4 The Ladies,if your BF/Husband Slaps U Whats your Best Reaction?

Hapo sasa! Ila mateso ya huyu dada, kama ni msalaba wa ndoa, mmh, wa mwenzetu wa chuma cha pua.

Wamependana hao nyie mnaona anaumia wkt anampenda mmewe hata chakula cha night wanapeana kwa raha zao
 
mmh imezidi,sijui kama ningeweza kuvumilia.
 
nendeni mkaripoti TAMWA akifa hapo na nyie mnaojifanya kuona na kuuchuna wote mmehusika thtz too much
 
Dina mami hakuna mtu angependa kuwaacha watoto wake tena ikiwa ana fikra kwamba watalelewa na mama mwingine, hakuna mtu anaeweza kukulelea mwanao kama wewe mzazi uliemzaa utakavyoweza kumlea, hilo nalikubali kabisa, lakini inapobidi inabidi jamani, tena kwa uchungu mwingi, kwa mie ningeweza kabisa, kama huyo mdogo wa mwiho bado ananyonya ningeondoka nae nikagangamale nae mbele ya safari, wengine kwa ujacri mkubwa,kwa kujipa moyo ningewaacha nikatafute maisha.
 
Wamependana hao nyie mnaona anaumia wkt anampenda mmewe hata chakula cha night wanapeana kwa raha zao

Hili nalo neno baba, coz nilistuka nilipomuona mjamzito (mtoto wa mwisho ana kama miezi 10), nilishindwa kujizuia nikamuuliza, dada tena? Akabaki, bahati mbaya ndugu yangu...pale ndio nilipotafuta lizipu likuuubwaa, nikafunga mdomo!
 
mmh imezidi,sijui kama ningeweza kuvumilia.

c ndio hapo, mtu mpaka unajish2kia umeokoka bila kujua mana ya wokovu, unahic dunia imekutenga, yaani unapoteza uhalisia wa maisha yako kabisa, mie nilikuwa namuulizaga sis wangu kwani huweizi kuanza maisha mengine bila huyu mtu jamani, mana alikuwa anapigwa mpaka unamuonea huruma jibu analonipa ni kwamba mie nishukuru nimeolewa na mwanaume nilienae, yani unajiuliza huyu akili yake ipo wapi unashindwa kuelewa, na sis ana kazi yake nzuri, anajimudu kwenye familia lakini yupo radhi apigwe mpaka alazwe lakini anagangamala an ndoa, ndoa hizi....
 
Hili nalo neno baba, coz nilistuka nilipomuona mjamzito (mtoto wa mwisho ana kama miezi 10), nilishindwa kujizuia nikamuuliza, dada tena? Akabaki, bahati mbaya ndugu yangu...pale ndio nilipotafuta lizipu likuuubwaa, nikafunga mdomo!

Hahahahaha umeona sasa eheeeee..
Majirani mnaweza mkawa mnamwonea huruma huku mkimhurumia alafu akirudi Mr. anamwambia majirani wanasema hivi na vile wanatuonea wivu kesho na kesho kutwa mnaona watu wanafrahi pamoja huku waki cheer hizi ndoa jamani si za kuingilia na kuacha kama zilivyo mambo yanaenda na baadae yanajiset unakuta mwanamke anaendelea kupika na kupakua hata kama anabamizwa ukutani amechagua maisha hayo unafikiri kama angekuwa hampendi huyo mwanaume angevumilia kweli mateso yote hayo? Lazima angebeba watoto na kuanza mbele aidha kurudi kijijini bora akalime kuliko kuteseka hivyo yeye kwake anaona sawa tu safi miaka inakwenda na ataendelea kuzaa na kuzaaa maisha yanasonga.
 
Ulipo kuwa unamvisha pete ilikuwaje?
Na ukakubali pale mbele ya ndugu mtaishi kwa shida na raha

Nasubiri kwa hamu harusi yako wewe Fidel80 ..nitakuwa dereva wenu wa Bajaji ..
 
hapo ndo ujue tatizo la yeye kutoondoka si UWEZO japo huyu wa DINA anasingizia HANA PA KWENDA,wengine wanasingiziaga watoto bado ni wadogo wangekua na umri fulani ningeondoka.hata mie huwa sielewi lkn nahisi ni uwoga na kukosa ujasiri na kutojua thamani yako.
 
Hili nalo neno baba, coz nilistuka nilipomuona mjamzito (mtoto wa mwisho ana kama miezi 10), nilishindwa kujizuia nikamuuliza, dada tena? Akabaki, bahati mbaya ndugu yangu...pale ndio nilipotafuta lizipu likuuubwaa, nikafunga mdomo!

halafu cjui kwanini wengi wao huwa wanazaa sana, yani mpaka unajiuliza huyu ana matatizo hivi kila kukicha kuzaa ya nini jamani, wawili wangemtosha kabisa.
 
hehehehe umenifurahisha Fidel nimekosa ki-button cha Thanx
 
uwoga mwongine wa kijinga, na kuhofia jamii cjui itanifikiriaje ninapoanza kuishi mwenyewe, walimwengu watasema ndoa imenishinda, cjui nimeachika...khaa namuulizaga uliolewa na walimwengu au?...yaani hana sababu za binadamu mwenye akili timamu kumuelewa.
 
Me nicngeweza kisa cha kutoana roho

halafu kinachoniumaga zaidi ni kwamba kabla tanga halijaanuliwa ameshajua nani ata cover nafac yako, mtoto wa mwanamke mwenzangu haniui kwa kweli, nikaacha wanangu wanataabika.
 
nyamayao kula tano,hilo ndio hasaa linalotuua.mbaya zaidi ukiamua kuwa strong na kutoka ktk ndoa ya mateso wanawake wenzio ndio watakua wa kwanza kukupa label zote mbaya.wkt ilibidi tupeane moyo,ndo mana wengi wanaogopa kuondoka maana akiondoka inakua ajiandae tena kukabiliana na kejeli na dharau za jamii,so sad.
 
halafu kinachoniumaga zaidi ni kwamba kabla tanga halijaanuliwa ameshajua nani ata cover nafac yako, mtoto wa mwanamke mwenzangu haniui kwa kweli, nikaacha wanangu wanataabika.

huko ndo kugangamala.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…