4% ya mapato kwenda Zanzibar kama Hoja ya Muungano

Usichokifahamu ni kwamba TRA wanakusanya kodi hadi Zanzibar. Ndio maana sheria inataka 4% ya mapato yote Tanzania iende Zanzibar. Tena hio 4% kwa maoni yangu ni ndongo ingepaswa walau 15%.
 
TRA ni yabara so kama inakusanya kodi mpaka Zanzibar basi wanahaki ya kupewewa zaidi ya 4%, pia kama Tanganyika inakusudia kuenzi Muungano basi misaada inapoletwa Tanzania inamaana zanzibar watakua na % yao kwa sababu misaada inapokuja haiji kwa jina la Tanganyika but inakuja kwa jina la Tanzania ambayo ni Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
 
Kwasababu kulikua na viongozi rohombaya ambao walikua wanaenda kinyume na makubaliano ya Muungano

Wanaitwa wanga ukitaka kuwa mkweli. Lakini roho mbaya ni hao waliosema mafuta yetu haya wahusu Watanganyika hapa napo kama utataka kuwa mkweli wa nafsi yako na kuukataa unafiki kama dhambi.
 

Msaada ambao ni general kwa Tanzania ni sawa. Kwa mfano msaada wa vyandarau kwa Tanzania wa chukue 4% yao. Lakini msaada kwa Serikali ya JM Tanzania kwa ajili ya Hospital ya Mnazi mmoja ZNZ utapiga 96% ya huo msaada ije Tanganyika?
 

Zanzibar haichangii chochote, yeye mwenyewe Samia mshahara wake na marupurupu yote ni jasho la watanganyika

TRA ipo zanzibar lakini inakusanya mapato kwenye maeneo chache sana, na kisha mapato yote huachwa Zanzibar (hakuna shilingi inayokusanywa Zanzibar huvuka maji)
 
Hata ikitokea maisha ndivyo yalivyo wewe umepata jana yule anapata leo. Kwani si jamhuri ya muungano mkuu
 
Ninavyoelewa ni 4% ya misaada na mikopo kutoka nje in atakuwa kwenda SMZ.
Asilimia 4 ni kubwa sana kwa Zanzibar

Ratio ya wakazi wa Zanzibar kwa total population ya watu milioni 59 ni chini ya hiyo asilimia nne

Pia Ratio ya gdp ya Zanzibar kwa gdp ya nchi nzima nayo ni chini ya hiyo asilimia 4

Na hata ki-jographia eneo la Zanzibar ki uwiano ni dogo chini ya hiyo asilimia 4
 
Zanzibar wanapenda kutumbua tu, kwenye kugharamika hupiga chenga

Hawajawahi changia chochote kwenye kulipa deni la taifa
Basi hapo kuwapa 4% ya mapato tu itakuwa ni uonevu wa hali ya juu kwa upande wa pili wa Muungano.
 
Usichokifahamu ni kwamba TRA wanakusanya kodi hadi Zanzibar. Ndio maana sheria inataka 4% ya mapato yote Tanzania iende Zanzibar. Tena hio 4% kwa maoni yangu ni ndongo ingepaswa walau 15%.
Kodi yote inayokusanywa na TRA Zanzibar hubaki Zanzibar, hakuna senti inayovuka maji

Wakati huo huo wafanyakazi wa TRA Zanzibar ambao wote ni wazanzibar wanalipwa na TRA Taifa (ambayo mapato yake yanatokana na jasho la watanganyika)
 
Msaada ambao ni general kwa Tanzania ni sawa. Kwa mfano msaada wa vyandarau kwa Tanzania wa chukue 4% yao. Lakini msaada kwa Serikali ya JM Tanzania kwa ajili ya Hospital ya Mnazi mmoja ZNZ utapiga 96% ya huo msaada ije Tanganyika?
Iwe msaada ama mkopo Zanzibar haipaswi kupata asilimia 4

Asilimia 4 kwa Zanzibar ni nyingi kwa hoja kuu mbili:

Moja: asilimia ya pato la Zanzibar katika pato jumla la nchi nzima ni chini ya hiyo 4

Mbili: asilimia ya wakazi wa Zanzibar katika total population ya milioni 59 ni chini ya hiyo 4
 

Basi kikotozi kitumie vigezo hivi ulivovitaja. Pato la serikali na population.

Hili la mgao wa 4% ya ZNZ , Sheria ya makao makuu Dodoma na kusema kuhusu mapungufu ya uongozi wa mwendazake haya kuhitaji kusubiria angalau tumalize arobaini. Yote ni heri lakini.
 
kwani Zanzibar ni NCHI?.
Zanzibar HAINA tofauti na morogoro au singida au dodoma n.k
fedha zinazoenda kwenye miradi ya maendeleo ya mikoa ziende pia Zanzibar.
Ukitathimi kwa kina utagundua iyo 4% inatoka Tanganyika kwenda Zanzibar.

Ni kama vile Tanganyika inalipia gharama za muungano.
 
Na ndo maana wazanzibar wanataka NCHI YAO.
KWANINI MSIWAPE KUEPUKA HAYA MAMBO.?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…