4% ya mapato kwenda Zanzibar kama Hoja ya Muungano

Ha ha ha
 
Je si kuna mambo ya muungano ? Na ya upande kila mtu kivyake ? Mfano , TFF wapo FIFA kwa jina la Muungano (ndo maana Tanzania ina timu moja ya taifa ) ukiachia haya makombe yetu ya Afrika Mashariki n.k . TFF wanachukua mkwanja kutoka FIFA lakini sijui kama Zanzíbar wananusa !!! Hospitali , barbara n.k kila mtu kivyake (ikija hiyo haitokuwa ya Muungano, ila ikija ELIMU YA JUU, Polisi n.k itabidi naõ wawemo tu).
Hili mbona lipo zamani ila kila akaae analikwepa , sasa mama kasema litekelezwe wala huwo mgao wa 4% hakusema yeyé.... Waliletwa "wataalamu" wa kizungu ndo wakasema hilo.... Mgao wa faida na hasara pia.
 
Kodi yote inayokusanywa na TRA Zanzibar hubaki Zanzibar, hakuna senti inayovuka maji

Wakati huo huo wafanyakazi wa TRA Zanzibar ambao wote ni wazanzibar wanalipwa na TRA Taifa (ambayo mapato yake yanatokana na jasho la watanganyika)
Hapo ndio huwa nauchukia huu muungano, angalia wabunge kutoka zanzibar hivi wako Dodoma kwa kazi gani ? kutunga sheria ambazo hazitumiki zanzibar? kujadiri budget ambayo haitumiki zanzibar !! yaan naona wamekuja bara kuchuna tuu.
 
Umedadavua vizuri mkuu, je wabunge kutoka Zanzibar wanafanya nini Dodoma nisaidie tujue faida zao kwa bara.
 
Swali je muungano uvujwe? waweke hoja za msingi pasi kuficha ili watu waamue mana haiwezekana watu bara wakienda zanzibar wanaonekana kama foreigner tu
 
Huo ndio ukweli wenyewe fedha zote zinazokusanywa na TRA tawi la Zanzibar hubakizwa Zanzibar kama ulikua hujui anza kufuatilia sasa bunge la bajeti la mwaka wa fedha 2021/2022

Zanzibar ni kupe kwa Tanganyika

Vipi kuhusu mapato yanayotakana na kodi za makampuni? vipi kuhusu mapato yanayotokana na immigration ? vipi kuhusu mapato yanayotokana na Bahari? Anga?
 
Umedadavua vizuri mkuu, je wabunge kutoka Zanzibar wanafanya nini Dodoma nisaidie tujue faida zao kwa bara.

Hawana faida yoyote, na ndio moja ya kero za muungano. Lakini wanayoyasababisha hayo ni serekali ya Bara mana wao ndio wanaong'ang'ania serekali 2, Pakiwa na serekali 3 au ya mkataba hapatakua tena na tatizo kama hilo. Ila Serekali ya bara kwao ni bora kuendelea kuwalipa wabunge wa Zanzibar 50 kuliko kutatua kero zakweli ambazo kwao wanahisi zitawagharimu.
 
Hawa watu hata umeme wa kutoka bara hawaulipii na hawana mchango wowote wa kustahili hiyo asilimia,si wanajifanya wana mafuta na mafuta sio suala la muungano sasa wameona mama ametoka kwahiyo wanamtega, hawa ni waroho na walafi wanapenda sana kujiangalia wao,sisi tukihamia kwao wanakuwa wa kwanza kulalamika ujinga mara oh wao wana ardhi kidogo wakati wao wamejazana huku bara,hawana tofauti na mtoto aliyedekezwa sasa akinyimwa hata peremende basi hulia na kugalalagala chini ili tu apate attention kutoka kwa wazazi wake. Na wamesema kwa miaka 30 hilo suala halijapatiwa ufunguzi ,kwa hiyo leo ndio wameona ni muda wa kupata ufumbuzi ,tatizo hao wanaobweka tayari wanajiona chama cha zambarau kina madaraka huko Zenj.
 
Nisaidieni TRA inakusanya mapato hadi Zenji? Na yanarudije? Au mapato Zenji ubaki huko huko, kama sivyo serikali ya mapinduzi Zanzibar inaendeshwa na vyanzo vipi?
 
Inasadikika kwamba tunatumia kiti cha Zenj pale UN, moja ya faida ni kupata fursa ya kuomba misada na mikopo kutoka nchi waisani na mashilika ya kimataifa. Zenj inapoteza fursa ya kuingia ktk makubaliano km hayo kimataifa.
Kwa kuzngatia ukubwa kijiografia na idadi ya watu ikakubalika Zenj iwe inapatiwa 4% Tu. Ila cc c wajanja, ata iyo 4 atuwapatii.
Pia inasemekana zenj ilichangia $ nyingi sn BOT yaani km inapigwa maesabu wanatudai ela ndefu mnooo.
Ni ktk mambo ambayo wazenj awaoni faida ya Muungano.
Sorry nmetumia vyanzo visio rasmi
Nadhani Ndo mana Mh Rais aliwaagiza wausika wa fedha kulishulikia jambo ili coz watakua na kumbukumbu rasmi juu ya makubaliano hayo
 
Msaada sawa kama haujalenga eneo maalumu. Mkopo si unachukuliwa kufanya kitu husika. Mkopo wa kujenga stigilazi ZNZ wa gawiwe wa nini? Hili la mkopo wasaidiwe kwa kudhaminiwa kama watakuwa na mkakati wa kuulipa.
Na huu ndio ujinga tunaouzungumzia kila siku. Eti halafu na wewe ni msomi.

Zanzibar ni MSHIRIKA na wala sio ombaomba. Eti wasaidiwe, Tanganyika yenyewe ina madeni kede wa kede ina uwezo gani wa kuisaidia Zanzibar.

Kama huna ujualo kuhusu Muungano uliza wajuvi
 
Wanaitwa wanga ukitaka kuwa mkweli. Lakini roho mbaya ni hao waliosema mafuta yetu haya wahusu Watanganyika hapa napo kama utataka kuwa mkweli wa nafsi yako na kuukataa unafiki kama dhambi.
Haya mambo yapo kwenye makubaliano ya mambo ya Muungano.

Na yarudiwe yaangaliwe. Rasilimali hazipo kwenye mambo ya Muungano
 
Msaada ambao ni general kwa Tanzania ni sawa. Kwa mfano msaada wa vyandarau kwa Tanzania wa chukue 4% yao. Lakini msaada kwa Serikali ya JM Tanzania kwa ajili ya Hospital ya Mnazi mmoja ZNZ utapiga 96% ya huo msaada ije Tanganyika?
Sasa mkuu hakuna huo msaa wa JM Tanzania kwa ajili ya hospital ya Mnazi mmoja.

Ukija msaada kwa ajili ya MMH ujue huo umetolewa specifically kwa ajili ya znz. Na hii ni kutokana kwamba znz inayo serikali na ukiwa na serikali maana yake unatambulika. Zanzibar ina balozi za nchi nyengine hapa tofauti na Tanganyika ambao wao wanajifanya ndio Tanzania
 
Yaani hili koloni letu linatunyonya sana sioni umuhimu wa sisi kuwapa hio 4%


Wanatulalamikia bure tu yaani ni sawa unaishi na mke mwenye gubu unamuhudumia unamlipa bado ana lawama


Na niwaambie ukweli sio nyinyi tu hamtupend hata sisi hatuwapendi vile vile lakini kwakuwa tumewa dominate ktk kila kitu hilo linatupa faraja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…