youngkato
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 3,811
- 3,888
25. Re-create yourself (Rebrand, ongeza huduma.)
Kufanya rebranding ni kitu kampuni kubwa nyingi duniani zinafanya mara kwa mara. Rebranding inakusaidia kuonekana mpya, na kuzuia mazoea kwa wateja.Pia rebranding inakuaidia kubadirika na kuendana na mazingira ya technologia.
26. Keep your hands clean
Hakikisha unaweka band yako chafu, Ilinde isichafuliwe na wateja. Ikitokea imechafuka sana tumia sharia ya 25 (Rebrand). Mteja mmoja anaweza kuchafua au kuua kabisa biashara yako. Jifunze kukwepa negative clients wasikuharibie brand yako.27. Play on people’s need to believe to create a cult like following (Wapatie watu imani na ndoto)
Wafanyabiashara wanaita hii copywriting, kuna hatua unatakiwa kutumia mbinu nyingi sana ili wateja wakuamini. Mfano onesha shuhuda nyingi sana za wateja, tumia sana copy.Kuna saikolojia za wateja ambazo unatakiwa kuzielewa ili uweze kushawishi watu wakuamini. Tumia mbinu nyingi za kivita, ili kuwapata wateja.
28. Fanya kila jambo kwa ujasiri
Biashara inahitaji ujasiri sana (Half-heartedness leads to failure). Kuna rafiki yangu ananiambiaga usimuonee huruma mteja hata siku moja.Biashara inahitaji ujasiri sana; hutakiwi kuleta mazoea na wateja.
29. Plan all the way to the end
Usianze bila kuona mwisho utakuwaje. Kabla hujaanza biashara yoyote, hakikisha unafanya analysis kujua watu wanataka nini.Njia pekee ya kuuza ni (Content, ads, na outreach) lakini kama unachokiuza hakihitajiki na watu, basi unapoteza tu muda wako na pesa zako.
30. Fanya mafanikio yaonekane kuwa ni rahisi
Ukinfata tajiri yeyote au mfanyabiashara aliyefanikiwa atakwambia nilifanya kazi kwa bidii, hakuna atakayekwambia nilipambana kwa kuanza hivi au niliiba nikapata mtaji.Unaambiwa hii inawafanya watu wasijue mbinu zako za kupata mafanikio.
31. Control the options — get others to play with the cards you deal
Kucheza na akili za wateja, huwa tunatumia mfumo wa package kutengeneza offer zako.Control options maana yake, nimsaidie mteja kufanya maamuzi bila yeye kujua.
Katika kumfanya mteja afanye maamuzi huwa tunatumia njia tofauti kumshawishi mteja ili anunue bila yeye kujua au aone bidhaa zetu ni za bei ndogo sana.
32. Ongea na ndoto za watu. (Uza ndoto)
Wateja wanapenda matumaini, kwamwe mteja wako usimuoneshe ugumu wa nachoenda kukipitia.Mfano unauza kozi ya kusaidia wafanyabiashara kurusha matangazo, usiwaambie ugumu wa kusoma hiyo kozi, ila waambie faida watakazozipata baada ya kusoma hiyo kozi. (promise the moon, the great and sudden transformation, the pot of gold).
33. Gundua udhaifu wa kila mteja
Ukishajua udhaifu wa mteja wako ni rahisi kumuuzia. Unakuwa unagusa kwenye point tu.Ukishajua weakness ya mteja wako ni rahisi sana kumuuzia.
34. Wateja watakuheshimu kama unavyojithamini.
Ukiuza bidhaa zako kwa bei ndogo utapata wateja wa bei ndogo sana, ukiuza bidhaa za bei kubwa, utapata wateja wa bei kubwa,Utapata wateja kulingana na jinsi ulivyojiweka standard za biashara zako.
35. Jifunze kuchagua muda sahihi (Launch when the market is ready — not when you are)
Lazima ujue muda sahihi wa kuingia sokoni, kuingiza bidhaa sokoni. Mara nyingi tunasema tunaenda na trend,Mfano kuna muda wa kupost content, kuna muda wa kurusha tangazo, kuna muda wa kupost status.
Pia na kila bidhaa inaenda na msimu wake. Kuna msimu wa mavuno, msumu wa shule, msimu wa pesa kuingia mtaani.
36. Ignore haters, copycats, and noise.
Washindani wako, competitors wako, kelele za watu wengine zisikutoe kwemye mstari.Kelele ni nyingi kila mtu anapambana kuwa juu yako, watu wengi watacopy unachokifanya kwahiyo hakikisha hizo kelele hazikutoi kwenye mstari.
37. Itaendelea
Tumefanya biashara nyingi kukua kwa kutumia hizi sheria 48 za kukuza biashara yako tutakusaidia kufanya hivyo kwa kukuletea wateja, kuktangazia na kufanya branding kwenye biashara yako pamoja na kukufundisha mbinu za kuongeza wateja kwa kutumia hizi sheria 48. Tutafute whatsapp wa.me/+255693880325