Mdude_Nyagali
Member
- Dec 11, 2022
- 79
- 1,444
Mnano karne ya 4 kabla ya kuzaliwa Yesu Kristo kulikuwa na mamilion ya wayahudi waliochukuliwa mateka wakati wa utawala wa Babel (Iraq ya sasa) chini ya mfalme Nebukadreza. Wayahudi hao walikuwa wametapakaa nchi zote za mashariki ya kati wakitumikishwa kazi mbalimbali. Hata baada ya ufalme wa Babel kuanguka na kuingia Umedi & Uajemi ( Iran ya sasa) wayahudi wengine walibakia baadhi ya nchi za mashariki ya kati kama watumwa na wakimbizi.
Sasa huko Uajemi (Iran ya sasa) kulikuwa na waziri mkuu mmoja anaitwa Hamani. Huyu alimshawishi mfalme Ahasuero kutaka wayahudi wote wanaokaa kama wakimbizi na watumwa katika nchi hiyo wauawe kwa sababu wawazishiki sheria za mfalme huyo. Baada ya mfalme kukubali ombi la waziri mkuu wake, wayahudi wote walioishi katika nchi hiyo walihuzunika sana.
Lakini palikuwa na mtu mmoja aliyeitwa Mordekai jasusi aliyeweza kumbadilisha mjomba wake aliyemlea jina kutoka Hadasa jina la kiyahudi na kumpa jina kiajemi la Esta ili tu asijulikane ni myahudi aolewe na mfalme Ahasuero. Huyu Mordekai aliposikia mbiu ya wayahudi wote wanatakiwa kuuawa alizirarua nguo zake na kuvaa magunia kisha kwenda kukaa kwenye malango ya ikulu. Lengo la jasusi huyu Mordekai lilikuwa kwamba wasaidizi wa Esta ambaye wakati huo alikuwa malkia wakimuona katika hali hiyo watamwambia Esta na Esta atakuja kumuona kwa dharura.
Ni kweli Esta alionana na mjomba yake huyo Mordekai na akaambiwa kwamba waziri mkuu Hamani ametangaza wayahudi wote kuuawa. Japokuwa Esta asingeuawa kwa sababu hakujulikana kuwa ni myahudi baada ya mjomba wake kumbadilisha jina na kuwa mke wa mfalme, lakini Esta alipiga ukunga na kulia kilio kikuu. Damu ni nzito kuliko maji. Baada ya hapo Esta alimwambia mjomba wake Mordekai akawaambie wayahudi wote wafanye maombi kwa ajili yake ili apate kibali cha kwenda kumuona mfalme mume wake kwa dharura na kumshawishi mfalme afute mpango huo. Esta alisisitiza maombi yawe ya kufunga wala wasile na kunywa kwa siku tatu.
Hatimaye baada ya maombi siku ya nne Esta alienda ofisini kwa mfalme bila kibali na kumlilia. Mfalme akafuta mpango huo akaamuru waziri mkuu Hamani anyongwe hadharani mbele ya Umma. Huo ulikuwa ushindi wa wayahudi wakiwa katika nchi ya ugenini.
Sisi Watanganyika hatupo ugenini kama wayahudi bali tupo katika nchi yetu ambayo Mungu alitupa japo tunaishi kama tupo ugenini. Mamia ya wenzetu wanaharakati na wasio wanaharakati, wanasiasa na wasiokuwa wanasiasa wanatekwa na kupotezwa na watawala. Sisi hatuna bunduki wala mabomu ya kujilinda kama wao , isipokuwa tunaye Mungu ambaye anaweza kutushindia .
Hivyo basi tunawaalika katika maombi ya kitaifa yatakayofanyika siku ya jumapili tarehe 8 September 2024. Tunawaalika wote wakiwemo viongozi wa dini katika maombi haya. Sisi hatutavaa magunia kama Mordekai isipokuwa tutavaa nguo nyeusi kuashiria nchi ina msiba. Nenda katika ibada msihi mchungaji wako, Padri ama Askofu kwamba tunaomba dakika 5 za kuwaombea waliotekwa na hatujui huko waliko wako katika hali gani. Tunawaomba viongozi wa dini muwape ushirikiano watu watakaofika katika nyumba za ibada kwa ajili ya maombi haya.
Hatutakula wala kunywa kuanzia saa 06:00 Asubuhi ya siku hiyo mpaka saa 18:00 jioni ya siku hiyo. Tutahitimisha maombi haya katika mtandao wa 𝗖𝗹𝘂𝗯𝗵𝗼𝘂𝘀𝗲 katika room ya 𝗦𝗮𝘂𝘁𝗶 𝘆𝗮 𝗪𝗮𝘁𝗮𝗻𝘇𝗮𝗻𝗶𝗮 kuanzia saa 18:00 jioni.
Soma Pia: Special Thread: Taarifa za Watu waliopotea au kuchukuliwa na “Watu Wasiojulikana”
Mungu hashindwi.
Amen.🙏🙏
Sambaza ujumbe huu kwa watu wote wakiwemo viongozi wa dini.
Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.