+255 Champion Boy, Mbwana Samatta atajwa kama mchezaji wa kuangaliwa baada ya kufanya maajabu

+255 Champion Boy, Mbwana Samatta atajwa kama mchezaji wa kuangaliwa baada ya kufanya maajabu

Nadhani ni fursa kwa DSTV Dicoder kuweka mkataba na Mbwana Samatta ili kutufanya sisi Wapenzi wake tununue ving'amuzi vyao
 
Goooo Samagoal...

Akicheza england nahisu nusu ya watanzania tutapeleka ushabiki kwenye hiyo timu

Tatizo wachezaji wa Afrika wakienda Uingereza wanapaswa kuangalia ni timu ipi itawanufaisha kimpira na kimaslahi.

Wapo wachezaji kama Asamoa Gyan ambae imebidi aende China kwa kushindwa kufurukuta.

Pia yupo Saido Berahino ambae yule meneja wa West Brom alitaka aozee kwenye bench.

Romelu Lukaku ni mfano mwingine kwamba alipokuwa Chelsea Mourinho aliamua kumpeleka timu ingine kucheza kwa mkopo na nafikiri umemwona sasa yupo Everton na ana thamani ya 60M pauni kwa kuwa mshambulaji wa kutisha.

Wachezaji wa Afrika na khasa Tanzania ni timu za ligi ya daraja la kwanza ndizo zinawafaa kwa kuanzia na baadae wakizoea wanaangalia ligi kuu.

Au zile timu za katikati kama Everton, Stoke City, West Ham na Bournemouth.

Timu za daraja la kwanza kuna zile top 10 ambazo zina uwezekano wa kupanda daraja kwenda ligi kuu.

Ila Mbwana Samatta sasa amefungua njia kwa wachezaji wengi wazuri kuceza katika ligi za kimataifa barani Afrika na baadae kupata nafasi ya kwenda huko ughaibuni.
 
Samatta 77 kwa epl nampeleka Southampton/ Tottenham halafu Chelsea
 
Nitapenda kama kina samata wa tano watoke serengeti boys, na imani heshima kwa nchi kimchezo
 
Samata bado sana! Nasema bado sana japo amejitahidi lakini hajafikia level ya kuw mchezaji maarufu. Hata club na nchi anazochezea si za level kubwa. Wasiwasi wangu tukianza ''kumtukuza'' kwenye level hii na yeye atajiona amefika na kuishia hapo. Tunataka tumwone mwakani akipata club ya lvel ya juu na yenye ligi ya ushindani zaidi. Kwa level hii aliyo sasa kuna nchi nyingi za Afrika zimeshatoa wachezaji hivyo tujitahidi kupunguza kelele ili tusionekane malimbukeni sana!
Sikusapoti. Kila anaefanya mazuri apewe pongezi zake hapo hapo. Hakuna MTU aishie milele. Level aliyoifikia Samata hakuna mchezaji Wa soka nyakati hizi kwa hapa bongo . tunatakiwa tumpongeze na kumpa hamasa ya kusonga mbele na haipaswi kuacha kumpongeza et kwa kuogopa atalewa sifa. Vip ikiwa halewi hizo sifa na hatujampongeza hauoni kama hatutamtendea haki?
 
Uzi mzuri lakini sijui kama hautachafuka!
 
huyu jamaa ni fundi sna but akitaka a2sue zaidi ni bora akaanzia france kbla ya kwend kweny ligi ngum zaid ila EPL simshauri!!
EPL ina ugumu gani!!!? De bruyne, Ndindi na wengineo wametoka club aliyopo samatta na bado wanakimbiza Epl. Acheni upinzani wa kichawi!!! Mbwana ameiva na ni wakati sahihi kuingia EPL, LAlLIGA au ligi yoyote ile Duniani. Kwa taarifa yako Genk ya samatta imeitoa Gent europa league na ukumbuke hiyo gent iliyotolewa na Genk ndiyo iliyoitoa Totenham ya ligi yenu pendwa ambayo ni yapili kwenye msimamo pale EPL. Acheni uchawi...
 
Checking...100%
Searching...100%
Network connected !

Near by Igawilo Mbeya.
 
Wanakuwa na mibalaa, halafu ni kosa sana eti ukishakuwa star unamuacha yule demu wako ulokuwa naye awali na alikupenda hata kabla hujawa star unakimbilia kwa wenye nuksi hao unajua hiyo inakuwa kama laana mambo yanaeza yasikunyokee tena.
acha uongo ww ukipata pesa tafuta mwanamke wa hadhi ya juu
 
EPL ina ugumu gani!!!? De bruyne, Ndindi na wengineo wametoka club aliyopo samatta na bado wanakimbiza Epl. Acheni upinzani wa kichawi!!! Mbwana ameiva na ni wakati sahihi kuingia EPL, LAlLIGA au ligi yoyote ile Duniani. Kwa taarifa yako Genk ya samatta imeitoa Gent europa league na ukumbuke hiyo gent iliyotolewa na Genk ndiyo iliyoitoa Totenham ya ligi yenu pendwa ambayo ni yapili kwenye msimamo pale EPL. Acheni uchawi...
Mkuu kuna tweet niliiona ya wakala mmoja wa Juventus wanasema kwamba mwakani wataanza kumpigia misele Samatta.

Lakini binafsi naona kama Samatta hana tena haja ya kutafuta timu ya daraja la kwanza kama wengi wanavyopendekeza hapa, yule tayari amesha kwiva hebu tazama muda alioingia Genk na mambo anayoyafanya sasa hivi... Wenzake kutoka west Africa wanatumiaga hadi misimu mitatu kuanza kuonyesha cheche zao lakini yeye msimu mmoja tu tayari ameshajitengenezea uhakika wa namba.

Kingine, wewe unahisi Samatta anastahili kuendelea kuwepo pale hata kwa msimu ujao?
 
Samata bado sana! Nasema bado sana japo amejitahidi lakini hajafikia level ya kuw mchezaji maarufu. Hata club na nchi anazochezea si za level kubwa. Wasiwasi wangu tukianza ''kumtukuza'' kwenye level hii na yeye atajiona amefika na kuishia hapo. Tunataka tumwone mwakani akipata club ya lvel ya juu na yenye ligi ya ushindani zaidi. Kwa level hii aliyo sasa kuna nchi nyingi za Afrika zimeshatoa wachezaji hivyo tujitahidi kupunguza kelele ili tusionekane malimbukeni sana!
Acha longolongo wewe tatizo umekariri hujui kuna maagent wanazunguka ligi za ulaya kuangalia talents. Usije shangaa jamaa yupo bundesliga timu kama FC Schalke inamfaa.
 
Tanzania tunawachezaji wazur sana tatizo mpira wa bongo umejaa siasa , na unafiki ndio maana soka letu halikui. Hongera sana samata kwa malengo na juhud ulizo jiwekea, we ni mfano wakuigwa
 
Back
Top Bottom