Kuna tatizo kwa Rais Samia
Inaonekana kwa kauli zake ni kama alikuwa na ''chuki' fulani na sasa anataka kutekeleza hoja za Wazanzibar na si kero za pande zote za muungano. Hili litamkwamisha sana kwasababu Watanganyika watakapochachamaa itakuwa tabu
1. Kama anataka pesa za 4% na nyingine , Rais Samia pia aeleze Mchango wa Zanzibar ni upi katika muungano?
2. Rais pia aimbie SMZ igharamie wazanzibar pale Bungeni na Wizara na taasisi za muungano kwasababu wanapata mgao wao.
3. Rais aweke wazi kipi cha muungano kipi sicho ili Watananyika nao wawe na fursa zao bila kuingiliwa
Rais Samia atambue ni Rais wa JMT si Mwakilishi wa Wazanzibar na kwamba Zanzibar wana Rais, nani atawaongelea Watanganyika?
Nimefuatilia kauli za Rais Samia ni kama vile amekuja kutekeleza hoja za Wazanzibar, hili litamsumbua sana hasa Watanganyika watakaposema 'enough is enough'. Yeye si Rais wa Zanzibar ni Rais kutoka Zanzibar
Rais Samia ana fursa ya kurudi katika Rasimu ya Warioba ili mambo ya muungano yawe wazi na Zanzibar ipate inachotaka. Tutaendelea kuidai Tanganyika ili nasi tuwe na nafasi ya kuamua masuala yetu
Kuna tatizo na Rais ashauriwe kwa kauli zinazoelekea kule kule tulipotoka '' Ni zamu yetu''
JokaKuu Mag3