BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mwenyekiti wa jumuiya ya wakulima wa parachichi Tanzania (ASTA), Rebeca Hesewa amesema changamoto inayowakabili wakulima kunufaika na masoko ya nje ni kukosekana kwa ubora wa mazao wanayozalisha.
Kukosekana kwa ubora huo, alisema kunatokana na aina ya viuwatilifu wanavyotumia wakati wa uzalishaji ambavyo alibainisha asilimia 90 vilivyopo katika soko la Tanzania havifai.
“Hii inatusababishia tunazalisha maparachichi yenye sumu ambayo hayakidhi vigezo vya masoko yote hata la ndani, ingawa hapa nchini tunakula kwa kuwa hatuna vipimo vya kubaini sumu, lakini ukipeleka nje hayatakiwi,” alisema.
Ili kukabiliana na hilo, Rebeca aliiomba Serikali ielekeze nguvu kuelimisha wote wanaohusika katika mnyororo wa thamani wa zao hilo, ili kuwa na mazao yanayokidhi vigezo vya kusafirishwa kwenda katika masoko ya nje.
Mwenyekiti huyo alieleza kufanya hivyo kutasaidia kulilinda soko hilo, kwani ukibainika udhaifu wa zao linalotoka katika nchi fulani, kuna hatari ya kufungiwa kusafirisha tena. Hata hivyo, alieleza kuridhishwa na juhudi zinazofanywa na Serikali kusaka masoko hayo, akisema yanaongeza hamasa kuzalisha zaidi.
Alisisitiza utafutaji masoko hayo uende sambamba na uelimishaji wakulima mbinu za kuvifikia vigezo vya masoko ya kimataifa, ili wanufaike nayo.
MWANANCHI