unasoma salamu hizi, ujue pia nimekuombea ya kuwa, Mungu aulinde moyo wako, usije ukaacha kuomba, wala usikate tamaa, na wala usikatishwe tamaa kuomba. Wakati wa semina ya kufungua mwaka ya Arusha tarehe 8 – 12 Januari 2025 – nitafafanua zaidi juu ya mazingira hayo ya kukatisha tamaa usiombe, na mambo yakufanya ili usikate tamaa, wala kukatishwa tamaa na mazingira hayo.
11. Mimi na mke wangu, na watoto wetu, na timu nzima ya huduma ya MANA, tunakushukuru kwa kusimama nasi katika huduma mwaka 2024. Tunamwomba Mungu tukiamini ya kuwa, atakupa neema ya kusimama pamoja nasi tena, katika huduma ya mwaka 2025.
12. Tunakuombea, na kukutakia mwaka 2025 wenye baraka zaidi, kuliko mwaka 2024! Tuzidi kuombeana!
 
Haya mahubiri ni ya kwako usiingize maneno kwa Mtumishi wa Mungu Mwakasege! Kwanza Mwakasege pamoja na kutumia neno, hatumii wingi wa neno kuwachanganya waumini! Haya maelezo ya kwako! Tunaomfahamu Mwakasege tunajua sauti yake!
 
pita kwenye Facebook page yake, Christopher & Diana Mwakasege (MANA Ministry), urudi uombe msamaha kwa kunishambulia
 
Back
Top Bottom