4R za Rais samia vs R moja walio ichukua CHADEMA; Mgongano wa mwelekeo

Mr Devil

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2019
Posts
15,410
Reaction score
35,923
Mheshimiwa Rais wa Tanzania na serikali yake walikuja na dhana ya 4R kama dira ya kujenga taifa lenye umoja, maendeleo na demokrasia. Dhana hii ya 4R ilijumuisha:

1. Reconciliation (Maridhiano) – Kujenga mshikamano wa kitaifa na kuondoa migawanyiko ya kisiasa.
2. Resilience (Ustahimilivu) – Kujenga uwezo wa taifa kukabiliana na changamoto kiuchumi, kiafya, na kijamii.
3. Reforms (Mageuzi) – Kufanya mabadiliko ya kisera na kisheria kwa ajili ya kuimarisha utawala bora.
4. Rebuilding (Ujenzi Upya) – Kuimarisha taasisi na uchumi kwa manufaa ya Watanzania wote.

Hata hivyo Chadema wame chukua "R" moja tu REFORMS ambayo mpaka sasa Rais Samia na serikali yake wame shindwa kuifanyia kazi , Sasa kama ameshindwa kudeal na icho kipande kimoja tu kulikua na haja gani ya kuja na zote 4 au hata yeye hajui wala haelewi izo ni nini just tu kaambiwa aziimbe na washauri wake .

Ukosefu wa hatua madhubuti kwenye mabadiliko ya kweli—kama marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa, tume huru ya uchaguzi, na haki ya usawa wa kisiasa—unaashiria ama kushindwa kwa dhamira ya kisiasa au upungufu wa uwezo wa kisera. Kwa hali hiyo, swali linabaki: kama Rais ameshindwa kutimiza hata kipengele kimoja, ilikuwaje akajitwika majukumu yote manne?

 
No reform no election
 
CCM ni matapeli wa kisiasa, dawa yao hakuna mabadiliko hakuna uchaguzi.
 
CCM ni matapeli wa kisiasa, dawa yao hakuna mabadiliko hakuna uchaguzi.
Jeh Unazani mabadiliko yatakuja kwa ku comment mtandaoni ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…