unfortunately, amini usiamini, mafuta zenji hakuna. na kama yapo, yapo kidogo sana, na kama yakiwepo zenji basi na bara yapo. hata gesi tu hawajagundua. binafsi, ninaamini kama tunataka muungano, tuungane kabisa kabisa tuwe nchi moja, hata hoja ya kuwa na marais wawili kwenye nchi moja hii huwa naona ni ukakasi.
ila kama kweli kuna mafuta zanzibar, ni haki wayatumie wao tu, na sisi gas na mafuta na helium etc zitumike huku tu. Zanzibar kama wakipata mafuta kweli wataendelea sana, kama wakipata kitu cha kuwaingizia hela wataendelea sana kwasababu nchi yao ni ndogo kuiendeleza ni rahisi. hata hivyo.
wamejaa sana bara na ninapenda wajae zaidi ndio maana ya muungano, ila sisi sasa kwenda kwao tunaonekana wageni fulani hivi. tukija ndani ya hoja, ni kitu gani hiki kinachotakiwa kugawanywa? isije kuwa wana hoja ya msingi halafu inafunikwa.