2030 Itafika, hakuna katiba mpya, hakuna tume huru ya uchaguzi na uchaguzi utafanyika na CCM itaendelea kuongoza na maisha yataendelea

kiroka

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2018
Posts
417
Reaction score
1,999
Huu ni ukweli mchungu, kwa mazingira tulio nayo na siasa za chadema kwa sasa Itafika 2030 tupo hivi hivi,..

Ukawa walifanya kosa kubwa sana mwaka 2012/13 kususia bunge la katiba kwa kigezo kikuu Cha serikali tatu, huu ni uroho wa madaraka unawagharimu Leo
Kama ukawa wangekubali kipindi kile kucompromize tusingekua hapa tulipo, Jakaya alionesha Nia kabisa ya kutaka tupate katiba mpya lakini ujuaji mwingi umetufikisha hapa

Ukiwa unamdai mtu laki Moja akikupa 50 Leo pokea kesho ukirudi haudai laki utadai 50,ambayo ni ndogo kuliko laki,tungekubaliana miaka Ile Leo Kuna vitu vingi vingekua vimebadilka sema Hawa chadema wanavitaka vyote kwa pamoja kitu ambacho ni kigumu, ccm hii ilojijenga kwa zaidi ya miaka 50 huwezi kuiangusha kwa siku Moja inahitaji kuibomoa kidogo kidogo

Leo tunataka katiba mpya, lkn hatujakubaliana tunaanzia wapi, je tunaanzia kukusanya maoni au kwenye maoni ya jaji warioba au kwenye rasimu ya bunge, hapa lazima tukubaliane pande zote, mkwamo tayari

Ukifika 2029 hatuna katiba mpya Wala tume huru ya uchaguzi na chadema wataendelea kushikilia msimamo wao wa no reforms no election baadhi ya wanachama wataondoka chadema wakashiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwenye vyama vingine na Ile kukata wagombea haitakuepo na wengi watashinda kwenye vyama pinzani, kufika 2030, Ngoma tena itawekwa uwanjani bila chadema, ccm itaibuka mshindi na rais mpya wa ccm nae atakuja na mambo yake maisha yataendelea.

Mwisho kile kilichotokea October 29 serikali imejifunza na wanaotaka kuvuruga uchaguzi wamejifunza, hakuna mtu atatoka barabarani tena siku ya uchaguzi na siku ya uchaguzi haitakua ya kawaida kama miaka ya nyuma ulinzi utaimarishwa Kila Kona.
 
Chadema bado hawajatangaza kuachana na No Reforms No Election. Huo ndio mwiba wao kwa sasa.
 
2030 Mama nasikia ana gombania tena ccm wanasema Nyerere alikaa miaka 25 kwanini mama nae asifanye kama Nyerere?.
 
Back
Top Bottom