A best way foward: Kwa yanayotokea na hatari iliyopo mbele yetu, tufanye haya kulikomboa Taifa letu.

Lord denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
15,819
Reaction score
33,255
Kwa wenye akili, dalili si nzuri kuhusu mustakabali wa Taifa letu katika miaka michache ijayo.

It's obvious, tumezidiwa nguvu na maadui watatu aliotutangazia Mwalimu nyerere hasa ujinga. Kushindwa kupambana vizuri na adui ujinga kumeliweka Taifa letu kwenye hatari ya kupotea na kuangamia.

Kukosekana kwa Think Tanks sahihi wanaopanga na kusimamia mipango sahihi ya kuliweka Taifa letu mbele kwenye dunia hii ya ushindani na pia kuongezeka na watu wasiofikiri sawa zaidi ya kuwaza kujipendekeza, kupata vyeo, kusufia ( kuwa chawa) ili wawe na maisha mazuri na wapate hela ni hatari nyingine kubwa iliyolikumba Taifa letu ambayo vyovyote vile, ni lazima ishughulikiwe ipasavyo.

Nchi kuamuliwa mustakabali wake na Wanasiasa ambao kwa bahati mbaya wamekuwa ni watu wanaowaza madaraka na kujinufaisha binafsi zaidi kuliko maendeleo ya watanzania wote ni hatari nyingine iliyolikumba taifa letu. Siku zinavyozidi kwenda kwa kutumia ujinga wa watu wetu ikiwemo kwenye vyombo vya ulinzi na usalama, Wanasiasa wamekuwa wakitengeneza Empire yao ambayo kiuhalisia inatishia usalama na mustakabali mwema wa Taifa letu katika siku zinazokuja.

Wanasiasa wamekuwa wakitumia nguvu zao kuteua katika nafasi za juu za utendaji watu wasio na uwezo ili mradi wanasema ndio kwao na hawawapingi katika ujinga wao, na hili limeanza kutugharimu maana watu hawa wasio na uwezo sahihi wanarigharimu Taifa kwa kushindwa kusimama vizuri kukabiliana na maadui wa ndani na nje. Watu hawa wameshindwa kusimamia na kupanga mipango sahihi ya kulifanya Taifa hili kufanya vizuri na kuongoza vizuri katika nyanja za kiuchumi na kimaendeleo.

Ukiacha hao maadui wa ndani nchi yetu pia saivi imezidi kuwa vulnerable kwa maadui wa nje kutokana na udhaifu wa ndani. Tumeona udhaifu wa ndani ulivyolifanya Taifa letu kushindwa kusimamia na kupoteza nafasi yake ya ushawishi kisera na kidiplomasia katika Ukanda huu wa Maziwa Makuu.

Nchi yetu kuzidi kupoteza ushawishi wake katika maziwa makuu kumeanza kuifanya nchi yetu kuendelea kuwa kwenye hatari zaidi ya kuingiliwa na maadui wa nje. Tetesi za watu wasio raia kuingia zaidi kwenye mifumo yetu ya Uongozi na Utawala sio tu kunatufanya kuwa weak ila kunafanya maadui wa nje kutujua inside out kiasi cha kuweza kutufanyia chochote kile wakati wowote ule.

Sio hivyo tu Jeshi letu la Wananchi kufeli kwenye mission yake ya Congo ni taarifa mbaya zaidi inayopaswa kutufanya kurudi kwenye ubao wa mipango na kujipanga upya huku tukijitafakari vizuri.

Ili kulikomboa Taifa letu ambalo kiuhalisia sasa liko kwenye hatari ya kuangamia, inabidi Watanzania wote haijalishi walio kwenye vyombo vya ulinzi na usalama au wananchi wa kawaida tukubaliane yafuatayo.

1. Ni muhimu sana tufanye mchakato wa kutengeneza Katiba Mpya. Katiba itakayoweka nguvu kwenye mifumo na sio Wanasiasa.

2. Vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama vijitenge kabisa na Wanasiasa pamoja na Siasa za Nchi. Vyama vya siasa viishie kuwa vyama vya siasa tu na vipambane vyenyewe katika majukwaa ya siasa. Vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama vijikite kwenye masuala ya Taifa tu na strategies za kulilinda na kuliimalisha Taifa kiuchumi, kiusalama na kimaendeleo.

3. Utumishi wa Umma usijihusishe vyovyote vile na Wanasiasa. Uteuzi wa Makatibu Wakuu na Watendaji Wakuu ufanywe na chombo maalum na watu hawa wapatikane kupitia uahindani na mchujo unaotizama na uwezo, uzoefu na weredi. Uteuzi wa Wakuu wa Mashirika na Wakurugenzi ufanye pia kwa njia ya ushindani kwa kuzingatia Uwezo, Uzoefu na Weredi.

4. Vyovyote vile siasa za nchi zisiruhusiwe kuingilia mipango ya maendeleo ya Taifa. Watendaji wa Serikali ( Umma) wawe na nguvu ya kusimamia na kutekeleza mipango ya maendeleo yq kitaifa bila kuingiliwa vyovyote vile na Wanasiasa.

Cc. Bams benjamin Netanyau Tindo Mshana Jr Erythrocyte
 
Moderator kama mna mfumo wa uzi kuwa pinned, naomba uzi huu uwe pinned kwenye profile yangu.

This is my best thread!
 
Ramli zilianza march 2021 ,mnazidi tuu kusogeza tarehe mbele 🤣🤣

Tutafika 2030 Bado mnapiga ramli 😂😂
 
Back
Top Bottom