50Cent - 21 QUESTIONS, Mike Tee- JE UTANIPENDA& Diamond- UTANIPENDA?



jajajaa!!! you made my morning...those gold days...hapa 50 alitishaa!!!!
 
Mkuu si uweke mashairi ya MIKE TEE hapa ili tuone kama alichoimba diamond ndo kipo huko. Kinyume na hapo unaonekana Mlevi mlevi tu.
Kwa mashabiki wa muziki haya mashairi ni common sana kwao, ila kwa ajili ya wageni wa muziki kama wewe basi yacheki hapa chini.

Kiitikio ? Mad Ice
Je Utanipenda mi nisipong?ara, Je Utanipenda Mi nikiwa Fukara,
Je Utanipenda? Au Ndio Utaniponda?
Je Utanipenda mi nisipikua Star, Siku nimechacha mi Nimekosa Chapaa,
Je Utanipenda? Au Ndio Utaniponda?

Mike Tee,
Yo yo, Yo yo, Bado nina mashaka,
Kila kunapokucha,
Hawa nilio nao iko siku wataniacha,
Wametulia, wameficha makucha,
Nje ni Binadamu kumbe ndani ni ndondocha,
Wananichora, kila ninachofanya,
Nikiwa nao- Hi, Pembeni wananichora,

Si wasichana, si wavulana,
Watoto kwa wazee, mazee kwa vijana,
Niko nao kila siku bega kwa bega,
Hata lafudhi yangu baadhi wameshaiga,
Kila sentensi mwishoni kuweka GA,
Mfano alikula, nasema alikulaGA,

Hata siku za kazi sisi ulabu tu,
Sisi ni raha tu, hatupendi tabu,
Rafiki zangu, kwangu ni ndugu zangu,
Ndio maana nashea nao kila kilicho changu,

Lakini je Tutakua pamoja,
Siku Mike Tee nikianguka moja kwa moja,
Mtani-hug, au mtanitusi,
Na kuniona moyoni mwenu sina nafasi,
Je mtanipa heshima kama zamani,
Kipindi hicho ninang?ara jukwaani,
Mapromota je mtakwenda hewani,
Japo kunisabahi au ndio bye bye

Kiitikio ? Mad Ice
Je Utanipenda mi nisipong?ara, Je Utanipenda Mi nikiwa Fukara,
Je Utanipenda? Au Ndio Utaniponda?
Je Utanipenda mi nisipikua Star, Siku nimechacha mi Nimekosa Chapaa,
Je Utanipenda? Au Ndio Utaniponda?
 
Kuna watu akili zenu finyu sana...... Hivi wewe hujui kuwa hamna jambo jipya chini ya jua? Je unaweza ukanitajia wimbo ambao ni idea ya kipekee dunia nzima😠
 
Kachemka vibaya diamond,kaishiwa,usishangae akaiga chemsha bongo
 
Kwaio huyu Mike T atapata kik sabb ya Platnumz coz hajulikani.
Dah, unamkosea sana Mike Tee aisee. Yaani wewe kuanza kufuatilia muziki wakati Diamond ndio anaimba kusikufanye useme walioimbaga kabla ya hapo hawajulikani. Google hizi ngoma hapa za Mike Tee zilizovuma miaka ya 2003 - 2004 wakati Diamond yuko wapi sijui.

1) Kama (Mike Tee Ningekua Star)
2) Je Utanipenda ft SUGU & Mad Ice
3) Sintobadilika ft Q Chief
4) Nampenda ft Juma Nature
5) Hodi
6) .......
 
Kuna watu akili zenu finyu sana...... Hivi wewe hujui kuwa hamna jambo jipya chini ya jua? Je unaweza ukanitajia wimbo ambao ni idea ya kipekee dunia nzima
Mvua na Jua, Maisha ya Boarding zote za Jay Mo.
Ushawahi kuzsikiaga wapi hizi japo kwa lugha ingine??
 
Mvua na Jua, Maisha ya Boarding zote za Jay Mo.
Ushawahi kuzsikiaga wapi hizi japo kwa lugha ingine??

Ni vigumu kusema nilisikia wapi lkn bila shaka hizo idea ni repeatition tu hamna jipya hapo
 

Nlimxahau hyu jamaa mpaka bac!
 

Kipi kilichofanana zaidi hapo.Tune,Beatz na Melody iz very differ.
 
Kipi kilichofanana zaidi hapo.Tune,Beatz na Melody iz very differ.
Idea Mkuu,
Kwamba kwa sasa mko na mimi sababu tu niko matawi, je siku nikija kufulia still mtakua na mimi??
Bila kusahau JINA LA WIMBO
 
Kama watu humu wamepanic hivi...jamaa katupa jiwe kichakani nini?
 
Ni either hujui muziki au hujui unaongelea nini. Maudhui ya wimbo na kukopi wimbo ni vitu viwili tofauti. Kuna nyimbo zaidi ya laki duniani zenye maudhui ya "utanipenda nikifulia" 50, Mike T na wengine sio wa kwanza au wa mwisho kuimba wimbo wenye maudhui hayo.

Hivi kuna nyimbo ngapi za msanii kuimba jinsi anavyompenda au kumsifia mpenzi wake huko nako ni kucopy au ni maudhui sawa tu!
 
Ally kiba-cinderella
Eminem-cinderella

Nan kamkopy mwenzio hapo mtoa mada, ebu tusaidie na hapo?
 
We umeambiwa ideas we unataja jina kufanana jina sio tatizo tatizo ni maudhui na idea zinafanana wewe gas na mzee wa essay
 
Basi kwa reasoning yako ... chris brown alimuiga Mr blue kwa kuimba Kiss Kiss..??
 
We umeambiwa ideas we unataja jina kufanana jina sio tatizo tatizo ni maudhui na idea zinafanana wewe gas na mzee wa essay

Tuanze na hapa.
-Nini maana ya maudhui?
-Nini maana ya idea?
Halafu zen tuchambue mashairi ya Make Tea na SIMBA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…