joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Usituchekeshe kwa sauti asubuhi hii, unasema baada ya kumaliza mlichokifuata Somalia mkaombwa kujiunga na AMISOM?, hicho ni kichekesho. Kiukweli baada ya ninyi kuingia Somalia, Alshaabab ndio waliongeza mashambulizi dhidi ya Kenya mara kumi zaidi ya kabla hamjaenda Somalia, usalama wa Kenya ulizidi kudorora, hadi leo usalama Kenya haujatengemaa, hasa maeneo ya pwani. KDF wamekuwa wakishambuliwa sana huko Somalia kuliko jeshi lolote huko Somalia, baada ya kugundua mnazidiwa na Alshaabab, ndio mkaona bora muunganishe na majeshi mengine ili mpate msaada ukiwemo wa pesa toka UN.
Ukweli ni kwamba mlisaidia adui wetu sometimes in the past, hata kama jumuia ya East Africa ilivunjika, hiyo haikuwa sababu ya ninyi kumsaidia adui yetu kwasababu sisi na ninyi hatukua maadui, hivi kama Idd Amini angetushinda leo mngeweza kutuomba tuwasidie huko Somalia?, rafiki wa adui yako, pia ni adui yako, Kwetu sisi Kenya na Idd Amini wote ninyi ni maadui zetu.