80% ya magonjwa yanayosababishwa na viini (vijidudu) husambazwa kwa njia ya mikono

80% ya magonjwa yanayosababishwa na viini (vijidudu) husambazwa kwa njia ya mikono

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Karibu 80% ya magonjwa yanayosababishwa na viini husambazwa kwa njia ya mikono kwa mujibu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa Nchini Marekani (Centers for Disease Control and Prevention - CDC).

Ni kwanini vimelea ni viumbe hatari sana?
Kiini ni kiumbe kidogo sana kinachoweza kusababisha magonjwa au ugonjwa. Vimelea wanaweza kuingia mikononi mwako baada ya kutumia choo, kubadilisha nepi (diaper), kukata au kushika nyama mbichi, au kugusa kitu chochote chenye vimelea.

Wakati haunawi mikono kwa sabuni na maji safi yanayotiririka viini vya magonjwa kama vile virusi na bakteria huweza kusambaa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine, na bila shaka usingependa kuugua.

Ukweli ni kwamba baadhi ya magonjwa yanayosambazwa kwa mikono michafu yanaweza kuwa mabaya zaidi.

Pia watu wengi wanaougua, hupewa dawa za kukabiliana maambukizi (antibiotics) ambazo mara nyingi sio muhimu.

‘’Kadri unavyotumia dawa za maambukizi ndivyo unavyojenga kinga dhidi yake na hivyo hazitafanya kazi ya kupambana na maambukizi utakayoyapata tena’’ Aliiambia BBC, Dkt Timona Obura wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan mjini Nairobi.

Magonjwa yanayosambazwa kupitia mikono
Kulinganana Dkt. William Sigilai wa Hospitali ya Rufaa ya Kenyatta Mjini Nairobi kuna magonjwa mbalimbali yanayosambazwa kupitia mikono, yakiwa ni yale ya tumbo kama vile homa ya tumbo (Typhod), na kipindupindu yanayosababisha kuhara na kutapika.

Mengine ni yale yanayoshambulia mfumo wa kupumua kama vile homa ya mafua ya kawaida, mafua (Influenza), Covid na kifua kikuu.

Dkt. William Sigilai anasema: “Watu wanapaswa kunawa kwa maji safi na vitakasa mikono (sanitizer) hasa wanapotumia choo, kabla ya kupika chakula ili kuepuka viini vya magonjwa kusambaa kwa watu wengine.”

Unapopiga chafya au kukohoa na kuweka mkono wako kwenye kinywa na kisha unasalimiana na watu au unashika kwenye maeneo mbalimbali bila kunawa viini vinasambaa kwa watu wengine utakao wasalimia au watakaogusa eneo uliloligusa… hivyo kudumisha usafi wa mikono ni muhimu.

Licha ya hayo na magonjwa mengi yatokanayo na maambukizi ya macho na ngozi.

Viini hatari vinavyosambazwa kwa mikono yetu:
Kiini kimoja kinaweza kuzaa zaidi ya viini milioni 8 kwa siku
Karibu 80 ya magonjwa yanayosababishwa na viini husambazwa kwa njia ya mikono
Rimoti unayoitumia kutazama TV hubeba bakteria zaidi kuliko vifaa vingine vya nyumbani
Kuna viini zaidi kwenye simu yako ya mkononi, keyboard kuliko kiti cha choo (toilet seat).
Mtu mmoja kati ya watu watano hawanawi mikono yao na kati ya wale wanaonawa mikono yao, ni 30% pekee wanaotumia sabuni mara kwa mara.
Wakati unapo flash maji chooni, viini vinaweza kupaa futi 6 juu


Njia bora ya kunawa mikono yako
Lowesha mikono yako, paka sabuni
Fikicha mikono pamoja mpaka povu jingi la sabuni
Safisha maeneo kuanzia kwenye vidole na chini ya kucha hadi juu ya kiganja na kisha nyuma ya kiganja
Sugua kwa walau sekunde 20
Fungua tena maji na isuuze vizuri mikono yako
Kausha mikono yako na taulo safi au kitambaa na utumie kitambaa au taulo kufunga bomba la maji


Chanzo: BBC
 
Back
Top Bottom