3 Years Review: Bajaj Boxer Bm 150X

3 Years Review: Bajaj Boxer Bm 150X

Ukitaka kuipaki boxer pasipo kuitumia kwa muda wa kama miezi minne u atakiwa ufanyaje ili utakapokuja kuitumia tena iwe in gud comdition
 
Watu wengi wanaziogopa sana boxer lakn n bonge la boda ...sema inahitaj mtu anayejielewa. Spair pia og zmechangamka ninalo kama la mtoa post aseee mhindi hapa alicheza kama pele...hutataman kuendesha mchina yoyote ukiachana na speed,power boxer haina overheating na vibration za hovyo kama boda za mchna
 
Ukitaka kuipaki boxer pasipo kuitumia kwa muda wa kama miezi minne u atakiwa ufanyaje ili utakapokuja kuitumia tena iwe in gud comdition
sio Boxer tu hata pikipiki nyingine unatakiwa ufanye mambo yafuatayo kama unataka kuipaki kwa muda mrefu;

[emoji117] drain mafuta yote kwenye tank pamoja na yale yanayobaki kwenye carburattor...maana petroli ina tabia ya kuganda na kuwa kama gundi nzito ikikaa muda mrefu hivyo kusababisha tank kuziba ama carburattor

[emoji117] Pili, disconnect battery na iweke sehemu ambayo ni well ventilated, kumbuka kuicharge kidogo pindi utakapotaka kuitumia

[emoji117] tatu, kama ni muda mrefu sana....fungua spark plug na uweke matone kadhaa ya oil kwenye tundu la plug ili oil iende kwenye combustion chamber kuzuia piston kustick

[emoji117] hakikisha umeiosha vzr na imekauka na iweke sehemu ambapo haitaweza kupata unyevu ili kuzuia kutu

Yangu ni hayo tuu wadau wengine wataongezea
 
kuna boxer 150 imeletwa hapa ofisini, haina hata kiezi sita muungurumo siku hizi utadhani sacania 113
matunzo tuu mkuu, shida inaanzaga kwenye kubadili oil & oil filter kwa wakati
 
Watu wengi wanaziogopa sana boxer lakn n bonge la boda ...sema inahitaj mtu anayejielewa. Spair pia og zmechangamka ninalo kama la mtoa post aseee mhindi hapa alicheza kama pele...hutataman kuendesha mchina yoyote ukiachana na speed,power boxer haina overheating na vibration za hovyo kama boda za mchna
ni kweli kabisa mkuu, spea OG ni bei ila ni genuine haswa na ukiweka ni mkataba
 
Oil unabadilisha kila baada ya km ngapi? vip kuhusu oil filtre unabadilisha kila unapobadilisha oil?
Miye ninayo boxer kama yako na ina miaka 2 lakini ilipofika km 20,000 ilianza kula oil sana now nimebadilisha piston ring imerudi kuwa normal
 
Oil huwa nabadilisha kulingana na mizunguko niliyoifanya...Mfano, nikifanya route ndefu ndefu nyingi huwa naibadili baada ya Km 1,000.

Ila kama ni route ndogo ndogo huwa nabadili km 1,200 mpaka km 1,500 kulingana na uchafu wa oil.

Kuhusu Oil filter, binafsi huwa nanunua ile OG ya mhindi mwenyewe na kama nikiiweka, round inayofata naiacha nakuja kuitoa round nyingine. Japo user manual inasema replace baada ya km 5,000
 
Back
Top Bottom