5G vs Starlink

Wana latency 25ms sababu ya fiber, tushaongea sana mimi na wewe kuhusu hilo ila vinaingia sikio la huku vinatoka sikio la kule subiri ije hio starlink ujionee mwenyewe. Manake hapa unabishana hadi na Musk mwenyewe na website yake ambaye anaonesha ukanda wetu ping ni 100-150ms.
 
Muda waliopewa unatosha😁 wacha soko liamue sasa.
 
Kwamba unazunguka na dish, waya, power supply router etc kama hivi unakula mishe mishe zako View attachment 3154707
While you get poor latency, poor upload speed, and paying more than 1 million to get it?
Its way more better kuliko kuhangaika na manyaya ya fiber na yale ma antenna ya microwave mnaweka juu ya nyumba...

Mtu unavuta nyaya inatoka posta hadi Mbagala eti internet kama sio upuuzi na hapo unatumia ukiwa nyumbani tu kama upo gerezani...

Hio antenna ni kama laptop tu, utatoka nayo utafika mahala utaitoa utaweka juu ya meza unatumia na kuperuzi safi kabisa..
 
Duh! Mkuu mbona umejibu kwa ukali hivyo?,
 
Hakuna mtu kabisha latency kwa Africa inacheza kwenye 100ms lakini nimesema , fvck latency , sina matumizi na latency ya 30ms , ya nini na itanisaidia nini?

Upload speed una uhakika ni ndogo?
 
Hakuna mtu kabisha latency kwa Africa inacheza kwenye 100ms lakini nimesema , fvck latency , sina matumizi na latency ya 30ms , ya nini na itanisaidia nini?

Upload speed una uhakika ni ndogo?
Upload speed ni ndogo ndio sometime hata 10mbps haifiki, na ping ndio most important thing kwenye internet ndio maana fiber inakuwa rated vizuri.

Ping ya 100ms sahau kuangalia kitu online, kufanya video call ama simu za internet, browsing itakua slow etc
 
Usijali mkuu, inakuja tutawaona na Antena zenu mkitembea, kilo 5 mpaka 10 begani
 
Usijali mkuu, inakuja tutawaona na Antena zenu mkitembea, kilo 5 mpaka 10 begani
Kilio kimesikika.. It’s happening.. StarLink Starlink ni kampuni ya Elon Musk. Inasambaza internet kama zilivyo kampuni za simu au zuku, TTCL na wengineo. Starlink inatumia satellite. Wakitupa Rates Kama za Kenya bei inaweza kua Hivi:
Hardware Kit (Mini) - 560,000 Tsh (Kidishi) - Unaweza connect device 128, na inashika umbali wa mita 112.
Hardware Kit (Normal) - 936,000 Tsh (Kidishi) - Unaweza connect device 235, na inashika umbali wa mita 297.
Pia wana option za kukodisha kile ki dish kwa 40,000 Tshs
Unlimited kwa mwezi 135,000 (Nyumbani)
Unlimited lite kwa mwezi 83,000 (Nyumbani one location)
GB 50 kwa mwezi - 30,000
Options zote zinakupa internet speed ya 50mbps mpaka 220mbps
Unaweza lipia online au kwa mobile money
Ukitaka kununua devices.. Wana distributors wao watatangazwa.
 
Hii ya leo kali, sijui hata kama unaelewa unachoandika...
100ms unasema ni ndogo? Mimi nimetengeneza media server ya kurusha sauti na video live, na ping ikawa 300ms , na inakwenda as if ni real time...

Ping hata iwe 500ms haikuzuii kuangalia video online , 500ms ni ping nzuri tena sana tu hata kwa wanaorusha matukio ya live sports n.k... media kama cnn wanatumia internet siku hizi kuacha satellite kurusha live events kwa ping hizo hizo 300ms hadi 500ms..

Halafu tofautisha latency na speed, how latency itapelekea video kukwama?

Labda kama unatumia UDP protocol, hata UDP bado ina consider 500ms ni ping nzuri tena sana tu, UDP inaweza kwama kabda ping ya 1 sec itaaanza kwaruza...

Https ndio ya kisasa, youtube, netflix n.k wanatumia https ambayo haikwami hata kukiwa kuna loss ya packets inarudi kwenye server na kuchukua packets zilizokosekana...

Ping ya 100ms vide call inakwenda vizuri zaidi ya sana... Na live events unarusha...
 
star link ni ya lini
 
Kuna live video service na service ambazo zina buffer.

Service zote zinazo buffer kaMa youtube Netflix etc hazidhuriwi na latency

Vitu vyote ambavyo ni real time kama video call, kuangalia tv online, kucheza games etc vinadhuriwa na latency

Pia usitupige kamba 500ms ni horrible latency internet inakua kama konokono.

Pia Tofautisha baina ya wewe kutengeneza stream na mtu ku access live stream ni vitu viwili tofauti visivyo na mahusiano.
 
Bongo 4g Tu ya kutaftiza, mara mtandao ukate siku nzima😩

Sisi watumiaji tunaomba tujaribu na star link..
 
Sijajua rates za Starlink zitakuwa ni ni kiasi gani wakishaanza hapa, ila rates kwa nchi za wenzetu. Ni ghali zaidi ya bei za bundle tunazonunua hapa.

Mfano 50GB ni dola 50 ambayo hapa mjini kwa $50 ninapata unlimited fiber internet ya Vodacom. Netsolution fiber internet unlimited napata kwa 69k

Starlink hautakuwa mtandao wa kila mtu. Wako expensive unless waje na special package ya Kwetu huku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…