2nd Agritech Tanzania youth in Agribusiness conference at Mlimani City

2nd Agritech Tanzania youth in Agribusiness conference at Mlimani City

KOMBAJR

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2011
Posts
5,827
Reaction score
1,271
Heshima kwenu wanabodi,

Nimekutana na hii taarifa ya Mkutano wa Vijana ambao wanafanya Kilimo biashara na Maonyesho ya technolojia na vifaa vya kilimo ambayo yanafanyika kwa mara ya pili hapa nchi. Hii ni fursa kwa vijana ambao wapo kwenye kilimo kukutana na waonyeshaji kutoka nje ya nchi kujione technolojia mbali mbali ambazo zinaweza kuwasaidia katika kubadilisha shughuli zao na kuongea tija.

Pia itatoa fursa kwa vijana ambao wanataka kuingia katika shughuli za kilimo kujifunza jinsi wenzao ambao wamefanikiwa katika nyanja ya kilimo..

Mkutano huu wa Siku Mbili utawakutanisha vijana wapatao 500 kutoka mikoa mbali mbali, viongozi kutoka serikalini,sekta binafsi,asasi za kiraia,watafiti,taasisi za kifedha na mashirika ya kimataifa lengo likiwa ni kujadili kwa pamoja changamoto mbali mbali ambazo vijana wanakumbana nazo katika shughuli za kilimo.

Lengo la Mkutano huu ni kuwapatia fursa vijana kutambua fursa mbali mbali zilizopo kwenye kilimo na kuchangia mawazo ni kwa jinsi gani serikali kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wanaweza leta mazingira wezeshi katika kilimo.

KILIMO KINALIPA, JAWABU LA AJIRA, VIJANA TUCHANGAMKIE FURSA .....

Date: 2015_ 9th- 10th April, 2015

Venue: Mlimani City

nilisoma makara moja hivi kuhusu hili tangazo na nikaona kuna mahara inaitajika gharama ya kiingilio vipi hii imekaaje mkuu
 
nilisoma makara moja hivi kuhusu hili tangazo na nikaona kuna mahara inaitajika gharama ya kiingilio vipi hii imekaaje mkuu

Inawezekana mkuu!hao waleta mada hii unafikiri wanajua kilimo zaidi ya kuongea tu
 
nilisoma makara moja hivi kuhusu hili tangazo na nikaona kuna mahara inaitajika gharama ya kiingilio vipi hii imekaaje mkuu

Mkuu ni kweli gharama kwa siku mbili ni Tsh. 250,000/- ambayo inajumuisha break fast, lunches na materials ila kama unaovyoona kwenye hiyo link hapo waaandaji wanajaribu kutafuta wafadhili ambao wanaweza kuchaingia kidogo ili vijana wengi wanufaike kwa maana walipe nusu ya hiyo 250,000/- we jaza hiyo fomu unaweza kuwa miongoni mwa watakao nufaika. Msingi hapa ni Vijana wa kitanzania wanufaike na waone kilimo kinalipa na siyo bodaboda!
 
Mkuu, usajili unafanyika kwa njia gani? Hiyo link mbona sokoni?

Vv
 
Mkuu, usajili unafanyilka wapi, hiyo link unayosema mbona haionekani?

Vv
 
Gharama kubwa sana.

Muda upo, hata mimi ningehudhuria japo nipate experience ya modern agriculture.

Ila kwa hiyo pesa, wasubiri kwanza.
 
Mkuu ni kweli gharama kwa siku mbili ni Tsh. 250,000/- ambayo inajumuisha break fast, lunches na materials ila kama unaovyoona kwenye hiyo link hapo waaandaji wanajaribu kutafuta wafadhili ambao wanaweza kuchaingia kidogo ili vijana wengi wanufaike kwa maana walipe nusu ya hiyo 250,000/- we jaza hiyo fomu unaweza kuwa miongoni mwa watakao nufaika. Msingi hapa ni Vijana wa kitanzania wanufaike na waone kilimo kinalipa na siyo bodaboda!

Je kama nitajitegemea kila kitu ikiwa ni chakula na malazi bado nitatakiwa kulipa kiasi chochote?
 
Back
Top Bottom