Kasomi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 11,030
- 20,391
Krismasi (pia Noeli) ni sikukuu ambayo Wakristo wengi husheherekea kuzaliwa kwake Yesu Kristo zaidi ya miaka 2000 iliyopita.
Kuna majina mawili yaliyo kawaida kwa Kiswahili kwa ajili ya sikukuu hii:
1- Krismasi inatokana na neno la Kiingereza lenye maana ya "Christ`s Mass" yaani misa au ibada ya Kristo.
2- Noeli inatokana na neno la Kiingereza "Noel" (au "Nowell") ambalo limepokewa kutoka lugha ya Kifaransa "Noël". Hilo ni ufupisho wa neno la Kilatini "Natalis (dies)", "(siku ya) kuzaliwa".
Lakini baadaye Ukristo ulienea katika Dola la Roma kati ya mataifa yaliyokuwa na kawaida ya kuzingatia siku ya kuzaliwa. Hivyo ilijitokeza hamu ya kusheherekea pia sikukuu ya kuzaliwa kwake Kristo. Ndiyo asili ya sikukuu ya Krismasi.
Tangu mwanzo wa karne ya 3 BK kuna kumbukumbu ya waandishi mbalimbali waliojadili tarehe ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo.
Habari za kwanza kabisa za makadirio ya tarehe ya kuzaliwa kwake Yesu zinapatikana kutoka Misri mnamo mwaka 200 BK. Mwandishi Mkristo Klemens wa Alexandria alilalamikia udadisi wa wataalamu kadhaa wa Misri waliodai kwamba wamekadiria tarehe hiyo katika mwezi Mei, wengine katika Aprili. Alisema pia kuwa kikundi cha Kikristo cha wafuasi wa Basilides huko Misri walisheherekea Epifania pamoja na kuzaliwa kwake Yesu tarehe 6 Januari.
Lakini kadirio la tarehe 25 Desemba lina asili katika Misri pia. Kuanzia mwaka 200 (kwa mara ya kwanza katika maandishi ya Sixtus Julius Africanus) wataalamu nchini Misri waliona tarehe 14 Nisan ya kalenda ya Kiyahudi ambayo ni sawa na 25 Machi ilikuwa tarehe ya kufa kwake Kristo na pia siku ya utungaji mimba wake. Kwa kuongeza miezi tisa ya mimba inajitokeza 25 Desemba kama tarehe ya kuzaliwa.
Inaonekana tarehe 25 Desemba ilijitokeza wakati huo. Kuna taarifa ya mwaka 204 kutoka Ipolito wa Roma kwamba tarehe 25 Desemba ilikuwa sikukuu ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo.
Happy Christmas day
Kuna majina mawili yaliyo kawaida kwa Kiswahili kwa ajili ya sikukuu hii:
1- Krismasi inatokana na neno la Kiingereza lenye maana ya "Christ`s Mass" yaani misa au ibada ya Kristo.
2- Noeli inatokana na neno la Kiingereza "Noel" (au "Nowell") ambalo limepokewa kutoka lugha ya Kifaransa "Noël". Hilo ni ufupisho wa neno la Kilatini "Natalis (dies)", "(siku ya) kuzaliwa".
HISTORIA YA CHRISTMAS
Hakuna uhakika ni lini Krismasi ilianza kusheherekewa. Ni sikukuu ya kale katika Ukristo lakini haikuwepo tangu mwanzoni. Tarehe halisi ya kuzaliwa kwake Yesu haijulikani kwa sababu utamaduni wa Wayahudi wa wakati ule haukuwa na sherehe au kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa.Lakini baadaye Ukristo ulienea katika Dola la Roma kati ya mataifa yaliyokuwa na kawaida ya kuzingatia siku ya kuzaliwa. Hivyo ilijitokeza hamu ya kusheherekea pia sikukuu ya kuzaliwa kwake Kristo. Ndiyo asili ya sikukuu ya Krismasi.