Uchaguzi 2020 28 Oktoba vita ya ama zao, ama zangu; kiama chao, ama changu; chama chao, ama changu. Amiri Jeshi Mkuu katangaza vita, watoto wa mama wanachonga sana!

Uchaguzi 2020 28 Oktoba vita ya ama zao, ama zangu; kiama chao, ama changu; chama chao, ama changu. Amiri Jeshi Mkuu katangaza vita, watoto wa mama wanachonga sana!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Uchaguzi ni wakati mzuri wa kufanya tafakari mbalimbali, saa hizi niko mji kasoro, kwenye kiwanja kipya kinaitwa Star Park, mimi kama kawaida yangu, ni mimi na Joni Mtembezi, kiwanja hiki, Night Shift wanaingia mapema! Hivyo kwa wale wenzangu na mimi ambao macho hayalali njaa, kiwanja hiki wanashiba mapema!

Zimepigwa Old is Gold zikanikumbusha mbali mara ukapigwa wimbo wa King Crazy GK wa East Coast featuring Lady JD wa Ama Zao Ama Zangu.



Wimbo huu umenifikirisha sana kuhusu uchaguzi wa mwaka huu, mambo ya uchaguzi huu wa tarehe 28 October, ni kama vita kubwa ya

"Ama Zao, Ama Zangu"
"Kiama Chao Ama Changu"
"Chama Chao Ama Changu"


Amiri Jeshi Wetu Mkuu, Tayari Ameisha tangaza vita kuu ya tatu ya mapinduzi ya uchumi kujenga Tanzania ya viwanda, Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati, sasa iweje bado kuna hawa watoto wa mama wanachonga sana?

Nimejaribu kutafuta lyrics za huu wimbo zikufanikiwa kuzipata. Wengi wanaonijua humu JF, wananijua Pasco Mayalla kama mwandishi wa habari wa kujitegemea, lakini sio wengi humu wanajua kuwa Pasco Mayalla pia ni Mtangazaji wa Television kwa miaka 10, toka 1995- 2000, DTV na 2000-2005 TBC.

Ila kabla sijawa mtangazaji wa TV, nilikuwa Mtangazaji wa Redio, Radio Tanzania Dar es Salaam, RTD, mwaka 1990-1995, nikiwa Radio DJ, nikitangazia External Service. Enzi hizo kuna baadhi humu walikuwa sio hawajazaliwa bali hata hawajafikiriwa kuzaliwa!

Pale RTD, wimbo hauwezi kupokelewa bila kwanza kuwasilisha lyrics, hivyo kulikuwa na vipaji kibao wanaimba ad lib, lakini hawajui kuandika, hivyo nimesaidia sana kuandika lyrics za nyimbo kibao pale RTD.

Kufuatia wimbo huu kunigusa, na kukuta hauna lyrics, kama Joni Mtembezi asiponizidia, nitakushushia lyrics zake, na kukuambia uusikilize upya with uchaguzi Mkuu huu in your mind utadhani Mwana FA anamuimba mtu!

Hii sio mara yangu ya kwanza kuhusianisha nyimbo na uchaguzi.

Hizi ni rejea zangu:
Leo nimemkumbuka mwanamuziki Kikumbi Mwanza Mpango, King Kikii, aliposema "Tushike ya kwetu, tusiwape muda karagosi", karagosi ni nani?

Umechoshwa na Ujinga, Umasikini, Maradhi, Rushwa na Ufisadi? 25/10 "Give It, "Just One More Try!"

Kwa Wapenzi wa Muziki: "Bado tunapanda, Tunapanda milima, Najua tutafika, Tutafika lazima!"


Pasco
 
umepoteza dira umekuwa kama buku 7
Mtu akiwa na mawazo tofauti nawe haimaanishi kapoteza dira, tatizo wengi mnao shabikia upinzani mnaongozwa na hisia hamfanyi analysis za kutosha juu ya maneno yanayosemwa na viongozi wenu, mfano "mnataka maendeleo ya watu na sio vitu" wakati kipimo cha maendeleo ya mtu ni pamoja na vitu anavyomiliki...
 
Pascal Mayalla, kayanda kane, we need change.


Tunataka katiba mpya ambayo itampunguzia Msukuma mwenzetu madaraka, tunataka freedom of speech, Sheria zilizopo nyingi zinatakiwa kuangaliwa upya, tunataka bunge huru, mahakama huru, ambayo hamna zuzumagic yeyote anaweza kuingilia. We need new Tanzania
 
Wanabodi,

Uchaguzi ni wakati mzuri wa kufanya tafakari mbalimbali, saa hizi niko mji kasoro, kwenye kiwanja kipya kinaitwa Star Park, mimi kama kawaida yangu, ni mimi na Joni Mtembezi, kiwanja hiki, Night Shift wanaingia mapema! Hivyo kwa wale wenzangu na mimi ambao macho hayalali njaa, kiwanja hiki wanashiba mapema!..

Pasco
ad lib
/adˈlɪb/

adverb
  1. 1.
    without previous preparation
 
Back
Top Bottom