4% ya mapato kwenda Zanzibar kama Hoja ya Muungano

Walioweka hesabu kwa vigezo hivi walikuwa realistic? Ugawiwe hata kama huchangii inawezekana wapi? Gharama za Majeshi ya Muungano tu pamoja ya kuwa ni siri kuu, sidhani kama ZNZ inaweza kuzihimili wenyewe. Na mimi nimetoa tu eneo moja kama mfano.
Ndio maana tukasema uvunjwe. Hatuutaki
 
Na katika mada kama hizi ndio kuna watu ulidhani huko nyuma wana akili, hapa ndio unawajua ni wajinga na wapumbavu tu. Hawajui mambo kadhaa muhimu ya taifa lao
 
Hii hoja yako namba 2 imenifanya nione upeo wako wa kujua mambo ni mdogo. Nenda angalia nchi zenye population ya chini ya 1M hawana mashirika ya simu???
 

Mngelilia urithi kwenye matanga na kuita watu wanga?
 
Kama Kuna kitu nyerere alibugi ni kukubali kuunganisha hizi nchi mbili, na huu muungano sisi watu wa bara ndiyo tunaulazimisha kwa hiyo lazima tuweke vitu vya kuwavutia, tunapoacha kutekeleza ndiyo tunakumbushwa
 

Tukiwa na viongozi wenye akili kama zako jua Muungano unaenda kufa. Jua hilo.
 
Amini usiamini lazima Kuna hoja ya msingi hawawezi kukurupuka Hawa watu,Kuna kitu tu ambacho kina maslahi kwao Ila hakitekelezwi
 
Tukiwa na viongozi wenye akili kama zako jua Muungano unaenda kufa. Jua hilo.
Ndio,

Either ufe au uwe muungano wa kuheshimiana kwa pande zote mbili. Kila upande upate haki yake.

Sitokubali Tanganyika inyonywe na kuonewa au Zanzibar inyonywe na kuonewa. Nimefunzwa kusimamia haki hata kama baadhi ya watu hawaipendi.
 
Haki ya kunyonya wengine?
Kuwanyonya vipi??

Haya mambo yapo kwenye mkataba.

Suala la Bakia ya pato la Taifa kwenye mambo ya muungano, suala la misaada yote inayokuja Tanzania Zanzibar inatakiwa ipate share yake.

Tena baadhi yenu mnajitia wazimu kwamba ni 4%. Tambueni ni 4.5%

Miaka ya MEMKWA mlikwenda kuombea misaada jina la Tanzania halafu mkakataa kutoa share ya Zanzibar kwa kisingizio eti elimu ya Msingi sio jambo la Muungano.

Pumbavu kabisa!!!

Sasa si mngeenda kusema Tanganyika ndio inaomba msaada
 
Ndio,

Either ufe au uwe muungano wa kuheshimiana kwa pande zote mbili. Kila upande upate haki yake.

Sitokubali Tanganyika inyonywe na kuonewa au Zanzibar inyonywe na kuonewa. Nimefunzwa kusimamia haki hata kama baadhi ya watu hawaipendi.

Tanganyika inyonye Znz kwa kusaidia kulipia watu wake umeme?!
 
Easier said
 

Mngekua mnalitaka, kuliheshimu na kulithamini hili jina la Tanzania mngebakia na jina lenu la Zanzibar? Ila kwenye shekeli mnalithamini na kuliheshimu. Tuondoleini unafiki huu tena ni dhambi mbele ya Mungu.
 
Tanganyika inyonye Znz kwa kusaidia kulipia watu wake umeme?!
Mkuu,

You are either missing the points intentionally or arguing just for the sake of arguing.

Don't have time for that!

Maana naona tunajadiliana vizuri tu nakueleza mambo yalivyo halafu bado unajitia hamnazo vile vile
 
Mkuu,

You are either missing the points intentionally or arguing just for the sake of arguing.

Don't have time for that!

Maana naona tunajadiliana vizuri tu nakueleza mambo yalivyo halafu bado unajitia hamnazo vile vile

Ukiheshimu utaheshimiwa. Tabia mlizorithi kutoka kwa mabwana zenu waarabu za kudharau, kudhalilisha na kutweza utu wa mtu pale walipowafanya mababu zetu kuwa bidhaa na kuwauza kama mifugo hazina nafasi dunia ya leo.
 
Ukitathimi kwa kina utagundua iyo 4% inatoka Tanganyika kwenda Zanzibar.

Ni kama vile Tanganyika inalipia gharama za muungano.
Ni kweli ulichokiandika.
Kwa muundo huu wa muungano, Zanzibar ni koloni la Tanganyika, hivyo Tanganyika inawajibika kulipia gharama ya kulitunza koloni lake.

Upande wa pili utajiuliza ni kwa vipi Tanganyika inapata faida kwa kuikalia kimabavu Zanzibar? Jibu nitakupa hapa.
1. Sababu za kiusalama. Tanganyika haiwezi kuwa salama ikiwa Zanzibar itakuwa nchi huru. Watu wenye akili wameshanielewa........

2. Uchumi wa Tanganyika kibiashara unategemea sana bandari ya Dar na makusanyo ya kodi kwa bidhaa kutoka nje. Zanzibar ikiwa nchi huru, itakuwa na mamlaka ya kuwa na bandari huru kubwa, ushirika na Oman, China au nchi za mabeberu katika uwekezaji wa kibiashara kama kisiwa huru (mfano wa Dubai) na hapo itaua bandari ya Dar na makusanyo ya kodi kwa bidhaa za nje kwa Tanganyika.

Hizi blah blah za kutaka kujenga bandari Bagamoyo zitahamia ghafla Zanzibar siku chache tu baada ya Zanzibar kuja kuwa nchi huru.
 
mishahara gani munayowalipa mkuu?

Na je vipi kuhusu mapato ya anga? mapato ya bahari? Kodi za makampuni? Visa fees? zote ziende Bara au ?
Sioni faida yoyote watanganyika wanapata kwa kuendelea kuikumbatia Zanzibar wala sioni hasara endapo muungano ukivunjika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…