90 Minutes in raid on Entebbe: Tukio la ukombozi wa mateka wa Israel Nchini Uganda - THUNDERBOLT

donlucchese

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2011
Posts
17,128
Reaction score
21,885
Operation Entebbe was a counter-terrorist hostage-rescue mission carried out by commandos of the Israel Defense Forces (IDF) at Entebbe Airport in Uganda on 4 July 1976. A week earlier, on 27 June, an Air France plane with 248 passengers was hijacked, by members of the Popular Front for the Liberation of Palestine and the German Revolutionary Cells, and flown to Entebbe, the main airport of Uganda.

The local government supported the hijackers and dictator Idi Amin personally welcomed them. Sasa hapo ndipo kilinuka baada ya israel kutuma makomandoo wao kuja kupiga moja ya greatest hostage rescue in the history.

Hii hapa documentary inayoelezea bayana nini kilichojiri katika operation hiyo:


Jenerali Idd Amin Aliporatibu Ugaidi Wa Kimataifa Akiwa Kampala..( Uchambuzi)
Ndugu zangu, Waziri Mkuu wa Israel , Benjamin Netanyahu ametua leo uwanja wa ndege wa Entebbe.

Netanyahu yuko Kampala Uganda kushiriki kusanyiko la wakuu wa nchi saba za Afrika kujadili masuala ya usalama ikiwamo mapambano dhidi ya ugaidi. Ni kwenye uwanja wa Entebbe, takribani miongo minne iliyopita, kaka yake Benjamin Netanyahu, aliuawa mahali hapo. Ni kwa nini?

Nitakumbushia hapa, tukio la utekaji wa ndege ya abiria ya Ufaransa iliyokuwa na abiria wengi wa Kiyahudi. Na mmoja wa wahusika wakuu katika tukio hili la kigaidi alikuwa Jenerali Idd Amin Dadah wa Uganda.

Ndio, licha ya Jenerali Idd Amin kuendesha ugaidi wa dola kwa maana ya State Terrorism, kwenye tukio hili, Jenerali Idd Amin alishiriki rasmi kwenye Ugaidi wa Kimataifa. Maana, tukio lile la utekaji ndege lilianzia Ulaya, likaambaa Mashariki ya Kati na kumalizikia kwenye ardhi ya Uganda. Ni kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe huku Idd Amin mwenyewe akishiriki kuratibu harakati za kigaidi.

Maelezo marefu juu ya sakata ya Entebbe yanasimuliwa kwa umahiri mkubwa na mwandishi William Stevensson katika kitabu chake cha (90 Minutes At Entebbe), Yaani Dakika 90 katika Entebbe.

Ndege hiyo ilitekwa nyara Juni 27, 1976 mara ilipoanza kurukakutoka uwanja wa ndege wa Athens nchini Ugiriki kuelekea Tel Aviv. Miongoni mwa watekaji nyara, walikuwemo Wapalestina, lakini raia mmoja wa Ujerumani naye alishiriki utekaji huo. Mjerumani huyo alikuwa ni mfuasi wa kikundi cha kigaidi cha Ujerumani kulichojulikana kama ”Baader-Meinhof.”

Inasadikiwa, kuwa Dr. Wadi Hadad, mwanaharakati na Kiongozi wa chama cha ukombozi wa Wapalestina cha PFLP (Popular front For Liberation of Palestene) alishiriki kwenye kupanga kazi hii ya kigaidi. Bila shaka, inaaminiwa pia, kuwa aliyekuwa gaidi nambari moja wakati huo, Ramirez Carlos, ambaye pia alijulikana kama ”The Jackal”, alikuwa na mkono wake kwenye kazi hiyo.

Baada ya kutua na kujaza mafuta Tripoli , Libya, ndege hiyo iliendelea hadi Uganda na kutua Entebbe.

Wakati huo Idd Amin alishakorofishana na maswahiba wake Waisrael na kutangaza kuunga mkono harakati za
Wapalestina kuikomboa nchi yao. Kuna wakati, Idd Amin alishawahi kutamka, kuwa anawaandaa askari wake kwenda kushiriki mapambano ya kuwandoa Wayahudi kwenye milima ya Golan waliyoiteka toka kwa Wapalestina. Na Idd Amin alishaviamrisha vikosi vyake kufanya mazoezi ya kivita kujiandaa na operesheni ya kuikomboa milima ya Golan.

Naam, ndege ilipotua Entebbe, abiria wote walikaribishwa na Idd Amin mwenyewe. Siku mbili baadae, watekaji nyara walianza kutoa madai yao; walidai mateka wangeachiwa huru kama idadi kubwa ya wafuasi wa vikundi kadhaa vya kigaidi wangeachiwa huru kutoka kwenye magereza ya Ulaya na hata Afrika.

Ni katika tukio hili la utekaji nyara ndege ambapo kwa kiasi fulani mateka walihisi kuwepo kwa tumaini la kukombolewa. Ni kwa vile maofisa wengi wa jeshi la Israel wamefanya kazi Uganda ikiwemo kutoa mafunzo ya kijeshi. Na kama kuna watu duniani waliokuwa wakimjua vema Idd Amin ikiwemo uwezo wa jeshi lake, basi, watu hao ni Waisrael. Maofisa wengi katika jeshi la Idd Amin walipata mafunzo yao ya kijeshi Israel.

Kabla ya operesheni hiyo iliyopewa jina la Thunderbolt kuanza, Mossad, Shirika la Ujasusi la Israel, liliamua kumtumia Jenerali wake mstaafu aliyeitwa Chaim Bal Lev. Bwana huyu alikuwa ni rafiki mkubwa na wa siku nyingi wa Jenerali Idd Amin. Wawili hawa walifanya mazungumzo ya muda mrefu na ya kirafiki kwa kutumia simu. Waliongea karibu siku zote kabla ya mateka kuokolewa.

Kwa kumtumia Jenerali huyu rafiki wa Amin, Waisrael walikuwa wanaiba muda ili kujiandaa zaidi, na vile vile kujaribu kumshawishi Amin asiwadhuru mateka hao na pengine kuwaachia huru. Hata kama majasusi ya Kiyahudi walikuwa na michoro yote ya uwanja wa Entebbe ambao waliuchora wenyewe na kuujenga, lakini, kazi ya vikosi vya Israel kutua Entebbe haikuwa rahisi sana.

Hawakuwa na hakika ya ukubwa wa vikosi vya Amin uwanjani hapo. Walitegemea zaidi, ufahamu wao wa uwanja wa ndege wa Entebbe. Maana, ni Waisrael waliojenga uwanja huo. Kutoka Tel- Aviv hadi Entebbe ni mwendo wa takribani saa nne kwa ndege.

Uganda na Israel wamekuwa na mahusiano mazuri ya muda mrefu. Mahusiano hayo yangalipo hadi hii leo. Ni kutokana na sababu za kihistoria. Kabla ya Jumuiya ya Kimataifa kupendekeza makazi ya Wayahudi waliokuwa wametapakaa dunia nzima yawe katika Israel ya sasa, nchi ya Wapalestina, kulikuwepo na wazo la Wayahudi kutafutiwa makazi mapya katika nchi ya Uganda. Mpaka miaka ya karibuni, nchi pekee ya Kiafrika ambapo raia wa Israel hakuhitaji kuomba viza ni Uganda. Raia wa Uganda pia hawakuhitaji pia kuomba viza ya kuingia Israel.

Tukirudi kwenye tukio lile la utekaji ndege. Kwa haraka, Waisrael waliendesha operesheni ambayo si rahisi kusadikika. Makomandoo wa Israel waliruka kwa ndege kubwa kutoka Tel-Aviv kuelekea Entebbe. Ndege yao ilitua saa sita na dakika moja usiku kwenye pembe ya mbali ya Uwanja wa Entebbe. Taa za ndani na nje ya dege lile kubwa zilizimwa wakati ndege ilipoukaribia uwanja wa Entebbe ikiwa na mwungurumo dhaifu. Mwungurumo usiosikika kwa mbali.

Waisarel walikuja na ndege mbili, moja ilibaki Nairobi ikiwa na vifaa vya tiba na vingine muhimu. Iliyotua Entebbe ilibeba gari mbili, Landrover na Mercedes Benz nyeusi. Gari hizo zilitumiwa na makomandoo wa Kiyahudi kufika kwenye jengo walilokuwamo mateka. Waliwakuta mateka wote na wateka nyara wakiwa katika ukumbi wa mapunziko kwa abiria.

Amri ilitolewa kwa lugha ya Ki-hebrenia ikiwataka Wayahudi wote wajilaze chini mara moja. Wote waliobaki wamesimama au kuinama kwa kusitasita, hawakupata sekunde zaidi za kutafakari. Risasi za makomandoo wale ziliwamiminikia miilini mwao.

Operesheni ya kikomandoo iliyochukua takribani dakika tisini pale Entebbe iliwaacha watekaji nyara saba bila uhai. Idadi ya askari wa Amin takribani ishirini nao waliuawa pale Entebbe. Mateka wotewalikombolewa isipokuwa mama wa miaka 75 Dora Bloch aliyekuwa hospitalini Mulago, Kampala.

Inasemekana, kuwa mateka huyo akaja kuuawa na Idd Amin mwenyewe.Habari hiyo haijathibitishwa.

Kwa upande wao, Makomandoo wale wa Kiisrael walimpoteza Kanali Yoni Netanyahu. Komandoo yule aliuawa kwa kupigwa risasi ya usoni na askari mmoja wa Idd Amin. Miaka ishirini baadae, kaka wa Yoni Netanyahu akaja kuwa Waziri Mkuu wa Israel na ambaye ni Waziri Mkuu wa Israel wa sasa, jina lake ni Benjamin Netanyahu, ambaye leo ametua Entebbe Airport.
Huu ni Uchambuzi Endelevu..


 
Last edited by a moderator:

Impressive and very interesting! These guys are very intelligent!
 
Last edited by a moderator:
Sante kwa hii picha maani nilikuwa niisikia tu ngoja nijione kwanza.
Nalog off
 
1976 watu walikuwa hawana vifaa vya kisasa mbona wameshindwa Westgate Mall kuokoa watu.
 
Tulikuwa na kitabu home kina kichwa cha habari 90 minutes AT Entebe na si IN Entebe, just google you will see

Daaah mkuu sasa in na at tu ndio tatizo? Iyo ni grammatical error ya kawaida!
 
The documentary is not saying anything about the mastermind of the whole plan the brave commander Yonatan
Netanyau!
He was the genius of the whole plan. Unfortunately he was killed by a Ugandan sniper who was also killed during the last minutes of the rescue mission!!The whole story is here Lt. Col. Jonathan (Yoni) Netanyahu official memorial web site - The Entebbe Rescue (Jonathan Operation) - Page 2
 
Last edited by a moderator:
Donluchesse kuna watu unawaumiza sana kwa kuwaonyesha uwezo wa Taifa la Kiyahudi wao wanataka uwasifie Al Shabbab, Osama, Hamas, nk. Ila ukweli utabaki hivyo kua The State of Israel will keep knocking their unrealistic wishes to ashes.
 
Yeah hii mission ilikuwa ya ukweli sana. Hivi wamarekani washawahi kutekewa ndege wakaenda okoa hostages nchi yoyote? Au waishia kutengeneza movies tu za missions kama hizi?
 
Donluchesse kuna watu unawaumiza sana kwa kuwaonyesha uwezo wa Taifa la Kiyahudi wao wanataka uwasifie Al Shabbab, Osama, Hamas, nk. Ila ukweli utabaki hivyo kua The State of Israel will keep knocking their unrealistic wishes to ashes.

I second you bro!! Long live the State of Israel! The blessed one!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…