Nina jirani yangu ambaye kwa kweli anasikitisha mno, yeye na mumewe wote ni Wakurya (wenyewe msiniue, hili hamuwezi kulipinga kamwe), I think kwao the slaps have advanced to another level. Mume anapiga mpaka nakosa mfananisho/ulinganisho. Mkewe alikuwa mjamzito, anamfungia mlango analala nje (I mean nje, sio upenuni mwa nyumba), na anapiga makelele mtaa wote tunasikia..nasema sikutaki, toka nyumbani kwangu! Na anawaambia wadogo zake (yeye mume), wahakikishe hawamruhusu kuingia ndani. Na yeye mke anasema anajua mumewe anafanya hivyo coz anajua kuwa hana pa kwenda (yeye mdada hana kazi, hana biashara). Ila ninachomsifu, ameanza kuweka mtaji wa shule (the QTs), akiwa na malengo kuwa atakapoweza hata kupata ajira ya kufanya usafi mahali, ndio atajua achukue uamuzi gani! Na ni mke ambaye ana watoto wa4 na huyo baba, anasema hawezi kuondoka coz hao watoto ni wadogo ana hofu na uangalizi wake (na ni wadogo haswa, wapo ambao hawajaanza hata chekechea).
Sasa hapa, pamoja na imani, lakini si utapekua bible mpaka?