chapwa24 Sheria inaitaka serekali ya muungano iipatie Zanzibar 4.5% ya misaada yote pamoja na Bakia la Pato la Muungano.
Swali la kwanza ni kua Bakia la pato la Muungano ni lipi? Pato la muungano ni yale mapato yote yanayokusanywa na jamhuri katika mambo ambayo yamo ndani ya muungano kisheria.
Inavyotakiwa ni kuwa baada ya mapato yote kukusanywa, fedha inatakiwa itumike kwenye Budget ya mambo ya muungano, fedha yote itakayobakia inatakiwa igawanywe kwa washirika wa muungano. Kwahiyo Zanzibar wanatakiwa wapate 4.5% na Bara wapate 95.5%
Mfano: kama mapato ya mwaka ya source zote za Muungano ni milioni 120. Halafu Matumizi ya muasuala ya Muungano kuanzia mishahara pamoja na miradi mambo mengine ni milioni 20. Kwahiyo itabakia milion 100, Sasa hiyo mia itatakiwa igaiwe Zanzibar wachukue milioni 4.5 na Bara wachukue milion 95.5. Sasa tatizo lnakuja kuwa Bara hawajawahi kuwalipa Zanzibar stahiki yao ya mgao wa mapato kwa miaka yote hiyo. Pesa zote wanachukua wao, na ndio mana Zanzibar wanalalamika na ndio moja katika kero kubwa za muungano.
Swali jengine linalokujia wewe ni, Kwanini Zanzibar wapewe mgao wa fedha wakati wewe huuoni mchango wao kwenye hayo mapato?
Mtu yoyote anaetaka kuja Tanzania anlipia visa, Pesa ya visa direct inaingia kwenye mfuko wa Muungano. Zanzibar kwa mwaka kunakwenda watalii wasiopungua laki 3, hawa malipo ya visa zao zote zinachukuliwa na Bara, Zanzibar haifidika na hela visa ya watalii wanaokwenda kwao.
Ma company yote ta TZ, kuanzia ya mitandao ya simu, ving'amuzi, Mabenk na mengineyo, Yanasajiliwa Bara, lakini yanafika mpaka Zanzibar kutoa huduma bila kulipa kodi yoyote kule Zanzibar. Yani ni hivi Voda wanalipa Kodi Bara lakini wanatoa huduma mpaka Zanzibar. Fedha wanazolipia za kodi ni kwa ajili ya kutoa huduma mpaka Zanzibar, ila sasa TRA hawagawi mgao wa fedha zinazotokana na makampuni kwa Zanzibar.
Hiyo ni mifano miwili na ipo mengi tu kwenye kila sekta inayohusu Muungano.
Kwa kifupi wanachokifanya Serekali ya SMT, ni wizi wa mchana kabisa, Kila mwaka wanawaibia Zanzibar karibu 1 trillion. kwa kipindi cha miaka kumi kiharaka haraka Zanzibar wanaidai Tanzania fedha isiyopungua Trillion 10.