50 Cent ayatosa mabilioni ya Donald Trump

50 Cent ayatosa mabilioni ya Donald Trump

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Rapa wa Marekani Curtis Jackson, maarufu kama 50 Cent, amekataa ofa ya zaidi ya TSh bilioni 8 aliyopokea ili kutumbuiza kwenye kampeni za Donald Trump. Katika mahojiano na Power 105.1 New York, 50 Cent alisema kwamba alialikwa kutumbuiza wimbo wake maarufu “Many Men” kwenye Mkutano wa Kitaifa wa Republican (RNC) Julai 2024, lakini alikataa kutokana na kutopenda kujihusisha na siasa.
1730369282528.png
"Ni kweli nilipokea ofa ya kutumbuiza kwenye mkutano wa kampeni wa Trump kwenye ukumbi wa Madison Square Garden, lakini nilikataa kwa sababu zangu binafsi, hasa mashabiki wangu. Siasa ni hatari; ukiingia, lazima kutakuwa na wanaokupinga," alisema 50 Cent, akisisitiza kuwa dini na siasa ni mambo yanayoweza kugawa mashabiki, kama ilivyotokea kwa Kanye West.
1730369394836.png

Kwa upande mwingine, wagombea wa urais wa Marekani wameendelea kupata sapoti kutoka kwa wasanii maarufu. Kamala Harris anaungwa mkono na wasanii kama Eminem, Beyonce, na Taylor Swift, huku Trump akiungwa mkono na Kid Rock, Amber Rose, na Jason Aldean, miongoni mwa wengine.13:05
 
Back
Top Bottom