36% ya Waathirika wa VVU/ UKIMWI wanafariki kutokana na kuugua TB

36% ya Waathirika wa VVU/ UKIMWI wanafariki kutokana na kuugua TB

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
1679854846367.png
Kwa mwaka 2022 maambukizi ya ugonjwa huo yalifika wastani wa wagonjwa 208 katika kila watu 100,000 hukua 25,800 wakifariki.

“Asilimia 36 ya waathirika wa Virusi vya Ukimwi wanaopoteza maisha inasababishwa na ugonjwa wa Kifua Kikuu. Hii inathibitisha ugonjwa huu ni hatari na kikwazo cha maendeleo ya nchi,” alisema Majaliwa.

Mwaka 2021 wagonjwa 87,415 waligundulika na kuwekwa kwenye matibabu, lakini watu 44,585 sawa na asilimia 35 hawakubainika, hivyo kuendelea kuwaambukiza wengine.

Sambamba na hilo, Waziri Mkuu alizindua mpango mkakati wa kisekta wa kutokomeza Kifua Kikuu ambapo Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema unawapata zaidi watu wa kipato cha chini.

“Bado kuna jukumu kubwa la kuwatambua wagonjwa wa Kifua Kikuu ili waanze matibabu, ugonjwa huu unatibika endapo mtu atawahi kituo cha afya kwa wakati na dawa zake zipo,” alisema Waziri Ummy.

Katika kupambana na ugonjwa huo, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Amref Tanzania, Dk Florence Temu alisema wamewafikia zaidi ya wahudumu 2,500 wa ngazi ya jamii pamoja na waganga wa tiba asili 1,000 kupambana na ugonjwa huo.

“Mgonjwa mmoja anaweza kuambukiza watu 20, hivyo kuibua wagonjwa wengi pamoja na kuwasimamia matibabu ili waweze kupona,” alisema Dk Florence.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Kituo cha Kudhibiti Magonjwa (CDC) Tanzania, George Mgomela alisema kwa sasa changamoto kubwa ni usugu wa dawa za Kifua Kikuu.

Wakati ikiwa hivyo nchini, kwa Zanzibar pekee, takwimu zinaonyesha wastani wa watu 30 hufariki dunia kila mwaka kutokana na ugonjwa huo.

Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Kinga wa Wizara ya Afya Zanzibar, Dk Fatma Kabole alisema wagonjwa 1,077 wamegundulika kuambukizwa maradhi hayo mwaka 2022, wakipungua kutoka 1,090 wa mwaka 2021.

“Wastani wa watu 30 hufariki dunia kutokana na ugonjwa huu hapa Zanzibar kila mwaka na wagonjwa 15 walibainika kuwa na Kifua Kikuu sugu na kuanzishiwa matibabu ya daraja la pili mwaka 2022,” alisema Dk Fatma.
Burhana Khamis, mkazi wa Unguja alisema Serikali inapaswa kuongeza nguvu kuwabaini watu wengi walioambukizwa.
“Ukiangalia malengo waliyojiwekea kuwabaini wagonjwa 1,600 lakini wamebainika 1,090 hivyo bado kuna kazi kubwa ya kufanya,” alisema

Mpango wa kisekta
Mpango wa kupambana na Kifua Kikuu umeandaliwa kuweka hatua zitakazoishirikisha jamii, wafanyabiashara, Serikali na mashirika ya kiraia, ukilenga kutengeneza mbinu za kuwafikia watu walio katika mazingira magumu na kuwapa huduma.

Ofisa wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) anayeshughulikia Ukimwi, Kifua Kikuu na homa ya ini, Dk Johnson Lyimo alisema huwa wanaishauri Serikali ili mapambano yawe na mafanikio ni lazima yakabiliwe kisekta.

“Tunasema mapambano ya Kifua Kikuu tunataka kuyafanya kisekta kwa sababu ukiangalia vifo vinavyosababishwa nao utaona unawashambulia zaidi watu masikini na wenye matatizo ya lishe,” alisema Lyimo.

Alisema mpango huu uliidhinishwa mwaka 2017 katika mkutano wa mawaziri wa afya ulioitishwa na WHO baada ya kudhihirika kuwa katika mapambano ya Kifua Kikuu unahitajika mkakati wa kisekta.

Alisema mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 2018 uliazimia kila nchi izindue mpango huo.

Mwenyekiti wa Muunganiko wa Wadau wa Kutokomeza Kifua Kikuu Tanzania, Dk Peter Bujari alisema ili kuutokomeza wadau wanatakiwa kushirikiana.

Dk Bujari alisema malengo ya nchi ni kuhakikisha TB inatokomezwa ifikapo mwaka 2030.

“Sisi ndiyo waratibu wa mpango, kazi yetu ni kufuatilia vilivyoahidiwa kama vimefanyika na kuwapa uwezo wa kufanya. Wao wajibu wao ni kufanya, kwa hiyo tutafanya kazi kwa kushirikiana na Wizara ya Afya kuhakikisha tunawajengea uwezo wa kitaalamu pamoja na kutafuta rasilimali fedha ili kuziwezesha wizara kutekeleza wajibu wao katika kuutokomeza ugonjwa wa Kifua Kikuu,” alisema Dk Lyimo.

MWANANCHI
 
I have a story to tell kuhusu TB...... Mungu ni mwema nipo sawa sasa
 
Pole ndugu. Iseme hiyo story tupone
Mimi aiseh nilinusurika kupata ukimwi nikapata TB mkuu.

Nilikuwa na mrembo kwa muda mrefu na nikikutana nae kama mara 20 hivi... kumbe binti ni muathirika na anatumia dawa pia alikuwa na hiyo TB..

Sema Mungu ni mwema sana kwangu.. kuna kipindi nilikohoa kama siku 4 hivi alafu nikapona.

ghafla week hilo kabla halijaisha nikajikuta napata homa kali sana usiku yani kichwa kinapiga naishiwa nguvu na kukohoa sana..

Nikapoteza fahamu (hapo sijawahi poteza fahamu kabla)..

Nilikuja shtuka ninamadrip nikapelekwa chumba cha X-ray nikapigwa X-ray kwamara ya Kwanza

Basi majibu yakatoka nina TB na ninatakiwa kupima ukimwi na kipindi hiko nilikuwa na girl mmoja tu niliepanga muoa..

basi nikapima HIV Mungu mwema sana kwangu nikakutwa sina HIV so nikaanza dawa za TB japo mwanzo zinatesa sana na baada ya siku 9 nikawa poa kama kawaida ila nakumywa madawa ya TB makubwa hivi.


Nilivyopona kiasi miezi 3 toka nianze dawa binti akawa amerudi tena nikafanya nae tena...baada ya week mbili ndio hali ya TB ikarudi kama mwanzo appetite hamna, naumwa siwezi toka hata nje dawa zikawa zimenikataa yani nikimeza Hali inazidi kuwa mbaya.

Sema Ile hali ikanifanya nigutuke (maana nilipata maono binti anahiv) nikamface binti akakataa baada ya muda akajaga kusema yeye ana HIV ila anatumia dawa.

To cut the story short nilienda pima tena nikiwa natokea na machozi maana niliona dalili zote ninazo... Mungu akanipa nafasi nyingine nikakutwa negative tena...

Nikamaliza dawa za TB nikarudi kuwa sawa kama zamani.

Japo kuna shida ya ngozi watu wa TB huwa wanakumbana nayo
 
Back
Top Bottom