52 week saving challenge imeanza tayari

52 week saving challenge imeanza tayari

Me nimeelewa nusu sijaelewa nusu.

Nilichoelewa ni kwamba;
kwa mfano, jumapili ya jana ndio tumeanza kuweka 1000, jumapili inayofuata tunaweka 1000 inakuwa 2000 inayofuata tunaweka 2000 inakuwa 4000, inayofuata tena tunaweka 4000 inakuwa 8000, inayofuata 8000 inakuwa 16000, inayofuata 16000, kila jumapili tunaweka kiasi sawa na kichokuwepo kwenye account

ladyfurahia
Umenielewa tofauti ndugu. Tazama juu hapo nimetoa ufafanuzi kidogo
 
Mkuu idea yako ni nzuri nimeipenda ila naomba nikusahihishe kidogo baada ya kusema kutoa hela m pawa ni bure kwa hili hauko sahihi kumbuka kuwa ukitaka kuweka au kutoa pesa via m pawa ni lazima pesa hiyo ipitie m pesa kwa hiyo ukitaka kuitoa pesa hiyo ni lazima ipitie m pesa ambapo hapo lazima makato yahusike. Kwa hiyo hiyo milioni na point itakayokusanywa kwa mwaka mzima ni lazima makato yahusike utakapotaka kuitoa but all in all idea yako ni nzuri na nimeipenda.
Napokea masahihisho haya.
 
Basi hivi ndio nimeamua kuanza mwaka!

--------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Nimepata hili wazo la kuweka akiba kila wiki kutoka kwa mmoja warafiki zangu anayeishi Kenya. nikajaribu kulifikiria mara mbili mbili huku swali kubwa ikiwa nitawezaje kufikia lengo hili?

Mwisho nikakumbuka ni afadhali anayejaribu na kushindwa kuliko anayekaa kulalamika na kusema siwezi hiki, siwezi kile.

"TUNAWEKAJE AKIBA"

Tulianza jumapili ya kwanza mwaka huu na tulianza na kiasi cha shilingi 1000 na kila wiki tunaongeza 1000 ingine juu ya ile tulioweka wiki iliyopita.

Mfano wiki ya kwanza tuliweka 1000 wiki ya pili tunaweka 2000 wiki ya tatu tutaweka 3000 wiki ya nne tutaweka 4000 hivi ndivyo inavyoenda hadi kufika wiki ya 52 tutakua tumeweka kiasi cha 1,378,000 kwa kila mmoja.

hadi kufikia sasa nimeweza kushawishi baadi ya rafiki zangu 9 ambao tupo nao pamoja tunaendelea na huu mchezo kumbuka leo ni wiki ya 4 hivyo leo tunapaswa kuweka 4000 kwenye akaunti zetu za akiba ikiwa tutafanikiwa kufika mwisho tukiwa pamoja hivi tukichanganya hela hizi (kwa atayependa) tutakua na kiasi cha 12,402,000 ambayo tunaweza kukubaliana kufanya kama mtaji wa biashara yeyote ambayo tutaona inalipa kwa kipindi hicho.

Kila mmoja anatunza hela yake peke yake ili kuepusha kutoaminiana,
Tumeonelea ni rahisi kuweka akiba M-PAWA ya voda kwani hakuna makato yeyote kwa kuweka au kutoa hela. Ukishaweka akiba yako unatuma ile sms ya uthibitisho kwamba tayari umeweka akiba katika kundi tulilolianzisha Whatsapp ili iwe changamoto kwa wale ambao bado hawajaweka waweze kuweka mara moja.

Unaweza kuona mfano wa fomu tunazotumia kutiki kila wiki tukiweka akiba katika picha.

Kama umevutiwa na Idea hii ama una swali lolote unaweza kuniuliza nikakusaidia.

Ahsanteni na karibuni sana.

52 WEEK SAVING CHALLENGE.
--------------------------------------------------------------------------

Naomba Share na wengine pia

View attachment 462515

Nimejifunza sana. Kwamba unaweka kwa kuanza kidogo na week ya 52 ni kama 52000/=

Ni nzuri sana. unakuwa na malengo yanayowezekana kufikika.
 
Me nimeelewa nusu sijaelewa nusu.

Nilichoelewa ni kwamba;
kwa mfano, jumapili ya jana ndio tumeanza kuweka 1000, jumapili inayofuata tunaweka 1000 inakuwa 2000 inayofuata tunaweka 2000 inakuwa 4000, inayofuata tena tunaweka 4000 inakuwa 8000, inayofuata 8000 inakuwa 16000, inayofuata 16000, kila jumapili tunaweka kiasi sawa na kichokuwepo kwenye account

ladyfurahia
so kwa mwezi unaweka ngapi nataka kujua kwa mwezi mmoja tu hapo maana sijaelewa
 
sasa hapa nimekuelewa nilidhani kila wiki unaweka 1000 tu sikuelewa kumbe ndo mtitiriko ulivyo
Sorry for late replay.

Iko hivi ukianza na 1000 utakua unaongeza 1000 kweye hela ulosave wiki iliyopita mfano.

Wiki ya kwanza 1000

Wiki ya pili unaweka 2000 ( utakua na 3000 jumla)

Wiki ya tatu unaweka 3000 (utakua na 6000 jumla)

Wiki ya nne unaweka 4000 ( utakua na 10,000 jumla)

Ndio mtiririko huu kwa wale ambao bado itakua inawasumbua mnaweza kunicheki pm niwape namba tuongee kwa simu. Ahsanteni
 
Back
Top Bottom