40 ya Membe yamvuruga Waziri Nape Nauye

Desprospero

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2023
Posts
1,015
Reaction score
2,493
KWELI siasa ni mchezo wa ajabu. Tarehe 27/8/2023 kutafanyika maadhimisho ya kifo Cha utata wa Bernard Membe kijijini kwake Rondo-Chiponda mkoani Lindi.

Waandalizi wa tukio hilo kutoka Dar es salaam wameamua kufanya hilo tukio la kishindo ambapo watu wapatao 1290 wanategemewa kuelekea Lindi tarehe 25/8/2023.

Aidha, imeelezwa kwamba Mawaziri wapatao 14 wamethibitisha kuhudhuria tukio hilo. Taarifa za uhakika zinaeleza kwamba Waziri Nape Nnauye ameudhika na tukio hilo kufuatia Wazee wa kabila la Wamwera kutumia tukio hilo kumsimika mdogo wa marehemu Membe, Stephone Kamilius Membe kuwa Chifu wa Mtama na hatimaye Mbunge wa Jimbo hilo 2025.

Tayari makampuni ya usafirishaji wanapishana nyumbani kwa Membe kutaka tenda hiyo ya usafirishaji wa watu kutoka Dar es salaam kwenda Lindi huku akitajwa Mwandishi nguli Bollen Ngetti kuratibu tukio hilo. Inaelezwa hili ni pigo kwa Nape Nnauye anayetetewa na kupiganiwa na Mh Hawa Ghasia. Kumekucha!
 
Maskini Nape! Ulimi umekuponza
 
Wacha kupambazuke mtu huwezi kuvaa nepi hadi utu uzima ni wakati sasa wana Mtama mvue nepi mvae kaptura au suruali
 
Hii ni kuhusu mademu arobaini aliowakanyaga? 🤔
 

 
Kazi ipoo hapoo Nepi atafuraaa sanaa muda ni mwalim mzuri sanaaa
 
Nape ana vinasaba vya usaliti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…