4% ya mapato kwenda Zanzibar kama Hoja ya Muungano

Sio hawajui tu Bali hata uwezo wa kujua hawana.
 

Hiyo sababu namba 1 ilikuwa enzi hizo za cold war si dunia ya leo mtu yuko pentagoni na laptop na kikombe cha capocino anakuletea kombora ukiwa chooni kwako.

Hata Uganda ilikuwa tishio la amani kwa Tanzania kumbuka walifanyiwa nini? Hadi leo tunalipwa fadhila ya bomba la mafuta.
 
Wanaibiana wenyewe kwa wenyewe mkuu.

Wamezoea wizi
 
Huu muungano sisi watanganyika ndo tunaonekana kutawaliwa
 
Wala hawajisahau. Wanajifanya wehu tu
 
Kwahiyo na hili deni letu la taifa la 71tr wao pia wanachangia asilimia ngapi?..au tunagawana nusu kwa nusu.[emoji28][emoji28]
Wazanzibari watakuwa na wajibu wa kuchangia if and only if hilo deni limegharamia mambo ya muungano.
 
Acha uongo, tra ukusanye mapato znz alaf yote yaachwe znz basi itakua tra yenu ya kikundi cha majambazi
Mwambie simtajii siku, lakini siku hiyo ikifika ndani ya kila mwezi, mzigo wa hela unakuwa na Escort unasafirishwa kutoka Zanzibar kupelekwa Airport na kupelekwa Benki Kuu.
 
Naona wengi hawaelewi huu Muungano ulivyo. Muungano si kila kitu cha Serikali kiko kwenye Muungano bali ni makubaliano ya baadhi ya mambo. Kwa uelewa tuyataje hayo mambo hapa
 
TAtizo linakuja wengi hawaelewi kabisa uhalisia wa mambo. wanakwenda kimihemko tu
Yes ila kuna baadhi wanaelewa. Kuna mambo ya muungano na ambayo si ya muungano na kuna kitu kinaitwa akaunti ya pamoja ya fedha ambapo ndio kunatakiwa kuwekwa mapato ya muungano na baada ya matumizi bakaa ndio inapaswa kugawanywa kwa 4.5% kwa visiwani na 95.5% bara
 
Hii akaunti bado haijaanzishwa na ndio vice alipewa agizo la kwenda kuanzisha. Inabidi tuyaelewe haya mambo kabla ya kuwa na jazba na kukashifiana. Haya mambo yalipaswa kufundishwa kwenye somo au topiki ya uraia
 
Mkuu wewe ni mtu umejijengea heshima humu jukwaani, si vizuri kuiharibu mwenyewe. Usiendeshwe na ushabiki.

Angalia heshima aliyojijengea Pascal Mayalla na halafu akaiharibu.

1. Rais Mama Samia sio jukumu lake kueleza mchango wa Zanzibar kwenye Muungano ila ni jukumu lake kuhakikisha kila jamii inapata haki yake inayostahili.

2. Rais Mama Samia anajua kwamba wabunge wote wa Zanzibar waliopo bungeni ni Wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo Zanzibar ni Mshirika. Ikisha kuwa tu jambo linalohusu jina Tanzania basi watanganyika wajue kwamba humo kuna haki za Wazanzibari na wala Wazanzibari hawafanyiwi ihsani. Hili ni muhimu lijulikane wala msijitie hamnazo.

3. Si kazi ya Rais Mama Samia Suluhu Hassan kuweka wazi kipi cha muungano na kipi si cha muungano, mkataba upo na Serikali ya Muungano haijataka kuuweka wazi, anachokisimamia mama Samia ni kuhakikisha mkataba unatekelezwa.

4. Rais Mama Samia Suluhu Hassan anajua kwamba yeye ni Rais na Amir jeshi mkuu wa JMT na anapotenda anatenda kwa kuzingatia hilo. Nongwa imekuja tu baada ya yeye kuagiza hili suala lishughulikiwe????

Rais Mama Samia Suluhu Hassan amekuja kutekeleza hoja na kutenda haki kwa Watanzania. Hatosumbuliwa na chochote na hao Watanganyika hawatosema enough is enough kamwe kwa sababu wamekuwa wakiinyonya Zanzibar for years. Besides there is nothing bad for Tanganyikans to say so when it comes about the union.

Ni imani yetu Rais wetu kipenzi Mama yetu Samia Suluhu Hassan atarudisha mchakato wa katiba mpya kwa maslahi ya Tanzania kwa ujumla ili kila upande washirika wa Muungano wapate wanachostahili. Angalizo: Watanganyika kamwe hajawahi kuidai Tanganyika yao kwahiyo hakuna suala la "tutaendelea kuidai"

Once again, umejijengea heshima hapa jukwaani kwahiyo ni bora kuilinda.
 
Umedadavua vizuri mkuu, je wabunge kutoka Zanzibar wanafanya nini Dodoma nisaidie tujue faida zao kwa bara.
Wabunge kutoka Zanzibar wapo pale kujadili mambo yote ya kibunge yanayohusu Muungano.
Wapo kwa ajili ya kuwawakilisha Wazanzibari kwenye Muungano
 
1. Rais Mama Samia sio jukumu lake kueleza mchango wa Zanzibar kwenye Muungano ila ni jukumu lake kuhakikisha kila jamii inapata haki yake inayostahili.
Hapana si kweli! kama tutakubaliana nawe basi useme kuwa ni wajibu wake kusimamia uwajibikaji wa pande zote mbili katika muungano. Haiwezekani kusimamia haki ya mapato bila kusimamia haki ya mchango na madeni.
Hapa ndipo penye tatizo, kwamba, muungano si kapu la kutoa! ni kapu la kuweka pia
Hao wabunge wanakuja Dodoma kwa gharama za SMZ au za JMT ambayo ni Tanganyika? Hapa uelewe muungano ni kuwajibika si jina. Huwezi kuongelea haki bila kuongelea haki ya kuchangia na haki ya kulipa madeni.
Wazanzibar wanafanyiwa hisani kwasababu pale Bungeni wanajadili TAMISEMI , Wizara ya Afya, Elimu, Mifugo, maji na mawasiliano kwa sababu gani. Ni hisani kwasababu mchango wa Zanzibar upo wapi ukiachilia jina?
3. Si kazi ya Rais Mama Samia Suluhu Hassan kuweka wazi kipi cha muungano na kipi si cha muungano, mkataba upo na Serikali ya Muungano haijataka kuuweka wazi, anachokisimamia mama Samia ni kuhakikisha mkataba unatekelezwa.
Mkataba upi ambao umesema haujawekwa wazi?
4. Rais Mama Samia Suluhu Hassan anajua kwamba yeye ni Rais na Amir jeshi mkuu wa JMT na anapotenda anatenda kwa kuzingatia hilo. Nongwa imekuja tu baada ya yeye kuagiza hili suala lishughulikiwe????
Hapana! suala la muungano ni la kitaasisi na lishughulikiwe kitaasisi. Suala la muungano si kero za Wazanzibar ni matatizo yanayohusu Tanganyika pia ndani ya muungano hasa kubeba gharama peke yake
Rais Mama Samia Suluhu Hassan amekuja kutekeleza hoja na kutenda haki kwa Watanzania.
Tunamuombea kwa mwenyezi mung amfanyie wepesi na kumuonyesha njia
Hatosumbuliwa na chochote na hao Watanganyika hawatosema enough is enough kamwe kwa sababu wamekuwa wakiinyonya Zanzibar for years. Besides there is nothing bad for Tanganyikans to say so when it comes about the union.
Sijui una maana gani maana kwangu mimi kiingereza kinanisumbua kidogo
Ni imani yetu Rais wetu kipenzi Mama yetu Samia Suluhu Hassan atarudisha mchakato wa katiba mpya kwa maslahi ya Tanzania kwa ujumla ili kila upande washirika wa Muungano wapate wanachostahili.
Hasa na kila mshirika abebe majukumu yake na ya muungano. Ushirika uwe wa kubebana si kubebwa
Angalizo: Watanganyika kamwe hajawahi kuidai Tanganyika yao kwahiyo hakuna suala la "tutaendelea kuidai"
OK! unakumbuka G55
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…